Picha: Misa ya mazishi ya Padre Babu Arusha leo hii

View attachment 451289 View attachment 451290 View attachment 451291 View attachment 451295 View attachment 451292 Hali ilivyokuwa katika viwanja vya Seminari ndogo ya Usariver Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, palipofanyika Ibada ya Misa Takatifu ya Kumsindikiza Fr JOSEPH BABU maarufu kama Fr Babu, katika Safari yake ya Mwisho hapa duniani.

Misa hiyo inaongozwa na Askofu Isaac Amani wa Jimbo la Moshi akiwa pamoja na Askofu Mkuu Josephat Louise Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha na Askofu Roghat Kimario wa Jimbo la Same pamoja na Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu Padri Amandus Kapele.

Wengine wanaishiriki Ibada hiyo ni Mapadri wa shirika hilo na Mapadri wa Jimbo la Arusha,Moshi, Same na Mbulu;wakiwa pamoja na Watawa wakike na wakiume na Walei mbalimbali.

Kwa heri Padre Babu...Ulikuwa na

Kwa heri Padre Babu...Ulikuwa na msemo wako maarufu sana,kila mtu alipokuwa anakuuliza,haya yote unajenga na kuyasimamia nani atayafaidi siku ukifa?Ulijibu " Life is more than just being alive",Kwako kufa sio mwisho wa maisha...Hakika leo umezikwa,lakini utaendelea kuishi.Miaka 99 sio mchezo.Sisi wanafunzi wako tutakukumbuka daima.

Padri Babu;Pumzika kwa Amani Mpendwa wetu.Ulivipiga vita vilivyo vigumu,na mwendo umeumaliza...Ulale Pema Peponi!!
Nakumbuka evening talk zake alikua anasisitiza watu wasiwe wanafiki
 
Mungu amlaze pema padri babu,
naomba kuuliza hapa wakuu kwa nini askofu wa arusha peke yake ndie anaeitwa askofu mkuu? wengine wanaitwa mf askofu yuda, askofu mkude askofu asaac lakini yeye anatwa askofu mkuu lebulu.
 
Rafiki yangu mwaminifu umetangulia umetuachia tunu ya huduma ya kutukuka.

Upumzike kwa amani maana unevipiga vita vya imani na matendo kwa kutukuka. Mimi ni mmoja wa mashahida wa kazi zako za kiroho na kimwili pale Ngarenaro.

Nina hakika umevaa taji yako mbele ya muumba wetu.
 
Mkuu ninaelewa hili lakini wale watoto watatu wa Fatima wote wamezikwa ndani ya kanisa.
Naomba nikijibu kwa elimu yangu ndogo na imani yangu.

Wale walibarikiwa kuwasiliana na Bikira Mariam moja kwa moja kwenye utoto wao.

Video ya Fatima inaeleza vizuri mimi niliinunua TEC Dar lakini wauzaji walikuwa wa ile bookshop ya St Joseph Dar.

Ni nzuri huwezi kosa kujifunza kitu.
 
Asante mkuu lakini huwa ninakwenda Fatima mwenyewe na makaburi ya watoto nimeyaona pia mahali mama alipokuwa anatokea limejengwa kanisa linaitwa apparition church, kanisa walilozikwa watoto ni Basilica na mama aliagiza lijengwe kanisa la Utatu Mtakatifu ni kubwa sana, linachukua watu 10,000.
 
R.I.P fr...hv alikuwa padre wa jimbo au wa shirika la Roho Mtakatifu? Mwenye uhakika basi anisaidie
 
Back
Top Bottom