PICHA:Katibu Mkuu wa Chama Kipya Cha Alliance For Democratic Change (ADC)Ziarani Mkoani Mwanza

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=1]Katibu Mkuu wa Chama Kipya Cha Alliance For Democratic Change (ADC)Ziarani Mkoani Mwanza[/h]

DSC-41.jpg

Waendesha pikipiki wakiongoza mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) Lucas Kadawi Limbu,alipowasili Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Igoma Jijini hapa.
DSC-21.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC),Lucas Kadawi Limbu mwenye suti katikati ,akiwapungia mkono wafuasi wa chama hicho baada ya kukagua kikundi cha ngoma muda mfupi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza mwishoni mwa wiki.Limbu alifanya mkutano wa hadhara na kupokea wanachama wapya katika Kata ya Igoma Jijini hapa.Kushoto ni Kamishin wa chama hicho Kanda ya Ziwa Shaaban Itutu.
DSC.11.jpg

Katibu Mkuu wa cha Democratic For Change (ADC) Lucas Kadawi Limbu akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Igoma Jijini Mwanza.


PICHA NA MASHAKA BALTAZAR -MWANZA

 

Mapikipiki KIBAO; Lakini Watu Wanaotakiwa kusikiliza HOJA za CHAMA KIPYA 5?
Kwanini kupoteza pesa kwa MAPIKIPIKI???
 
Hizo hela wanazopewa waendesha pikipiki si zingesaidia kuweka Panadol kwenye zahanati ya kata!!
 
hakuna kitu hapo,utakosaje 2000 ya kukodi bodaboda kwa ajili ya kushawishi umma kuwa unakubalika.hesabu hizi ni rahisi sana mfano. 2000x30=60,000 ,elfu sitini ndo imetolewa na ADC Kuweka boda boda hapo.
kwa maana hiyo huu ni mkumbo tu unaosindikiza wanaosindikzwa bila kufanya hesabu kama hizo hapo juu,
 
hakuna kitu hapo,utakosaje 2000 ya kukodi bodaboda kwa ajili ya kushawishi umma kuwa unakubalika.hesabu hizi ni rahisi sana mfano. 2000x30=60,000 ,elfu sitini ndo imetolewa na ADC Kuweka boda boda hapo.
kwa maana hiyo huu ni mkumbo tu unaosindikiza wanaosindikzwa bila kufanya hesabu kama hizo hapo juu,

Umekokotoa gharama hizi kwa sababu ya uzoefu wako kukodi hizo bodaboda kwenye chama chenu cha maandamano ya kila siku?
 
A D C ni tawi la CCM, Ccm baada ya kuishiwa sera now wameamua kutumia mbinu chafu ya kupunguza wafuasi wa vyama pinzania!
 
Kuna haja ya kumwambia Tendwa hii bendera imefanana na Chama dume Chadema,ibadilishwe haraka sana,watanzania baadhi wanaweza wasiitofautishe na yetu.Mmmmmhh wamejaza nyomiii.
 
Kazi ipo chadema nao wlipiti huku tofauti ya chdema na hawa ni kuwa ADC wanatumika na CCM...
 
Back
Top Bottom