PICHA: Binti amshangaza mpenzi wake kwa kumnunulia gari siku ya Valentine

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Binti mmoja nchini Kenya amempa mshangao ‘surprised’ mpenzi wake wa kiume kwa kumnunulia gari mpya aina ya Mercedes katika siku ya leo ya wapendanao maarufu kama ‘valentines day.’

28056031_997174100448831_13875309910269401_n.jpg
Binti huyo aliyejulikana kwa jina la Fridah Kariuki ambaye ni mwana mitindo aliamua kumnunulia Michael Musyimi ambaye ni mpenzi wake zawadi hiyo kama ishara ya upendo wake kwake.

Kwa mujibu wa Pulselive.co.ke, Fridah Kariuki mwenye umri wa miaka 20 ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Methodist nchini Kenya (KeMU) ambaye amesema, alimkopa baba yake fedha kwaajili ya kumnunulia mwanamme wake huyo gari alililokuwa akilitamani siku zote.

Wawili hao wanaopendana wamekuwa katika uhusiano huo kwa miaka minne na wamesema wanampango wa kuishi pamoja.

Licha ya mshangao huo wawili hao wameweka wazi kuwa uhusiano wao huo unapewa ushirikiano wa karibu na wazazi wao.


27973162_997172657115642_2769517376521410888_n.jpg

Chanzo: Azam TV
 
Kama Kenyaa sawaa. Sema huyo dada nae mkavuu bhanaa Achaa amuhongee jamaa kesho Jamaa apatee mkali zaidi yakee.
 
20ysr now na wana mahusiano kwa muda wa 4yrs so walianza akiwa na 16yrs. Hata Kenya kuna maigizo kumbe.
 
Back
Top Bottom