Mrembo huyo akishushwa kwenye lori la Manispaa
Mrembo huyo akipelekwa eneo la makaburi ya Manispaa
Mwili wa Mrembo huyo akiingizwa kwenye kishimo hicho chembamba
marmbo huyo akitumbukizwa kwa shida kwenye kishimo chembamba,mbali na mrembo huyo kuwa na mwili mkubwa lakini pia baada ya kukaa kwa muda mrefu kwenye majokovu wa Mochwari mwili wake ulizimba sana.
Wafanyakazi wa manispaa kitengo la makaburi,wakimfukia mrembo huyo kwenye makabuli ya manispaa leo asubuhi.
LICHA ya kuhifandhiwa kwenye majokofu ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa siku 20 akisubiri kutambuliwa na ndugu zake,mwanamke huyo aliyedaiwa kubakwa hadi kufa machi 1 mwaka huu eneo la Nane Nane mkoani hapa amezikwa leo na manispaa ya morogoro baada ya kutombambiliwa na ndugu zake.
Shukrani za pekee ziwafikie wafanyakzi wote wa kuchmba cha kuhifadhia maiti'Mochwari' kwa kukubali ombi la mwandishi wa habari hizi aliyeomba mrembo huyo aongezewe siku za kuhifahdia hapo tukitegemea huenda ndugu zake wangejitokea,kwa kawaida sheria za hospital ya ya mkoa wa Morogoro,marehemu anatakiwa kuhifadhia kwenye chumba hicho kwa majuma mawili[siku 14] ambapo baada ya hapo wanaukabidhi mwili uzikwe na manispaa,wafanyazi hao wa Mochwari walikubali ombi la mwandishi wa Mtandao huu na kuuhifadhi mwili huo hadi leo Machi 20,ikumbukwe mwili huo ulifikishwa kwenye chumbachi hicho machi 1 mwaka huu.
Majira ya saa moja na nusu asubuhi ya leo mwandishi wetu alipokea taarifa za uwepo la lori la Manispaa kwenye chumba hicho cha kuhifadhia maiti bila kuchelewa paparazi wetu alifika fasta na kushuhudia mwili wa maremo huyo uliokuwa ukitoa harufu kali ukitolewa kwenye majokofu ya Mochwari na kupakiwa kwenye Lori la manispaa.
Mtandao huu kwa kutumia usafiri wa pikipiki uliongozana na lori hilo hadi kwenye makaburi la Manispaa yaliopo eneo la Kolla na kushuhudia mrembo huyo akifukiwa bila kusaliwa.
Mbali na kushiriki mazishi hayo kwa kushika kole mwandisghi wetu pia alimsalia mrembo huyo sala ya dini zote mbili sambamba na kuweka alama kaburi hilo ambapo kama ndugu zake watajitokeza wakati wowote mwandishi wa mtandao huu atawaonyesha kaburi hilo ambalo alama iiyowekwa haiwezi kutoweka kwa kipindi cha miezi mitatu,hivyo mtu yoyote atakaye mtambu mrembo huyo kwa picha awasiliane na Mtandao huu kwa lengo la kuonyehswa kaburi na mepndwa wetu huyo aliyeuwawa kikatili na watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro ACP Faustene Shilogile Mwili wa Mrembo huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja ulikutwa kwenye mashmba ya mkonge njia panda ya kueleka Tungi huku sehemu za siri zikiwa wazi na kwamba alipopekuliwa polisi walikuta tiketi ya basi iliyoonyesha mrembo huyo February 28 alipanda basi hilo akitokea Dar es salaam kuja mkoani hapa. na kwamba Mach 1 mwili wake uliokotwa kwenye mashamba hayo ya mkonge.