Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro yazika Marehemu 52 wasio na ndugu, inasikitisha

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
SERIKALI wilayani Morogoro kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imelazimika kuwazika marehemu 52 wasio na ndugu kwenye makaburi ya Kola katika kipindi cha mwaka 2022/23.

Taarifa hiyo imetolewa na Meya wa Manispaa hiyo, Pascal Kihanga katika mkutano wa kawaida wa mwaka wa Baraza la Madiwani wa halmashauri manispaa hiyo.

Kihanga amesema watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa na kukaa hospitalini zaidi ya siku 20 halmashauri za jiji au manispaa huwazika.

Kihanga amesema kuwa kati ya mili hiyo wapo wanaume 40, wanawake 11 a fuvu la kichwa lililookotwa Machi 21 mwaka huu katika Kata ya Bigwa na lilizikwa Aprili mwaka huu.

Chanzo: Nipashe

===

Jamani Mkiondoka muwe mnaaga.
 
SERIKALI wilayani Morogoro kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imelazimika kuwazika marehemu 52 wasio na ndugu kwenye makaburi ya Kola katika kipindi cha mwaka 2022/23.

Taarifa hiyo imetolewa na Meya wa Manispaa hiyo, Pascal Kihanga katika mkutano wa kawaida wa mwaka wa Baraza la Madiwani wa halmashauri manispaa hiyo.

Kihanga amesema watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa na kukaa hospitalini zaidi ya siku 20 halmashauri za jiji au manispaa huwazika.

Kihanga amesema kuwa kati ya miili hiyo wapo wanaume 40, wanawake 11 na fuvu la kichwa lililookotwa Machi 21 mwaka huu katika Kata ya Bigwa na lilizikwa Aprili mwaka huu.​

SERIKALI wilayani Morogoro kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imelazimika kuwazika marehemu 52 wasio na ndugu kwenye makaburi ya Kola katika kipindi cha mwaka 2022/23.

Taarifa hiyo imetolewa na Meya wa Manispaa hiyo, Pascal Kihanga katika mkutano wa kawaida wa mwaka wa Baraza la Madiwani wa halmashauri manispaa hiyo.

Kihanga amesema watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa na kukaa hospitalini zaidi ya siku 20 halmashauri za jiji au manispaa huwazika.

Kihanga amesema kuwa kati ya miili hiyo wapo wanaume 40, wanawake 11 na fuvu la kichwa lililookotwa Machi 21 mwaka huu katika Kata ya Bigwa na lilizikwa Aprili mwaka huu.
 
Hawa wanaokufa bila ndugu zao kuwa na taarifa inawezekana ni wale watu wanaoenda kutafuta maisha kwingine bila mawasiliano na ndugu zao. Ndugu hudhani ndugu yao yupo hai duniani popote alipo anapambana na maisha kumbe alishafariki kitambo na hawana taarifa. Wengine inawezekana ni hawa wendawizimu wanaorandaranda mitaani maarufu kama vichaa au wagonjwa wa akili wasio na uangalizi, wakijifia ndugu zao wanakuwa hawana taarifa
 
Back
Top Bottom