mkuu naelewa sana na nimesema hivyo kutokana na dhana ya ngekewa. Madai yake ni kwamba ukishamkubali mwenyezi mungu na mtume wake (shahada) basi wewe tayari ni muislaam hivyo mengine yote ya kuasi na hayakuondoi ktk uislaam ila pale tu unapofanya kufur. Na ndio nakamtalia maneno hayo maana wengi tulifundishwa hivyo na tukaaminishwa hivyo..
Ni makosa ambayo sote tunayafanya na yametumiwa sana na wanasiasa kuitumia dini ya kiislaam to their advantage..nikisikia kadogoo anaitwa suleiman basi huyu muislaam, ndugu yangu lazima nimpe tafu, kumbe uislaam ni maisha unayotakiwa kuishi (way of life) ili uwe muislaam tofauti na imani ya wakristu ambayo ukishamkubali yesu kama mwokozi basi wewe utaokoka maana yeye tayari kisha beba mzigo wako kwa kujitoa mhanga msalabani.
Ni makosa ambayo waislaam wengi hutafsiri dini hii kutokana na influence ya ukristu ktk maisha yao bila kujua kwamba uislaam ni dini inayosimama peke yake na wakristu ni watu (society) wasiokuwa na dini ila wale waliomfuata yesu na wakaitwa wakristu (christians) wakati waislaam hawaitwi muhammadans. Pia jews ilikuwa dini yaani imani leo hii imebadilishwa na kuwa society ya kizazi cha daud sio tena followers wa mafundisho..
Na ndio nikamwambia uislaam sivyo hii ni dini inayojitegemea, wewe binaadam unaposhahadia ni presupposes kufuata sheria zake haina maana zaidi hata muislaam safi anaposali sala tano hutoa shahada kila siku..uislaam ni way of life and you got to live that life to be a muslim...it's total submission to god haina njia za mkato kufikiria kwamba uislaam ni kama uraia ukisha tiwa maji basi you are muslim...
Utaniuwia radhi mkuu wangu sina ujuzi wa kufupisha wala kuelezea vitu kinagaubaga lakini nachotaka kusema tu ni kwamba ile dhana walotujenga wazee wetu kuamini uislaam ni watu sii kweli bali sisi watu ndio huingia uislaam na tunatakiwa kuishi kama kitabu kilivyotuamrisha nje ya hapo unatoka ktk uislaam.