Picha: Bodaboda na Simba uso kwa uso

Teh teh teh nadhani waliokuwa kwenye hizo ndinga walivunjika mbavu kwa kicheko.

Vipi jamaa hakuomba lifti?

Watu wabaya wakaandaa vitecno vyao warekodi mtu akitafunwa na simba ili wakapost insta. Teh teh teh.
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
 
Hahahhaa animecheka sana sana ila ni hatareeeeeee, sipati picha jinsi alivyofunga breki dah, kifo sijui kina siri gani aiseee
 
Duuh, huyu bodaboda nimgeni nahiyo njia, au jeuri tuu. Njia kama hii ni hatari kwa kutumia Usafiri kama bodaboda au baiskeli.
 
Daah, yaani nimecheka weee, basi! Huyo boda najua hakufika salama, lazima alipata ajali tu, kwa 7bu hata anavyoongeza mafuta anajua mnyama yuko nyuma!
 
haaa haya madude yanatisha halafu hili la kike lilishiba au lilikuwa linangojea mchepuuko maana kama lingekuwa na njaa na watoto lingemtoa nduki limkamate ana bahati akatambikie
 
Mbali na huyo wa bodaboda kujisaidia haja yoyote ile iwe ndogo au kubwa ila sipati picha kama anageuza tu kapikipiki kanazima na hiv wanapenda kuweka mafuta robo lita duuu,,! Mungu mkubwa na leo huyo jamaa atakuwa shuhuda wa hiyo sentence
 

Ukiendelea hivi utakuwa chakula ya wanyama
 
Akiri za waendesha bodaboda bwana....weee umekuta wenzako wawili watatu wamesimama, hata kujiuliza kulikoni hakuna...

Wengine wanaudhi tena barabara za vijijini...! wawezakuta wengine wanapiga stori tu.

Na kama wangekuwa wema (hao waliokuwa wamesimama wakisubiri simba atoke barabarani) walitakiwa wamuwashie indikiketa ya kumzuia asipite(dereva wa bodaboda)...na kama wangeona hajajari hilo walitakiwa wamsimamishe kwa kutumia mkono alipokaribia maeneo hayo. Lazima unapokuwa barabarani usaidie na kuimarisha salama na maisha ya watumiaji wa barabara wa kada zote (watembea kwa mguu, dereva bodaboda na kadhalika).

Mimi sitashangaa ikija kugundulika kuwa kwenye tukio hilo ni gari moja tu lilikuwepo mahali hapo na mwendeshaji wa gari hilo alishindwa kumpa tahadhari dereva wa bodaboda ili apate nafsi ya kupata picha ya kurusha kwenye mtandao kama hapa JF...!

Watu wamerukwa na utu siku hizi.
 
Hii picha ni ya mwaka...hongera sana kwa kunasa hili tukio, Kama ulirekodi video unaweza kupeleka kwenye vituo vya tv wakairusha ili iwe fundisho kwa madereva wengine wa bodaboda.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…