Katika mapokezi na mkutano wa Zitto picha zote na hata jukwaa alilolutumia hakuna bendera ya CHADEMA,hata kwenye maandamano ya wafuasi wa Zitto na pikipiki hakuna bendera ya CHADEMA,na ikumbukwe Zitto amejitapa sana kuwa anakipenda CHADEMA na angependa hata mtoto wake aje kuwa CHADEMA,Mbunge wa CHADEMA na unayehubiri mapenzi kwa chama unakosaje hata bendera moja ya chama kwenye mkutano wako?? Huu sio unafiki??!!
Tukisema kuwa mkutano huu umeratibiwa kwa maelezo maalum na pia kuandaa hadhira mathalani wasibebe bendera wala alama yoyote ya chama Tutaongea?? Tukisema mkutano huu ni wa mamluki dhidi ya CHADEMA tutakosea??!! Zitto ni mtu wa ajabu sana!!
Kwenye hotuba yake amelialia kutokuaminiwa ila kweli inajulikana kuwa matendo ya mtu ya kutilia shaka au maouvu ndio hufanya mtu asiaminike,imani hainunuliwi bali inatengenezwa kwa hiyo matendo ya Zitto ndio yanafanya uonekane msaliti
Kigoma inahistoria chafu ya kutoa wanasiasa wanafiki,wazandiki na wachumia tumbo na Zitto nathubutu kusema ni mmoja wao,Kigoma ingebaki kutoa wacheza mpira na wanamziki kama wakina Kaseja,Maulidi,Ali Kiba n'a wengine lakini si viongozi wa siasa,kwani ni wezi wa fikra na imani za walalahoi kwa maslahi yao binafsi n'a watu wanaowatumikia!!!