PICHA: Makamba hizi si kampeni za urais

PICHA: Makamba hizi si kampeni za urais

kama ametumwa na mamvi je utasemaje?
watu hawajasoma mchezo,hapo mamvi kaamua yeye achukue urais wa muungano makamba anagombea Tanganyika...zinduka,chadema has to make new plan baada ya kumtupa zitto
 
Kuna kitu watu wengi hawakielewi. Makamba Jr ni kambi ya Lowasa. Kinachofanyika sasa ni mkakati maalum. Hiyo inaitwa divide and rule. Mwisho wa siku anajitoa na kumuunga mkono EL. Makamba kakabidhiwa kanda ya ziwa. Hii ni kanda muhimu sana kimkakati. Mark my words, time will tell.
 
mimi nintampa kura yule anayenifanya niende chooni,sasa km unanipigia porojo mwisho wa siku naona unapaa na elkopta kwanza ukiwa umeninyang`anya mia tano yangu , alafu mimi ikifika jioni naenda kulala njaa na watoto unadhani nitakuelewa kweliiiiiiiiiiiiiii
utafanywa vibaya wewe.
 
Ni kweli kabisa, kanda ya Ziwa ni muhimu mno kuamua Rais wa nchi hii, idadi ya wapiga kura ni kubwa mno kanda hii.

Kwa mbio hizi, Diallo atang'ara sana maana ni kiungo muhimu kuelekea urais via CCM.
 
Naona magamba wameamua kuwatumia bodaboda kama mtaji kuelekea 2015. Wengine mnapaswa kujipanga, kuwa wabunifu, na kuvunja bond hii haramu na ya ulaghai inayotaka kutengenezwa na hawa jamaa kwa maslahi binafsi na ya kilaghai.

Mtahangaika sana ths tym na ccm. Haoo wanachanja mbuga nyie mnavuana vyeo kwenye hiyo saccos
 
mimi nintampa kura yule anayenifanya niende chooni,sasa km unanipigia porojo mwisho wa siku naona unapaa na elkopta kwanza ukiwa umeninyang`anya mia tano yangu , alafu mimi ikifika jioni naenda kulala njaa na watoto unadhani nitakuelewa kweliiiiiiiiiiiiiii

Wewe ni kababu kweli, badala ya kuangalia suluhisho la muda mrefu wewe unaangalia hiyo mia tano, kofia, tisheti. Hiyo mia tano utaitumia kisha baada ya masaa mawili unaishusha through kinyesi. Sasa kesho yake utaenda choo vipi kama huyo wa kukupa mia tano hayupo?

Unaangalia tu kwenda choo, je hao wanao watasoma vipi na kwa elimu gani? Kababu, kwa sasa tafuta suluhisho la kudumu especially kwa wanao na kizazi kijacho. Kama utaendelea kufikiria suluhisho la siku moja, una haki ya kuitwa KIBABU.
 
NAIBU wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba ametaka ujio wake Jiji la Mwanza usihusishwe na Kampeni za chini kwa chini za Urais bali ni kutekeleza ombi la Umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza kuwasaidia kupata Bima ya Afya

Nimefurahi sana jamani hawa madereva bodaboda wanahitaji bima ya afya.Makamba hongera kwa kuwasaidia ni vyema uzunguke nchi nzima uwasaidie.Wodi za majeruhi zimejaa madereva boda boda nchi nzima bima za Afya zitawasaidia kuwanusuru maisha yao.
Kwa hili nakupongeza sana endelea kwenye mikoa yote ukiweza iwe wamekuomba au la nenda kawasaidie.
 
Hivi kwani Makamba kahamishiwa wizara ya Afya?Kwa nini yeye?
 
sio kweli hizi ni kampeni za wazi wazi,makamba huna majukumu mengine ya kufanya?????????????
 
Hivi kwani Makamba kahamishiwa wizara ya Afya?Kwa nini yeye?

Unataka kusema nikikutana na ombaomba barabarani nisimpe hela sababu mimi sio waziri wa ustawi wa jamii? Ukienda ustawi wa jamii wanakwambia hawana hela za kusaidia omba omba.Akitokea mtu kusaidia hao omba omba awe waziri wa misitu au nyuki au si waziri ni sawa tu.

Bima ya afya ni pesa haitolewi bure kama charity na wizara ya afya kwa taarifa yako sasa kama aweza kuwasaidia waipate kuna taabu gani? Bima za afya zinaendeshwa na makampuni ya bima kama hujui.Si kitengo cha waziri wa afya.Ni kama zilivyo bima za magari au za maisha huwezi enda kwa waziri wa afya akukatie hiyo bima wizarani.

Anyway basi kama na waziri wa afya naye anaweza tunaomba naye awasaidie wapate hiyo bima.Naye aende asaidie.Tunachohitaji shida halisi za watu zitatuliwe na ndio kazi ya mwanasiasa yoyote.Kazi yake si kukaa ofisini kuongea na kuandika kingereza na kuhutubia hotuba ndefu wananchi hotuba zisizotatua matatizo.
 
Hawa bodaboda wanatumika vibaya
Hawatumiki vibaya ila wanajua kula za wajinga. Hata wewe ukienda kesho mradi uwape chochote wataandamana na wewe. Wewe unafikiri wanafanya kazi hiyo bure? Boda boda ni wajanja wanajua kutumia fursa. Kesho Lowassa akitia timu hapo wanaye kama kawa! Viongozi wa dini nao ni wajanja wanajua namna ya kuzipata za wanaounyemelea urais. Kila mwenye harambee sasa hivi lazima amwalike EL na Makamba. Wewe hujiulizi kwanini hawamwaliki Nape au Magufuli? Wameshawajua wanaomwaga fesha kwa lengo la kujitangaza na kutafuta kuungwa mkono na viongozi wa dini.
 
Kama BABU anavyousikilizia bombani.

Mababu wako wengi sana ccm na wote wamejaribu kuwania urais...mzee john aka baba le-mutuz,salim.a.salim wote hao ni babu ila hatuwadharau kama ww unavyomdharau mzee wetu..Mungu akubariki umalize mwaka salama pamoja na dharau zako
 
Back
Top Bottom