CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 6,087
- 5,352
==
Nimekutana na hii taarifa kwenye group songezi la Whatsapp Kwa ruhusa yenu naomba tuijadili Kwa uwazi na haki,
Mimi mleta mada Kwa namna bwana huyu alivyoituliza Kilosa naona kama nafasi aliyonayo huyu DC Kwa sasa inambana sana atafutiwe nafasi nyingine ya juu saizi yake ili Taifa liweze kunufaika na uwezo wake huu wa kuacha alama isiyofutika kila anapopelekwa.
===
Taarifa yenyewe ni hii:
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka ameongoza viongozi mbali mbali, wadau wa maendeleo, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyoka kimkoa wilayani Kilosa.
Katika maadhimisho hayo DC Shaka alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Kighoma Malima ambapo amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya majanga na maswahiba mbalimbali ambayo yanapelekea kuharibu utu wao mbele ya jamii sambamba na kuwakatisha tamaa katika kutimiza ndoto zao za baadae.
"Kauli mbiu ya mwaka huu ni Haki za mtoto , tulipotoka, tulipo tuendako ambayo inaitaka jamii kwa ujumla kufanya tafakuri ya kina juu ya upatikanaji wa haki za watoto tangu zilipoainishwa katika Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008" alisema Shaka
Hata hivyo Dc Shaka ameendelea kutoa msisitizo juu kuwaelimisha na kuwakumbusha wazazi, walezi na watoa huduma wote wajibu wao katika kutekeleza haki tano za msingi za mtoto ambazi ni haki ya kuishi, haki ya kuendelezwa, haki ya kulindwa,hski ya kushiriki na haki ya kutobagliwa.
"Niendelee kuwahakishia kuwa serkali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na kuweka mazingira rafiki na shirikisha itaendelea kuhakikidha haki nilizozianisha na ulinzi wa myoyo unapatokana katika ngazi zote" Alisisitiza Shaka.
Recall:JAMII YATAKIWA KUWALINDA WATOTO DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI
===