Picha: Misa ya mazishi ya Padre Babu Arusha leo hii

Mkuu ninaelewa hili lakini wale watoto watatu wa Fatima wote wamezikwa ndani ya kanisa.
Kumbuka wale wamezikwa katka Kanisa la Hija,eneo ambalo linasadikika ndipo walitokewa na bikira Maria.
Wale wawili hawakukaa mpaka kuuona utu uzima wao,walikifa wangali watoto wadogo...Huyu binamu yao Yasinta ndio alikaa miaka mingi,alifariki akiwa na miaka 90 hivi,baada ya mwaka,mabaki yake naye yakapelekwa kwenye hilo kanisa....Kwa hiyo hawa ni "Special Case" madam Sky Eclat
 
Mkuu ni Lucia ndiyo alikaa miaka mingi na alipata maono mengi sana, wa kwanza kufa alikuwa Francis baadae alikufa Yasinta. Lakini walishaambiwa na mama mzuri kuwa atawachukua na watakuwa nae, Francis alipata homa na kufariki miezi michache tu baada ya kuonana na mama mzuri.
 
ajabu sana kumbe rc hawapendani kiivo
Hwapendani kivipi na wewe Mamaa Wa Feedback?
Padre Babu alikuwa ni Padre wa Shirika na si wa Jimbo.Utume wake aliufanyia sana Arusha,baadae Kenya na akarudi tena Arusha.

Sasa ukaazi wake ni Arusha.Hivyo yupo chini ya Jimbo Kuu la Arusha.Na Jimbo Kuu la Arusha ni Metropolitania yenye majimbo ya Arusha,Moshi,Same na Mbulu...Ndio maana kwa heshima ya Fr Babu,Maaskofu wa Metropolitania ya Arusha pamoja na Mapadre na watawa wamefika.

Pengo sio mkuu wa Kanisa Katolikia Tz,Yeye ni Askofu Mkuu tu wa Jimbo Kuu la Dsm..Ambapo ina majimbo kama Dsm,Morogoro,Mahenge,Ifakara(!?) na Tanga...huko sio kwake!Labda ungeweza hata kuuliza mbona Rais wa TEC simuoni?na si Pengo
Cc Otorong'ong'o
 
Mkuu ni Lucia ndiyo alikaa miaka mingi na alipata maono mengi sana, wa kwanza kufa alikuwa Francis baadae alikufa Yasinta. Lakini walishaambiwa na mama mzuri kuwa atawachukua na watakuwa nae, Francis alipata homa na kufariki miezi michache tu baada ya kuonana na mama mzuri.
Asante madam...Kweli hapo nilichanganya madesa...Si Jacinta,ni Lusia!!
Na ndio wanasema bado kuna mambo mengine au siri nyingine hakuzisema mpaka anakufa!!
 
Asante madam...Kweli hapo nilichanganya madesa...Si Jacinta,ni Lusia!!
Na ndio wanasema bado kuna mambo mengine au siri nyingine hakuzisema mpaka anakufa!!
Yah alitokewa na mama mzuri karibu kila siku na waliongea mengi, kanisa lilishtuka baada ya Pope John Paul II kupigwa risasi ndiyo liliamini maono ni ya kweli na Fatima palijengwa kama sehemu ya hijja, hili ni jambo alilolisisitiza mama, Lucia aliambiwa Fatima pakishajengwa na yeye hatakuwa na muda mrefu wa kuishi, na hayo ndiyo yaliyotokea.
 
View attachment 451289 View attachment 451290 View attachment 451291 View attachment 451295 View attachment 451292 Hali ilivyokuwa katika viwanja vya Seminari ndogo ya Usariver Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, palipofanyika Ibada ya Misa Takatifu ya Kumsindikiza Fr JOSEPH BABU maarufu kama Fr Babu, katika Safari yake ya Mwisho hapa duniani.

Misa hiyo inaongozwa na Askofu Isaac Amani wa Jimbo la Moshi akiwa pamoja na Askofu Mkuu Josephat Louise Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha na Askofu Roghat Kimario wa Jimbo la Same pamoja na Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu Padri Amandus Kapele.

Wengine wanaishiriki Ibada hiyo ni Mapadri wa shirika hilo na Mapadri wa Jimbo la Arusha,Moshi, Same na Mbulu;wakiwa pamoja na Watawa wakike na wakiume na Walei mbalimbali.

Kwa heri Padre Babu...Ulikuwa na msemo wako maarufu sana,kila mtu alipokuwa anakuuliza,haya yote unajenga na kuyasimamia nani atayafaidi siku ukifa?Ulijibu " Life is more than just being alive",Kwako kufa sio mwisho wa maisha...Hakika leo umezikwa,lakini utaendelea kuishi.Miaka 99 sio mchezo.Sisi wanafunzi wako tutakukumbuka daima.

Padri Babu;Pumzika kwa Amani Mpendwa wetu.Ulivipiga vita vilivyo vigumu,na mwendo umeumaliza...Ulale Pema Peponi!!
Huyu padri Babu ni tofauti na yule padri alikuwa akiendesha gari aina ya kombi enzi hizo nakumbuka alikuwa parokia ya samanga au mwingine ? R.I.P
 
Ulikuwa mwalimu mzuri hasa katika kutuhasa sisi tuliokuwa wanafunzi wako fr babu rest in peaceful
 
Fr.BABU amefanya mengi ya maana kwa jamii, kuliko hata PENGO.

Mungu amlaze mahala pema peponi.

BABU alikuwa ni zaidi ya Padri.
 
Kumbuka wale wamezikwa katka Kanisa la Hija,eneo ambalo linasadikika ndipo walitokewa na bikira Maria.
Wale wawili hawakukaa mpaka kuuona utu uzima wao,walikifa wangali watoto wadogo...Huyu binamu yao Yasinta ndio alikaa miaka mingi,alifariki akiwa na miaka 90 hivi,baada ya mwaka,mabaki yake naye yakapelekwa kwenye hilo kanisa....Kwa hiyo hawa ni "Special Case" madam Sky Eclat

Ni Lucia ndio alikaa miaka mingi kaka, nadhani pia kuna tofauti ya kulikuta Kanisa na kuzikwa humo au kuzikwa na kisha Kanisa kuja baadae, Mara nyingi watakatifu kama hao wa Fatima, huwa wanazikwa na kisha Kanisa linajengwa na kuwa kama kituo cha Hija
Mfano
Ni Kanisa la pale Namugongo Uganda, lililojengwa kwenye eneo ambalo wale Mashahidi wa Uganda Kizito, Lwanga, Mulumba na wenzao walipochomwa moto
 
Pumzika baba hakika hukuwa padre tuu, ulistahili zaidi ya ukadinali, kazi zako zitaonekana hata baada ya miaka mia tano
 
Mkuu ni Lucia ndiyo alikaa miaka mingi na alipata maono mengi sana, wa kwanza kufa alikuwa Francis baadae alikufa Yasinta. Lakini walishaambiwa na mama mzuri kuwa atawachukua na watakuwa nae, Francis alipata homa na kufariki miezi michache tu baada ya kuonana na mama mzuri.
heshima yako mkuu.uko deep hadi uku
 
Utamaduni wa kikanisa wa kuzika ndani ya Kanisa ni kwa ngazi ya Maaskofu,Kardinali na Papa
Mapadre huzikwa ktk eneo maalumu ambalo jimbo huwa wamejiwekea
Mkuu naomba ukipata muda utupe wasifu mfupi wa huyu Padri. Nimemsikia sana ila simfahamu kivile zaidi ya kazi zake
 
Back
Top Bottom