PICHA: Mkutano wa Waislamu Mtwara wakipinga gesi isiende Dar es Salaam (leo)

Mpaka kieleweke!!

Sultani Mangungo wa Bagamoyo amesema hajui hawa jamaa wanataka nini!!
kadri mwaka 2015 unapokaribia waislam watajua kwamba ni chadema tu,ndio wenye nia ya kuwakomboa watanzania wote bila kujali dini zao,kinyume na poropaganda za ccm kwamba,chadema ni chama cha wakristo,na watajua kwamba ccm uwatumia tu, kwenye uchaguzi wakipata wanawaacha kwenye mataa
 
Hii kauli ya GESI KWANZA UHAI BAADAE,ndiyo haswaaa!!!!!!tuliyokua tunaisubiria,inaonyesha ni kiasi gani watu wamechoka KUNYANYASWA,KUTISHIWA KUDHALILISHWA,na hata KUONEWA,,!! Heko WAISLAMU kwa kuamua KUFUNGUKA,,,,!kwa hapo tupo pamoja,na Hakika Mungu pia yupo nanyi.HERI VITA INAYOTAFUTA HAKI,KULIKO AMANI INAYOPUMBAZA NA KUZALILISHA UTU WA "MTANZANIA" (MWANADAMU)
BY GODBLESS LEMMA.

Huu ujumbe ni mzito Watanzania tuamke tusiendekeze amani na njaa kila mtu awe na haki nchii hii.
 
Mti uliopandwa na WanaCCM wa Udini umemea na unatoa matunda haya. Wazee wa Jihad ndo kwanza wameanza.

Sio udini kudai haki waislamu hii ni njia ya kawaida na pengine wakristo wao wanadai kwa kuandika barua. Zao zinajibiwa zetu sisi zinatiwa kwenye dasbini, ndio maana utaishi mpaka utakufa huwezi kuwaona wakristo kudai haki kwa kundamana. Na sio sula la elimu hapo Watz wote elimu zo hatujaona manufaa yoyote.
 
Dah...machozi yamenitoka kuona taswira na hali hii, imenikumbusha picha za watanzania kipindi cha kumng'oa mkoloni miaka kenda iliyopita ilikua ni kanzu na vibaragashia tu ndo vilionekana kwenye uwanja wa mapambano na hatimae mkoloni aling'atuka na kukimbilia kwao. Mungu wabariki watanzania hawa na kwa historia yao iliyo tukuka.
 
Kila la kheri ndugu zangu coz hii nchi wanataka kuifanya ya pande tatu yaani kusin haina thamani..hapa mpaka kieleweke Dua zetu zipo nyuma yenu..
 
Duuuuuuuuhh hadi Dini zinaanza kuingihingilia Jk anapumulia mashine sasa

Sio udini, ila rejea nyuma kipindi cha ukoloni hawa watanzania wenzetu wanahistoria ya kutukuka..kwenye mapambano kulikuwa zikionekana kanzu na bargashia na hata nyimbo zao za kuhamasisha zilikuwa zinasema ivi, "In sha Allah, Mungu akipenda mkoloni lazima tumng'oe..." so hatukujali imani wala nini wote kwapa moja tuliimba kwa sauti kuu tukielekea kwenye mapambano hivyo basi nikitu ambacho kipo na ushindi utapatikana, sina shakaa na waislam wa nchi hii. Bravo x x x:target::cheer2::cheer2::target:
 
Wanamtwara unganeni kwa pamoja kupigania saslimali hii. Mkienda kwa makundi mtaishia pabaya. Jiungeni wote kwa pamoja na mpinge kwa pamoja hapo serikali itawaheshimu na kuyaangalia matakwa yenu kwa akili. Mkija kwa makundi watatumia makundi hayo hayo kuwaangusha na mtakapoamka mtakuta gasi ilishaondoka.
 
mkuu sizinga tupo pamoja mkuu,

nadhan panapo majaliwa kesho uje hapa tena umwage nondo za kutosha

Mkuu habari bwana!! Huwa mi silazi man...panapo majaliwa namwaga kila kitu bila kuchakachua!! Mbona kwa hilo tupo pamoja!! Forever we go!!
 
Back
Top Bottom