Watu mkuu wamesha mpigia picha alipo.Inasikitisha sana,kweli damu nzito kuliko maji,walezi/wazazi wanahaha kumtafuta huku walimwengu wanasema sasa hivi analiwa kimasihara dah.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Sidhani hata hao wanaosema kama wana watoto, maana ikiwa una mtoto hata wa nduguyo unayemlea tu, ingelitosha kujaribu kuvaa viatu vya wazazi hawa na wangeelewa uzito wa kupoteza mtoto
Mwaka 2011 nikiwa natoka sofya (kasulu) kuelekea maeneo mjini mida ya saa 1 usiku nikakutana na katoto kadogo ka kike kakiwa peke yake, kwa umri wake jumlisha maeneo nilipomkuta na uelekeo aliokuwa anaenda ikanitia shaka, nikamuuliza akanijibu anaenda nyumbani, akaniambia mtaa tu, nilizunguka na yule mtoto mpka saaa nne usiku lakini hatukufanikiwa kupapata anapo ishi.
Nikarudi nae nikampa chakula akala akalala, ndo wazo la kwenda msikitini kutangaza likaja, nafika msikitini wananiambia mpaka wmuone mtoto ndo watangaze hapo ikabidi nirudi kwa mwenyekiti nikampa taarifa akaniambia, as long as ashalala wacha tu apumzike kesho tutafanya jitihada z kuwapata wazazi wake.
Usiku ukapita tumeamka tukaandaa kifungua kinywa, ile tunapata chai, mama wa mtoto anakuja. Kumuuliza akasema wameenda msikitini wakaelekezwa, maana pale msikitini niliacha anuani yangu. Yule mama alipo muona mwanae alilia asee.
Hapo ndo wakasimulia dogo alienda kwa mjomba wake na huko watoto wa mjomba wake wakampiga, dogo akaamua arudi nyumbani, bahati mbaya ni kwamba dogo ni mgeni pale coz pale kasulu ni kwao na mama yake na hapo hajui chochote, dogo akajikuta anapotea.
Kama wazazi au walezi tunapaswa kujua hali ya huyu binti, anaishi na nani, mahusiano yake na hao anaoishi nao kwa sasa. Anaweza kuwa kaondoka kwa sababu ya magumu anayopitia hapo nyumbani, hivyo kaamua aondoke akatafute unafuu, ahalafu bila kutumia akili kwa ufanisi, mtu anahukumu kwa mtazamo wake. Mungu atusamehe sana