Picha: JK kwenye ghorofa liloloporomoka

Onyo,kuanzia leo ukiwa una safari au kutembelea maeneo ya K.koo hakikisha unavaa Helmet kwa usalama wako.
 
Nae anashangaa,,? Ukilaza huo.
hivi ajui kinachoendelea?
Angeongozana na m waziri au naibu waziri wa ardhi, hapo hapo kuwepo na Mkaguzi mkuu wa majengo awaulize kinachoendelea coz hiii ngonjela ya kupolomoka kwa maghorofa tumeshachoka nayo.
 
Usanii huu utaisha tu mwaka 2015.Mungu atusaidie kwani Taifa linaangamia kweupe.
Mheshimiwa Rais JK amezuru eneo la maafa pale kulipoporomoka ghorofa leo asubuhi.

attachment.php
 
Ndio mana nilikua namkubali sana Lowasa..angekua yeye hapo watu wangeshatema kazi na kufika mahakamani ila sikukuu wangekula gerezani...mm naona hii nchi ina udhaifu uliopitiliza sio kawaida...shame
 
Chanzo cha kuporomoka hili jingo la NHC ni sink hole per RPC Kova, baada ya kugundua Mkandarasi ni Kada wa CCM

Huo ni upuzi kwa kuwa ujenzi hauwezi kuidhinishwa bila vipimo vya kuona uwezo wa ground kuhold mzigo ni tani ngapi; kaona cnn juzi wakiongelea chumba kilichozamisha mtu ajili ya sinkhole ndo anaona ni magumashi ya kutuletea kwa kuwa ni wajinga. Sink hole ingedidimiza ghorofa kwenda chini ardhini na sio kuli- overthrow kama ilivyotokea
 
Huyu ni rais wa maneno si vitendo! Mulugo sasa anafurahi kwani anajua attention inahamia kwingine!
 
kuna watu walishahadharisha utitiri wa majengo yanayomea kila kukicha DSM
akaonya kama yanakaguliwa na kusimamiwa na wahandisi waliofuzu na kusajiliwa.
mengi tunaona vibao lakini kumbe mhandisi jina lake limetumika kusajili basi..
mafundi nao wezi wa cement,mafundi wanapiga cha juu,nondo za kujengea ni duni,
kila kona wizi wizi wizi...
ahh kumbe Kova ana sura ya namna ile anatisha, bora akivaa kombat lake
 
Halafu itabidi tuchimbe kwa undani ni makandarasi na washauri wa aina gani wanaojenga maghorofa kama nyumba za nyasi
 
Huyu ni mzee wa matukio, sioni ajabu kumuona hapo na hana jipya.

Tumuombe Mungu atufikishe 2015 salama, aondoke akapumzike kwao.
 
Ndio mana nilikua namkubali sana Lowasa..angekua yeye hapo watu wangeshatema kazi na kufika mahakamani ila sikukuu wangekula gerezani...mm naona hii nchi ina udhaifu uliopitiliza sio kawaida...shame
 
Tatizo siyo ufundi wa ujenzi, bali ni quality ya vifaa vyetu vya ujenzi hapa nchini. Nondo zinazotumika si za kiwango takiwa, wala simenti yenyewe ni siment feki. Tusilaumu wahandisi, tuangalie pande zotezote. Nchi yetu ni usanii pande zote na siyo upande mmoja. Jiulize, kwa nini wachina wakati wanajenga uwanja wa taifa walitumia nondo zao na simenti yao????? Hii ni kwa kuwa vifaa vyetu havikidhi kiwango cha kimataifa. Hivyo majengo kuanguka ni tukio lililo tegemewa. na bado tutaona mengi.
 
Nilivyoona kichwa cha habari Jk kwenye ghorofa lililopolomoka nilidhani Jk ni kitengo kikubwa kuliko vyote hapa nchini ktk shughuli za uokoaji.

Mkuu umenifurahisha. Unajua hawa watawala hawapewi kashkash na wananchi ndio maana wanajipeleka kila mahali. Angalau angezomewa ili kimkumbusha wajibu wake sio kushangaa maafa bali ni kuzuia
 
Back
Top Bottom