Picha: Kinana akiwa ziarani jijini Mbeya

Picha: Kinana akiwa ziarani jijini Mbeya

Kandoro mwenyewe kavaa gwanda kwa kuwa anajua Mbeya hawadanganyiki ni wanamageuzi wa ukweli.
Kinana na Nape wanafanya tu mchezo wa kuigiza, mara wapande baiskeli, mara wapande bajaj, mara wale wali maharage, wale chai na vitumbua wamekaa chini, wabebe vitofali na kulima na jembe la mkono, yooote hayo majibu watayapata 2015

2015,ole wao itakapofika ile siku,wameamini haiwezekan,lakin ole!
 
Ukiona mtoto wako wa miaka 30 anang'ang'ania kwenda chekechea jua umeliwa.
 
kwenye ziara hii kinana na nape wameongoza kwa kupiga picha za maigizo. ndo mafanikio hayo.

2Q==
2Q==


Vigezo na masharti kuzingatiwa
 
Sio siri kama ndio wamefanikiwa kupata umati mkubwa kiasi hiki huko mby 5 kwa bwana kinana ? Hata mwanjelwa wanasimamishwa sio siri ccm ina mabadiliko maana zamani kupita pale ilikuwa mtihani
 
Hata mimi nashangaa, chama (CHADEMA) ambacho kinasemwa kimefikia mwisho wakati kinawanyima usingizi kila kukicha. CCM ni kama shetani, maana shetani kila siku anahangaika na wale wanaomcha mwenyezi Mungu kwa dhati, wale ambao hawana imani kabisa hao wala hana muda nao maana ni wake tayari. CCM hata siku moja hawataji TLP, UDP, CUF, etc., kila kukicha CHADEMA, jamani CHADEMA, CHADEMA, CHADEMA,......

well said mkuu! CCM hakiwezi kuyashambulia matawi yake. hata hayo matawi kazi ni kujikombakomba kwa mkuu wao. hakuna ushindi bila mapambano.
 
Watanzania wengi tuna shida kiuchumi, uelewa mdogo nk lakini kwa maigizo haya naamini 95% wataweza kuwaelewa hawa walaghai.
 
Na Chadema hawawezi kwenda sehemu bila kutaja CCM so akili kwako wewe mwenye Mahaba na Chadema

mkuu,rejea hotuba za Mwl Julius Nyerere alipokuwa anazungumzia nafasi na umuhimu wa chama tawala kwa vyama vya upinzani. ili vyama vya upinzani vistawi lazima vikikosowe chama tawala. CHADEMA kinakitaja CCM kuonyesha uozo ili watu wajue kinachoendelea serikalini chini ya CCM. Chama tawala kinapokiandama chama kimoja tu cha siasa kila kwa sekunde wakati kuna vyama vingine vya siasa lukuki, lazima ujiulize maswali mengi kama hujawa likizo kufikiri au juu ya shingo yako hujabeba koroma!
 


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda bajaji tayari kwa kuelekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe Mwanjelwa jijini Mbeya akitokea ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, huku Nape Nnauye naye akijiandaa kuinga kwenye bajaji. Kinana akiongozana na Ujumbe wake pamoja na viongozi wa mkoa wa Mbeya na wilaya leo wametumia usafiri huo ili kuonyesha kwamba Chama hicho ni chama cha wananchi wa kawaida ambao ni wafanyakazi na wakulima tofauti na wenzetu wanaojifanya wanawatetea lakini wanakuja na Helikopta na kuwachangisha michango ya fedha kisha wanatokomea zao. Katika msafara huo pia yupo Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA)

Vijana wa Mwanjelwa wakiuzuia msafara wa Kinana wakati alipokuwa akielekea uwanja wa Luanda Nzovwe kwenye mkutano jambo lililofanya Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye watembeee kwa mguu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye wakitembea kwa miguu katika eneo la Mwanjelwa huku vijana wakiwashangilia
Abdulrahman Kinana akiwa katika bajaji iliyomchukua


Nape Nnauye akiwa katika Bajaji iliyombeba
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakiwapungia mikono wananchi wakati wakielekea kwenye mkutano.


Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wakiwa katika meza kuu.
Umati wa watu waliohudhuria katika mkutano huo.
Kada wa CCM aliyejiunga na CCM hivi karibuni akitoka chama. cha CHADEMA Braison Mwasimba akiunguruma katika mkutano huo
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akimwaga sumu katika mkutano huo.
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akiwaimbisha wananchi katika mkutano huo.
Msanii wa muziki wa kizazi Kipya Michael Senka mashairi jukwaani wakati mkutano huo ukiendelea leo jioni.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akitolea ufafanuzi wa mbolea ya Minjingu ambayo imekataliwa na wananchi wa mkoa wa Mbeya huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza kwa makini

Kada wa Chama cha Mapinduzi Tambwe Shitambala akizungumza katika mkutano huo.

Ruanda Nzovwe haipo mwanjelwa,ipo ccm/ilomba
 
Unafiki mtupu, tangu lini muuza meno ya Tembo mashuhuri akapanda bajaj?
 
Naona wameona hii style hailipi.........Hapa wakiwa Nzega. Hawa jamaa akili zao sawa na wafuasi wao tu. Mbulula.

120.jpg
 
Back
Top Bottom