Picha: Kinana akiwa ziarani jijini Mbeya

Taswira

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Posts
1,198
Reaction score
452

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda bajaji tayari kwa kuelekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Luanda Nzovwe Mwanjelwa jijini Mbeya akitokea ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, huku Nape Nnauye naye akijiandaa kuinga kwenye bajaji. Kinana akiongozana na Ujumbe wake pamoja na viongozi wa mkoa wa Mbeya na wilaya leo wametumia usafiri huo ili kuonyesha kwamba Chama hicho ni chama cha wananchi wa kawaida ambao ni wafanyakazi na wakulima tofauti na wenzetu wanaojifanya wanawatetea lakini wanakuja na Helikopta na kuwachangisha michango ya fedha kisha wanatokomea zao. Katika msafara huo pia yupo Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA)

Vijana wa Mwanjelwa wakiuzuia msafara wa Kinana wakati alipokuwa akielekea uwanja wa Luanda Nzovwe kwenye mkutano jambo lililofanya Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye watembeee kwa mguu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye wakitembea kwa miguu katika eneo la Mwanjelwa huku vijana wakiwashangilia
Abdulrahman Kinana akiwa katika bajaji iliyomchukua

Nape Nnauye akiwa katika Bajaji iliyombeba
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakiwapungia mikono wananchi wakati wakielekea kwenye mkutano.

Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa kuteuliwa akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wakiwa katika meza kuu.
Umati wa watu waliohudhuria katika mkutano huo.
Kada wa CCM aliyejiunga na CCM hivi karibuni akitoka chama. cha CHADEMA Braison Mwasimba akiunguruma katika mkutano huo
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akimwaga sumu katika mkutano huo.
Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akiwaimbisha wananchi katika mkutano huo.
Msanii wa muziki wa kizazi Kipya Michael Senka mashairi jukwaani wakati mkutano huo ukiendelea leo jioni.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akitolea ufafanuzi wa mbolea ya Minjingu ambayo imekataliwa na wananchi wa mkoa wa Mbeya huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza kwa makini

Kada wa Chama cha Mapinduzi Tambwe Shitambala akizungumza katika mkutano huo.
 
Hofu kubwa yakikumba chama cha Mapinduzi.
°Waamua kutumia bajaji mitaani.
°Wajifananisha na Wakulima na Wafanyakazi
°Wagawa tshet kwa lazima.
°Watumia Polisi kutisha wana Mbeya.
 
Ulaghai unapofika kileleni huko ndiko kwenye point of no return zaidi ya kuparanganyika na kuanza ulaghai tena upya.

CHADEMA kimewalaghai wananchi kwa muda mrefu na kwa sasa kimefikia kikomo cha ulaghai ambapo kwa wananchi wameanza kuufahamu ukweli wa sababu ya CHADEMA kuwepo kwenye uwanja wa siasa.

Kwa sasa wameanza hata kuchakachua picha za kwenye mikutano kama walivyochakachua kuhusu mkutano wa Dr. Slaa wilayani Kahama jana

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

CHADEMA ni kampuni ya watu fulani fulani wanaotumia siasa kujitajirisha. Ole wako uwahoji kuhusu matumizi ya pesa za ruzuku. That will be the end of you as CHADEMA member.

These people are just political profiteers.

Waacheni wafu wa siasa mdani ya CHADEMA wazikane.
 
Weka mbazo hazijachakachuliwa tuzione mnadanganya watu kupanda bajaji kumbe maV8 mmeyaweka hotelini na vimada vyenu mmebakiza mwaka tu muondoke
 
Sasa mmeanza kufanyia mikutano sokoni na kuleta watu na bajaji badala ya fuso siyo? safi sana

Mkuu Asha Mohamed nimeamini kamera za maccm zina uwezo wa ku-triple idadi ya watu. Nilikuwepo kwenye wanja wa Shule ya Msingi RuandaNzovwe lomba Jana, kwanza zilitangulizwa bodaboda na bajaji kujazwa kwenye uwanja na ndipo watu wakajipachika kati yabodaboda na bajaji ili uonekane uwanja kujaa. Pia watu waliohudhuria robotatu walikuwa ni makada wa ccm kutoka vijijini, rejea uzi wangu nilioweka humu jana "maccm wamekuwa astaarabu Mbeya kwa kuwaleta watu kwenye mkutano wao kwa kutumia min bus aina ya Hice". Kwa jumla idadi ya mahdhurio ya jana ni 1/10 ya watu wanao hudhuria CHADEMA akiwa na mikutano yao katika uwanja huo.
 
Wadanganyeni ambao hawajaiona aibu yenu apa mbeya jana, huu mkoa hamuuwezi mtachakachua sana mapicha ila fundisho mmelipata jana mbeya hatudangay+ki
 
Ulaghai unapofika kileleni huko ndiko kwenye point of no return zaidi ya kuparanganyika na kuanza ulaghai tena upya.

CHADEMA kimewalaghai wananchi kwa muda mrefu na kwa sasa kimefikia kikomo cha ulaghai ambapo kwa wananchi wameanza kuufahamu ukweli wa sababu ya CHADEMA kuwepo kwenye uwanja wa siasa.

Kwa sasa wameanza hata kuchakachua picha za kwenye mikutano kama walivyochakachua kuhusu mkutano wa Dr. Slaa wilayani Kahama jana

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

CHADEMA ni kampuni ya watu fulani fulani wanaotumia siasa kujitajirisha. Ole wako uwahoji kuhusu matumizi ya pesa za ruzuku. That will be the end of you as CHADEMA member.

These people are just political profiteers.

Waacheni wafu wa siasa mdani ya CHADEMA wazikane.

Uzi wa Kinana na Nape lakini CHADEMA inatajwa mwanzo mwisho.
 
Hata mkikusanya viongozi wote wa mkoa na wa kitaifa, mbeya sio yenu. Tuacheni wenyewe na chama chetu.
 
1424452_10153520600210273_239004554_n.jpg
 
Ulaghai unapofika kileleni huko ndiko kwenye point of no return zaidi ya kuparanganyika na kuanza ulaghai tena upya.

CHADEMA kimewalaghai wananchi kwa muda mrefu na kwa sasa kimefikia kikomo cha ulaghai ambapo kwa wananchi wameanza kuufahamu ukweli wa sababu ya CHADEMA kuwepo kwenye uwanja wa siasa.

Kwa sasa wameanza hata kuchakachua picha za kwenye mikutano kama walivyochakachua kuhusu mkutano wa Dr. Slaa wilayani Kahama jana

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

CHADEMA ni kampuni ya watu fulani fulani wanaotumia siasa kujitajirisha. Ole wako uwahoji kuhusu matumizi ya pesa za ruzuku. That will be the end of you as CHADEMA member.

These people are just political profiteers.

Waacheni wafu wa siasa mdani ya CHADEMA wazikane.

Hivi hii ni ziara ya kuijenga CCM au ya kuinanga CHADEMA. Hebu hesabu hii post yako kuna maneno mangapi CCM, na mangapi CHADEMA...

Halafu wenye CHADEMA yao wametulia zao kimya... hata hawakumbuki kuna mtu anaitwa Kinana anaoita huko Mbeya...
 
Nashindwa kuelewa mmenda kuiua chadema au mmeenda kukagua miradi yenu.

Hivi hamwezi kwenda sehemu bila kutaja CHADEMA??
 
Hofu kubwa yakikumba chama cha Mapinduzi.
°Waamua kutumia bajaji mitaani.
°Wajifananisha na Wakulima na Wafanyakazi
°Wagawa tshet kwa lazima.
°Watumia Polisi kutisha wana Mbeya.

yaan huu ni ulaghai mkubwa wa kisiasa,na katib wa ccm iz good to manipulate people's mind,et mara wanatumia jembe la mkono,mara wamekaa kwenye mkeka wanakunywa chai,hapo wamepanda bajaj kujfanya,wao pia ni common wananch,kwanin siasa za kisanii,watu wana shida kaz kuwaigizia,CCM shame on you!
 
Kandoro mwenyewe kavaa gwanda kwa kuwa anajua Mbeya hawadanganyiki ni wanamageuzi wa ukweli.
Kinana na Nape wanafanya tu mchezo wa kuigiza, mara wapande baiskeli, mara wapande bajaj, mara wale wali maharage, wale chai na vitumbua wamekaa chini, wabebe vitofali na kulima na jembe la mkono, yooote hayo majibu watayapata 2015
 
Huyo jangili namba moja amechanachana zana za ujangili au?
 
Back
Top Bottom