Picha: Mwigulu Nchemba aitesa CHADEMA Iramba, mikutano yao yadoda haijawahi tokea

Taswira

JF-Expert Member
Sep 23, 2012
1,198
447
WAKUU,
Naomba kuwaletea sehemu ya picha za mikutano ya hadhara ya CHADEMA inayoendelea jimboni Iramba Magharibi kwa yule Mbunge anayewakosesha usingizi chadema Taifa,mkoa,wilaya,tawi na wanachama wake kila iitwapo leo Mh.Mwigulu Lameck Nchemba.

Ikumbukwe CHADEMA walitangaza kuweka kambi ndani ya jimbo hilo kwa lengo ya kuimarisha chama na kubomoa umwamba wa Mh.Mwigulu nchemba wa kisiasa ndani ya jimbo hilo(Thread ipo hapa JF).Bila ajizi chama hicho kimeweka kambi ambayo inaelekea kumaliza wiki sasa ndani ya jimbo la Mh.Mwigulu NChemba,kambi yao ikiwa na msafara wa gari moja ya chama M4C na Noah ya mwanachama mmoja wa singida.
Mikutano yao imeendelea kudoda kiasi kwamba mkutano kuhudhuriwa na watu 10 au 20 ni jambo la kawaida.
Ni wazi Mwigulu ni maji marefu sana kwa chadema,kwa namna Mh.huyo alivyojiimarisha kisiasa na kiutendaji ndani ya jimbo lake ndio matokeo ya chadema kupata watu 10 au 20 kwenye mikutano yao.Aidha wananchi wengi wameonekana wakiendelea na kazi zao za kila siku pembeni mwa mikutano ya chadema as if hakuna kinachoendelea kwenye eneo hilo.Matunda ya maendeleo imara ya umeme,barabara,maji,afya,elimu n.k yanayofanywa na Mh.Mwigulu Nchemba kila pembe ya jimbo hili inatajwa ndio sababu pekee ya wananchi wa iramba kuchana nakwenda kusikiliza mikutano ya chadema.

Chadema kupitia uongozi wa juu wa chama na bavicha waliweka kikao cha kuhakikisha wanafika jimboni kwa Mwigulu nchemba kwa ili waweke kambi ya kujenga chama na kutikisa mbunge huyo kisiasa.Lakini hali halisi ndio hii hapa chini kwenye picha ambapo ni aibu tupu kwa chama kikubwa kama chadema kupata watu 10 au 20 kwenye mkutano wa hadhara.Taifa linatambua wazi kuwa nchi hii kwa sasa MWIGULU NCHEMBA ndiye mwiba na msumari wa moto kwa chadema,bungeni na hata kwenye majukwaa ya kisiasa.
Jambo hilo linawafanya chadema wapagawe namna ya kumshughulikia Mbunge huyo,kila wanapopanga wanakwama kutokaa na kuzidiwa ujanja na Mh.Mwigulu Nchemba.
Nilipomuuliza Mh.Mwigulu anazungumziaje kambi ya chadema jimboni kwake alisema"Acha wapoteze muda,lakini mwaka ujao wa uchaguzi mgombea wa chadema akipata kura nusu ya kura zangu nitaandika barua tume ya uchaguzi imutangaze mshindi wa uchaguzi huo"Mwigulu Nchemba
Picha zaidi zitawajia kadri ninavyoendelea kuhudhuria mikutano ya chadema hapa Iramba.USHAURI WA BURE,Chadema na gari lao la M4C wageuze DSM waka kae tena kikao namna ya kupambana na Mh.Mwigulu la sivyo ipo siku watajikuta wanahutubia viti hapa Iramba.
1174444_336918299777845_1563010488_n.jpg
Moja wa makamanda wa chadema ambaye ni kiongozi wa chama kiomboi akikomaa kuongea na wananchi wachache waliojitokeza kwenye mkutano wa chama chao jimboni Iramba
1278231_336919233111085_1802697360_n.jpg
Mkutano unaendelea hapa,watoto na vijana wachache wamejitokeza kusikiliza mkutano wa chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA


photo.php
Ni kwenye kata ya Jesca Kishoa,wananchi kiduchu wakisikiliza mkutano wa hadhara huku gari ya chadema ikiwa imepaki bembeni yake



Sehemu ya makumi ya watu wakisikiliza mkutano wa CHADEMA jimboni Iramba kwa Mh.Mwigulu NChemba(CCM)










 
Tuwasaidie Wazee wakatibiwe India...... Hapana. Tujenge hospital zetu watibiwe hapa hapa Tanzania.

 
Last edited by a moderator:
Tambua kuwa mapinduzi yanaanza kwa mmoja. Hata kama hoja hii ni kweli, mimi sina shaka kabisa. Nafurahia mapinduzi haya.
 
Tambua kuwa mapinduzi yanaanza kwa mmoja. Hata kama hoja hii ni kweli, mimi sina shaka kabisa. Nafurahia mapinduzi haya.

ni kama fisi kusubiri mkono wa binadamu uanguke,utasubiri sana
 
Arsenal wamemsajili ozil kwa hela nyingi wamevunja record yao...hongera wenger
 
Nyie mnaomkalia kikao kila kukicha,na kuwaagiza wabunge wenu wasisalimiane naye ndio mnamuogopa ni balaa
Kuna haja gani ya kusalimiana na Mla nyama za watu, mmwaga damu! anaweza kukutia najisi bure. akafie mbali
 
naomba namba ya m pesa nitoe mchango wa matibabu ya mzee wa Hamisi kigwangala
 
Nyie mnaomkalia kikao kila kukicha,na kuwaagiza wabunge wenu wasisalimiane naye ndio mnamuogopa ni balaa

Yani ulivyokuwa elton John unatoa hoja ambazo zinaonyesha kabisa umetumwa au yawezekana ni Mwigulu mwenyewe. na hasa kwenye hayo maneno niliyo-bold kwa red colour. Au ama sivyo hii account itakuwa inamilikiwa na mke wa Mwigulu anayejua mpaka siri hizi.
 
Aaaha haha chadamu mujipangee maana Mwigulu yuko kamili so endeleen kumuamsha simba huku mukivaa earphone
 
Arsenal wamemsajili ozil kwa hela nyingi wamevunja record yao...hongera wenger

Mimi ni mpenz wa Arsenal ila wasiwasi wangu ni kwamba Ozil anaweza ku-maintain kiwango chake pale arsenal, kwani naona kama vile wenger amefikia mwisho kwenye uwezo wa kufundisha.
 
Back
Top Bottom