Picha: Dr. Slaa,Lissu na Suzan Lyimo watikisa SAUT

Picha: Dr. Slaa,Lissu na Suzan Lyimo watikisa SAUT

Nicholaus Kilunga

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2014
Posts
1,188
Reaction score
570
Wakuu,

Pamoja na kwamba magamba kupitia kwenye ofisi ya meya na ofisi ya mkurugenzi walitunyima kiwanja cha kufanyia mkutano ambapo awali tulikuwa tumepewa ruhusa kufanya mkutano kwenye eneo la shule ya msingi Nyamalango,bt gafla tu ikatolewa barua kwamba viwanja vyote vilivyopo chini ya mkurugenzi wa jiji haviruhusiwi kufanyia mikutano ya kisiasa,na kupelekea mzee mmoja alipoamua kutupatia uwanja wa kufanyia mkutano,hali iliyomlazimu mzee huyo ambaye kamanda huyo alilazimika kuvuna mahindi yake ili kutoa nafasi kwa mkutano huo kufanyika.

Pamoja na kwamba mkutano wetu wa CHADEMA uliokuwa umeandaliwa na CHADEMA SAUT(CHASO SAUT) ulianza mapema mida ya saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni,jumrisha jua nk,lakini shughuli ya kutoa elimu ya umma iliendelea kama kawa na makamanda a.k.a mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu,Suzane Lyimo ambaye ni waziri kivuli wa elimu alifunika mbaya,zaidi rais wetu wa awamu ya 5 Dr Slaa alitoa nondo za ukweli kiasi kwamba wasomi wa SAUT walimpongeza sana hasa pale aliposema wasomi inapaswa kujivunia kwa kile walichonacho kichwani na si vyeti.

Akaendelea kusema elimu yetu kwa sasa inawatayarisha wasomi kuwa wasomi wa vyeti na kitu kilichomo kichwani,akasisitiza umuhimu wa wasomi kuwa wazalendo wanaopinga vitendo vya uhujumu ,ufisadi na wanapaswa kwenda kuitumikia jamii.

Lissu akisema mchakato wa katiba mpya ni kama jini lililokuwa ndani ya chupa na sasa wamelifungulia jini hilo na likatoka nje,sasa lazima tuwe makini la sivyo litatumaliza.

Huku akisema CCM sikuzote wanasema rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na jaji Warioba kwamba ni rasimu mbovu,lakini ukiwauliza ubovu wa rasimu hiyo upo wapi,na kwanini walianzisha mchakato huo tena kwa kumpa kada wao nafasi hiyo huku,wakijikita kuutetea muungano wakati hawawataki wazanzibar.

Suzani Lyimo akiongelea ubovu wa elimu na mfuumo ambao kwa makusudi unaendelea kuasisiwa na CCM ili kuua ndoto za watoto wa maskini wa nchi hii kupata elimu bora wakati huo watoto wao wanasoma kwenye shule bora.

Pamoja na mambo mengine Dr Slaa aliwakabidhi vyeti vya uanachama wanafunzi wa mwaka wa 3 na 4 wanaomaliza chuo ikiwa ni pamoja na viongozi wa tawi la CHADEMA SAUT.


DSCN4363.JPGDSCN4327.JPGDSCN4327.JPGDSCN4330.JPG



DSCN4349.JPGDSCN4295.JPG
 
viongozi wa chadema wamejaa roho mbaya. Taifa lina msiba wao wanaendelea na mikutano yao uchwara
 
viongozi wa chadema wamejaa roho mbaya. Taifa lina msiba wao wanaendelea na mikutano yao uchwara
Kazi kweli kweli! Kwa hiyo unataka tutangaziwe siku ya mapumziko baada ya mama Zitto kufariki? Yale mabomu ya Arusha yaligoghalimu maisha ya watu wengi wasio na hatia mbona hatukutangaziwa siku ya mapumziko? Mbona bunge halikuahirisha shughuli zake?!!
 
Kazi kweli kweli! Kwa hiyo unataka tutangaziwe siku ya mapumziko baada ya mama Zitto kufariki? Yale mabomu ya Arusha yaligoghalimu maisha ya watu wengi wasio na hatia tulitangaziwa siku ya mapumziko? Bunge liliahirisha shughuli zake?!!

huo mkutano una faida gani zaidi ya majungu tu?
 
acha kuongopea watu bhana kulikua na watu kama 250 hvi kwaniliyo yaona Jana chadema kwaheri
 
viongozi wa chadema wamejaa roho mbaya. Taifa lina msiba wao wanaendelea na mikutano yao uchwara

msiba wa nani vile kila moja wetu atakufa; ukombozi pia ni jambo jingine dhidi ya mkoloni mweusi
 
huo mkutano una faida gani zaidi ya majungu tu?
Povu la nini? Si uende mahakamani iwapo unahisi mikutano ya CDM inakukera? Sasa unamshitaki nani hapa JF? Au kuna mtu kakuambia hapa Jamii Forums ni mahakamani?
 
Kazi kweli kweli! Kwa hiyo unataka tutangaziwe siku ya mapumziko baada ya mama Zitto kufariki? Yale mabomu ya Arusha yaligoghalimu maisha ya watu wengi wasio na hatia mbona hatukutangaziwa siku ya mapumziko? Mbona bunge halikuahirisha shughuli zake?!!

Asante huyu Mhaya mpuuzi (Abakorakamo- ni misemo ya kihaya). Who is mama yake Zitto in the national political scene! Tutamlilia kama mama yetu na si msiba wa taifa kama huyo mhaya alivyojitangazia nshomile!
 
Back
Top Bottom