Picha: JK kwenye ghorofa liloloporomoka

Kimbelembele namuona akielezea kwa JK utafikiri alikuwepo wakati ghorofa linadondoka...lakini nampenda kwani anajua kuishi mjini

...Kovu, sorry KOVA kwa kuuza sura ni balaaa. Jamaa anajua timing ile mbaya....shida yake kubwa anaendeshwa na kuagizwa toka Lumumba....

Kamanda alikuwa Tibaigana, alikuwa haangalii makunyanzi, haangalii "Muadhini wala Mteka Maji Msikitini" kwake yeye, Sheria Kwanza mengine baadae....

Sijui kama anasifiwa na Kibonde wa Clouds FM, ila Mchechu amekuwa akisifiwa na wengi kwamba ni mchapa kazi licha ya gharama kubwa ya nyumba za NHC hivi sasa

Kwa hili hasameheki, aje ajieleze

Kusifiwa na Kibonde tu ni sababu tosha ya kutufanya tuwe suspicious.

Nishamsema hapa kwamba hajaridhisha watashi kuhusu jibu la gharama kubwa za nyumba za NHC. It seems there is some sort of a trade cabal if not an outright cartel.
 
Huy md wa NHC yuko kisiasa siasa zaidi
yuko full masifa
last time aliandaa mdahalo Karimjee hall
na wakazi wa NHC kujadili wauziwe au wasiuziwe nyumba za NHC
kumbe alishaamua kuwa hawauziwi lol

sasa hili la kuingia partnership na watu binafsi na kuwaacha hao watu binafsi
wajifanyie wanalotaka bila NHC kujali quality ndo nalishangaa sasa

achilia mbali kwamba ile old Daresaalam ndio ina dsapear so fast
na infrastructure za City center za ku replace two stories building with a 20 stories building haziruhusu that much
hii nchi bana ...

Kipanya alipowachora NHC kuwa ni shirika la umma ambalo ni 'irrational' kufuatia kuuza nyumba za bei nafuu kwa mil.70
hatua aliyochukua Mchechu ni kuondoa matangazo yote Mwananchi

baada ya hili,sioni maamuzi thabiti atakayochukua as a way forward
 
Boss,

Una habari kuwa client hapo ni NHC?

Yaani jengo la taasisi ya umma linajengwa kiholela hadi linaanguka na kuchukua roho za watu?!

Huyo MD wa NHC ana maelezo gani?

Hasara iliyopatikana nani atafidia?

wewe kwanza tafuta uhusiano wa Nehemiah na P Luhanjo ndo useme kwamba dhaifu anaweza peleka m2 kisutu!
 
Kusifiwa na Kibonde tu ni sababu tosha ya kutufanya tuwe suspicious.

Nishamsema hapa kwamba hajaridhisha watashi kuhusu jibu la gharama kubwa za nyumba za NHC. It seems there is some sort of a trade cabal if not an outright cartel.

Kibonde alikuwa na kipindi kwenye TV kinachoitwa "Maisha ni nyumba" ambacho alikuwa akiipigia debe NHC.

Kwa hiyo kumsifu kwake huko Clouds itakuwa ni kuendelea kuchumia tumbo tu

Kama haiingii akilini kwa apartments za NHC kuuzwa kwa milioni 350 kila moja, inakosa chembe ya mantiki kwa jengo la NHC kuanguka likiwa kwenye ujenzi

Anatueleza nini huyu?

Wale wanaoishi kwenye majengo ya NHC hasa haya yaliyojengwa hivi karibuni wawe na hofu na usalama wao?

Ana-justify vipi hili la kuanguka kwa jengo lake?
 
Anaenda kufanya nini? Au anakagua jinsi alivyoshindwa kuwawajibisha watendaji kazi katika nyanja zote mpaka tunafikia hapa? Kesho wataunda tena tume ingine kuchunguza, wale pesa za walipa kodi hakuna linalobadilika. Anataka kuzika wangapi mpaka aelewe ya kwamba uongozi mbovu katika nyanja zote ndiyo uliotufikisha hapa? Hivi ni kweli hakuna watu wanaopaswa kusimamia ujenzi na kudhibiti ujenzi holela uliokitihiri kwenye miji yetu? Watu wanahonga wanapewa vibali, wahandisi mradi wamelipwa hawajali wanapoidhinisha na kusimamia majengo kama haya, tunakwenda wapi? Hakuna jipya na kwa uchungu ninaweza kusema hili halitakuwa la mwisho. Ikiwa tunao hata mawaziri wasiokidhi viwango vya kupewa wadhifa huo (below standard) sembuse hao wahandisi wa kusimamia ujenzi?

Dar high rise buildings at risk of collapsing
 
Huy md wa NHC yuko kisiasa siasa zaidi
yuko full masifa
last time aliandaa mdahalo Karimjee hall
na wakazi wa NHC kujadili wauziwe au wasiuziwe nyumba za NHC
kumbe alishaamua kuwa hawauziwi lol

sasa hili la kuingia partnership na watu binafsi na kuwaacha hao watu binafsi
wajifanyie wanalotaka bila NHC kujali quality ndo nalishangaa sasa

achilia mbali kwamba ile old Daresaalam ndio ina dsapear so fast
na infrastructure za City center za ku replace two stories building with a 20 stories building haziruhusu that much
hii nchi bana ...
Yap ni kweli. Pia maengineers wanahusika plus wanaoaprove ujenzi. Yaani hapo kuna msululu mrefu. Lkn nani anajali yote haya, hivi leo limeanguka hilo je ujenzi mwingine unaoendelea sehemu zingine umekaguliwa . Na hii si mara ya kwanza kuanguka jengo refu nakumbuka miaka kadhaa imepita kuna jengo lilianguka na watu walipoteza maisha. Ni hatari sana kuchanganya siasa na utaalamu au kuweka maslahi mbele badala ya ubora na uimara wa jengo. Kariakoo kuna ujenzi mbovu usipime, wahusika wanaona lkn wanafumba macho na baadae wanakuja kupretend hawakuona . Mungu atusaidie tu
 
Ndo zake hizo
atatoa pole na kuzuru eneo
na kwenda msibani
halafu yataishia hapo hapo
Ndio maana kuna mgawanyiko wa madaraka/majukumu hatua zitachukuliwa pale ambapo ripoti itamfikia mezani.

Ndio maana kuna mgawanyiko wa madaraka/majukumu hatua zitachukuliwa pale ambapo ripoti itamfikia mezani.

Ina maana hajapewa ripoti zote hizo?
Je ile ripoti ya mwaka 2008 mpaka leo bado hajaipata?
Sikio la kufa halisikii dawa...
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!
 
Ina maana hajapewa ripoti zote hizo?
Je ile ripoti ya mwaka 2008 mpaka leo bado hajaipata?
Sikio la kufa halisikii dawa...
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!
Siku zote kaa ukifahamu kuna uongozi na utawala.Si vibaya ukajifunza sifa za uongozi na utawala.
 
Bado jengo la Bunge Dom, mana walisema kuna sehem linavuja, sio muda mref litashuka chin...!!

Jk ashukuru magogon palijengwa na wakolon, pangejengwa wakat wake, sijui.....!!
 
Siku zote kaa ukifahamu kuna uongozi na utawala.Si vibaya ukajifunza sifa za uongozi na utawala.

Nashukuru mkuu kwa kunipa somo.
Nitaongeza ujuzi wangu kwa kuwa mimi ninafundisha somo hilo kwenye chuo kimoja huku ughaibuni, nafikiri ninahitaji kujifunza zaidi kutoka kwako na wanajamvi wengine. Elimu haina mwisho, shukrani za dhati mkuu!
 
Back
Top Bottom