Nicholaus Kilunga
JF-Expert Member
- Feb 15, 2014
- 1,188
- 570
Wakuu sasa hivi kuna mkutano unaendelea uliondaliwa na CCM ngazi ya wilaya mbali na kukosa watu kituko kikuu ambacho kinaweza kuzua mtafaruku ni maneno ya katibu wa wilaya CCM ,anasema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuwasemea waamini wao kwani hata wao hakuna msafi,ameenda mbali zaidi kwa kumtaja askofu flani jina kapuni kwamba alichaguliwa kwa rushwa.
Mkutano huu wa CCM umeandaliwa kujibu mapigo kufuatia mkutano mkubwa wa wazi ulioandaliwa na makanisa yote ya kikristo ya wilaya Kibondo siku ya jumapili ,ambao pamoja na mambo mengine katika mkutano wa umoja wa kidini uliwahamasisha waamini wao waipigie kura ya hapana katiba pendekezwa.
Sasa wananchi wamekerwa na matamshi yake na wameanza miguno.