PICHA: Makamba hizi si kampeni za urais

PICHA: Makamba hizi si kampeni za urais

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
NAIBU wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba ametaka ujio wake Jiji la Mwanza usihusishwe na Kampeni za chini kwa chini za Urais bali ni kutekeleza ombi la Umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza kuwasaidia kupata Bima ya Afya baada ya kuwawezesha kupata pikipiki 1745 za FEKON na si vinginevyo.

Kauli hiyo ya Makamba ameitoa leo wakati wa kufungua kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini hapa, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji ujio wangu Mwanza “Niko hapa kwa ajili ya shughuli hii mliyonialika bali kuja kushiriki Kampeni muhimu ya Bima ya Afya kwa ajili ya Usalama wa badae” na si vinginevyo.

Makamba amesema kwamba upatikanaji wa Leseni kwa urahisi na uharaka usiwe tiketi ya Kifo kwa wananchi. ImageUploadedByJamiiForums1388219288.863056.jpgImageUploadedByJamiiForums1388219312.733991.jpgImageUploadedByJamiiForums1388219330.134412.jpgImageUploadedByJamiiForums1388219355.656705.jpg
 
Wana angaika Sana ccm na kazi wanayo kweli kweli name bado tutazidi kuona mengi bado membe bado wassira bado name engine wengi tu ila nacho kiona watu hasa boda boda watakula ccm na kulala Chadema
 
Ana Umri gani huyu Seleman na je katiba inasemaje juu ya Umri wa kugombea Urais asije akawa anamaliza Rasilimali halafu Katiba ikaja kumtosa akahamia kuuza Sembe.
 
mkuu kwa mkoa wa mwanza wala usihofu.....

Huwa tunatumia msemo wetu maarufu " kula ccm lala(kura) cdm".. ...

Waache vijana wale bana....
mimi nintampa kura yule anayenifanya niende chooni,sasa km unanipigia porojo mwisho wa siku naona unapaa na elkopta kwanza ukiwa umeninyang`anya mia tano yangu , alafu mimi ikifika jioni naenda kulala njaa na watoto unadhani nitakuelewa kweliiiiiiiiiiiiiii
 
Naona magamba wameamua kuwatumia bodaboda kama mtaji kuelekea 2015. Wengine mnapaswa kujipanga, kuwa wabunifu, na kuvunja bond hii haramu na ya ulaghai inayotaka kutengenezwa na hawa jamaa kwa maslahi binafsi na ya kilaghai.
 
Naona na Biku Kutecha naye kavalishwa T-shirt,huko Dar ni Lowasa na bodaboda,huku kwetu Mwanza ni Makamba Jr.....
 
Mkuu kwa Mkoa wa Mwanza wala usihofu.....

Huwa tunatumia msemo wetu maarufu " KULA CCM LALA(KURA) CDM".. ...

Waache vijana wale bana....

Ndio maana mwaka 2010 mulipata viti 23.
 
Naibu wizara ya Sayansi na Teknolojia,na huku bima ya Afya!Mbona sikuelewi Makamba?Ungekuwa naibu waziri wa Afya sawa au hata uchukuzi na usafirishaji,lakini Sayansi na teknolojia Makamba?Na kile kikao cha Wachungaji(viongozi wa dini) juzi usiku?Husijali kijana,tutakukumbuka 2015,ila hela hizo unazotumia unazitoa wapi??????!
 
masikini vijana wa bodaboda.wamegeuzwa staircase ya wanasiasa kuelekea kuutwaa ukubwa 2015.ni huruma kwa kweli.
 
Kazi ipo kweli... urais unakuwa utumwa kwa vijana wetu.



Bodaboda amkeni mjitambue.
 
Watoka povu watakuja hapa na pumbapumba zao kama za yule mchungaji MKAMA6.
 
Last edited by a moderator:
mimi nintampa kura yule anayenifanya niende chooni,sasa km unanipigia porojo mwisho wa siku naona unapaa na elkopta kwanza ukiwa umeninyang`anya mia tano yangu , alafu mimi ikifika jioni naenda kulala njaa na watoto unadhani nitakuelewa kweliiiiiiiiiiiiiii

Sawa mtabiri
 
Back
Top Bottom