Hayo ndio matokeo ya kazi nzuri anayojivunia JK. Unafika mahali unawashangaa sana watu wanafiki wanaojifanya hawazioni shida hizi, na bila aibu wanaisifia na kuitukuza CCM. Nakereka sana na watu wa aina hii.
Natamani ningekuwa na uwezo kutengeneza posters zenye maandishi " Maisha Bora Kwa Kila Mtanzania".
Kukusanya picha za maisha bora haya na kuzipachika sambamba na zile za Waheshimiwa na Mahekalu/mashangingi yao.
Chini unaandika
1.Vote CCM- Vote JK- kuyaendeleza au
2.Vote Chadema Vote Dr. Slaa- kuyabadilisha.
Posters hizo kuzibandika kila mahali, watu wezeze ku- compare & contrast
Wafanye uamuzi sahihi October 31.
Na bado wahaahidi watajenga Barabara za lami kuzunguka mlima kilimanjaro. Bajaji 400 Mbeya. SUBILI TUJICHANGANYE TUWAPE KURA, MWENDO MDUDO KWENYE BEMBEA NA MKEWE. SHIDA KUBWA NI HAYA YANAYOJADILIWA HUMU KUISHAI HUMU HUMU NA HIZI PICHA NI FACTS AND FIGURES KUTHIHIRISHA KINACHOSEMWA NA HALI HALISI YA WATANZANIA WALIOWENGI. BAYA ZAIDI NI HAO KWENYE HIZO MACHELA NA TOLOLI WAKITOKA HAPO WANAIMBA WAO NAMBALI ONE DAMU. HURUMA INAISHA HAPO HAPO.
Punguzeni jazba jamani na muitumie kura yenu kwa umakini siku ya kupiga kura,ila shingangai unaweza kukuta hawa hawa watanzania kwenye picha ndio watakuwa wa kwanza kusahau yaliyowakuta na kufanya makosa.
Tetesi zinaonesha kuwa hata tukipiga kura kuleta mabadiliko hakutakuwa na mshindi atakayetangazwa mbali na Jk. Sababu ni kuwa kuna wizi mkubwa umeandaliwa na CCM so inabidi tulinde kura zetu maana kuna uwezekano wa kushinda uchaguzi wa Urais na akatangazwa mwingine.