Mbowe ni kijana wa JK humu JF Pro-Chadema povu linawatoka ovyo mwenye chama Mbowe yupo katulia kwa JK anawachora tu.
Mkuu Ritz,baada ya kumtambua kama rais,kugonganao chai ikulu, kitakachofuata ni lift za ulaya ndani ya gulf stream hapo ndio mwisho wao magwandwa.Hiyo picha angekuwa Zitto, ungesema yote lakini umemuona Mbowe umeamua kusifia Kombati, ha haa ha! JK bana anawapatia sana hawa watu.
Leo kupitia Itv nimeona juhudi zako kwa kuwa umeweza kumleta rais Kikwete na Magufuli wakazindua barabara ya kwasadala -masama kwa kiwango cha lami na huenda ikaunganishwa tokea MASAMA,SONU,BWANI hadi KALALI.
Nimekupongeza wewe kwa kuwa niliona juhudi zako toka bunge la bajeti ulivyoifuatilia hii barabara.
Ombi langu kwako vijiji vya USWAA,SHARI,KYERI havina huduma ya mwochwari wala zahanati ya uhakika ujitahidi uwabane hao magamba watumie hizo kodi zetu watuletee hiyo huduma.
Naomba kuwasilisha
Mbowe kazini, jk kazini, kilaza mkuu wa wilaya mnafiki sana simpendi binafsi namfahamu kuliko watu wengi humu jf. Najua yuko humu hakika ni mnafiki mtajajua subirini ni dhaifu zaidi ya mkuu wake novatus we ni ..... Nakuchukia kuliko unavyohisi unahisi umepewa dunia kuimiliki kwa ukuu wa wilaya we ni,,.. Toka
acha ukizibo wewe mami hoja huelewi unakurupuka tuUnaacha kuwaombea wananchi huduma muhimu za afya na vipimo ili wasife wewe unaomba mochwari. kweli wewe zoba.
kupongeza lazima wewe mama hao wa ccm mliowachagua na hata bungeni na majimboni hawaonekani utawapongeza kwa lipi?Anapongezwa kwa kazi aliyoiombea kura? tanzania bana , kichekesho kweli, mtu analipwa kwa kazi hiyo , then unampongeza, elimu ya uraia bado sana other wise iwe ushabiki tu.
Mheshimiwa Mbowe akipanga mikakati na Rais Jakaya Kikwete ;
slaa hawezi kubadilika.
Mbowe is cool.
angekua zitto ungewasikia pro chadema wangemrukia zitto, hapo hapo vipi?
-Kuwa mkweli na you should quote him right
-Acha kupotosha.Maendeleo yaliyopo hayalingani na miaka 50 ya uhuru.
Sijui kwanini mtafute faraja kwa nguvu kiasi hiki......
Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CDM amempongeza raisi JK kwa ujenzi wa miundo Mbinu hasa ya barabara hii inaonyesha ukomavu wa kisiasa kwani angeweza kumtolea vijembe na kejeli lakini nadhani hii pongezi haiondoi ukweli kuwa kuna pengo kubwa sana kati ya kilichofanyika na kilichotakiwa kufanyika hasa ukizingatia rasilimali tulizonazo
Nawasilisha
hii ndiyi vita ambayo mmeshaanza kugombea jimbo la Rombo?Mhe.Joseph Selasini naye alimshukuru JK lakini akatukanwa sana humu kuwa ni mamluki,mtu wa hovyo asiyefaa. Mdau mwingine alisema kuwa Mhe.Selasini alimsifu JK kwa sababu anajifagilia njia ya kwenda CCM 2015. Hapo niliona Ben Saanane akitokwa mapovu kuwa Selasini alikosea. Nilikuwa kimya kwa sababu nilitarajia Mbunge mwingine atafanya hivyo ili tuweze ku justfy licha ya kuwa hilo liliwahi kutokea kwa Mhe.Sugu na Mhe.Zitto.
Kwanza kama mwanasiasa unapaswa utumie maneno yako kwa mbinu na umakini mkubwa. Kumshukuru Rais ina maana pana sana ambapo hapa sitaiandika yote,ila kwa sehemu mkumbuke kuwa Rais ndiye Mwenyekiti wa Baraza la mawaziri ambalo hupanga matumizi( Budget) ya mwaka mzima. Rais anayo nafasi ya kuongeza au kutoa mpango wowote kwenye bajeti ya wizara yoyote.
Taabia ya kiongozi wa Siasa kushambuliwa na wasio wanasiasa au waliovaa pampers za kisiasa huku wakidhani kuwa ni Wanasiasa kama kina Ben Saanane ni tabia mbaya na ya hovyo!. Mwanasiasa anapofanikisha moja ya ahadi zake kwake ni moja ya ngazi ya kushinda tena kwenye siasa uchaguzi ujao. Wewe unayekaa Online huku huna ulichoahidi wala cha kutekeleza! Huwezi kufanya kama yeye! Unasubiri atoe kauli yoyote uweze kuongea. Yes! Endeleeni kuwalaumu wanasiasa wanapotekeleza ahadi zao kwakuwa nyie kamna cha kufanya kwa wananchi.
By Deus.