Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,552
Anaenda kama muwakilishi wa vyama vya upinzani nchiniHivi John Cheyo anaenda kama nani ? hii nchi hela zinaliwa kijinga sana .
Wamechukua nafasi ya Rais,mkewe na mpambe nadhani.Rais mstaafu Jakaya Kikwete ameondoka kwenda Harare nchini Zimbabwe kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais mteule wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa.
Rais Kikwete ameondoka leo asubuhi Agosti 26, 2018 kwenda kuhudhuria sherehe hizo zinazofanyika katika uwanja wa michezo wa Taifa Mjini Harare akimwakilisha Rais John Magufuli.
Akizungumza kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Kikwete amesema Tanzania na Zimbabwe zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kindugu.
Amesema katika kipindi ambacho Zimbabwe ilikuwa ikidai uhuru, baadhi ya wananchi wake waliishi Tanzania hasa wanachama wa Chama cha Zanu-PF na kupata mafunzo nchini.
“Baadhi ya wanajeshi wetu wameshiriki pamoja na wanajeshi wa Zimbabwe katika harakati za ukombozi,’’ amesema Kikwete.
Taarifa ya Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu aliyoitoa kuhusu safari hiyo inasema Kikwete ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na mwenyekiti wa UDP, John Cheyo.
Rais Mnangagwa anaapishwa leo kuongoza Taifa la Zimbabwe baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika Julai 30, 2018.View attachment 847176
Sent using Jamii Forums mobile app
kachaguliwa na nani ?
Kuchagulia kiaje, yeye ni mwenyekiti wa chama gani sijui cha upinzani. Kwenda Zimbambwe kateuliwa na President kuwakilisha rasmi upinzanikachaguliwa na nani ?
Halafu cha kushangaza huyo Cheyo ni Mwenyekiti wa Kudumu wa hicho chama na wala sijawahi kusikia uchaguzi wala mkutano Mkuu wa hicho chama wala kumfahamu Katibu Mkuu wake lakini hatusikii makelele ya Lumumba hapa.Inamaana hiyo ndege inawapeleka mpaka Zimbabwe na kurudi....?
Bila shaka hiyo ni ndege ya Rais...kwa hiyo Cheyo ameteuliwa ili kuonyesha Magufuli ana mahusiano mazuri na wapinzani.
Wakati ni kinyume chake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama mwakilishi wa WapinzaniHivi John Cheyo anaenda kama nani ? hii nchi hela zinaliwa kijinga sana .
Katiba yao imeshasema kuwa utawala wao ni wa kiimla.Halafu cha kushangaza huyo Cheyo ni Mwenyekiti wa Kudumu wa hicho chama na wala sijawahi kusikia uchaguzi wala mkutano Mkuu wa hicho chama wala kumfahamu Katibu Mkuu wake lakini hatusikii makelele ya Lumumba hapa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kweli mimi huwa naikubali sana UDP, wanajua kizipiga siasa bila chuki tofauti na CUF na Chadema ninaimani UDP kitakuja kuwa chama kikuu cha Upinzani.
Kikwete anaenda kama Rais.Hivi John Cheyo anaenda kama nani ? hii nchi hela zinaliwa kijinga sana .