Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 872
Sijawahi kuona uwanja wa Ndege mbaya na wenye hatari kubwa kwa maisha ya watumiaji wa viwanja vya ndege kama huu wa Mbeya uliopo katikati ya mji wa Mbeya.Nilistaajabia sana kuona mji mkubwa kama Mbeya bado ulikosa uwanja wa Ndege wenye hadhi kama huu.Kwa hakika uwanja wa ndege wa Songwe unapaswa uishe haraka sana na tena nasema serikali ilichelewa sana kujenga uwanja mwingine.Leo ninaposikia kuna ajali ya ndege katika uwanja huu sishangai tena.
Kwanza uwanja huu wananchi wanakatiza tu katikati ya uwanja kwa shughuli zao binafsi.Waendesha pikpiki wanapita hapo, magari yanakatiza tu kiholela, watu pia usiseme.Kutokana na uwanja huu kuwa katikati ya makazi ya watu imekuwa ni kawaida tu sasa hata kukaa na kupiga stori na wahusika wasichukue hatua zozote zile.
Barabara ya kurukia ndege ni hovyo na wala huwezi kuita ni runway.Mashimo ni mengi sana.Hapa ina maana ndege ikikosea ikaacha njia basi itaenda kupiga break kwenye makazi ya watu jambo ambalo ni la hatari. Wenyeji wanasema kama kuna ndege inataka kutua au kuruka basi itapigwa filimbi kuashiria kuna ndege hivyo watu watawanyike.Hii ni hatari mno,sijui kwa nini Mamlaka ya Anga Tanzania haiufungi uwanja huu.Tazama picha mbalimbali za uwanja huo.Kuna picha zingine hazijawa clear sana.