Mwalimu ajinyonga kisa kuachwa na Mpenzi, aagiza azikwe Siku ya Valentine na Mpenzi ndio asome Wosia wake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
MWALIMU wa shule ya sekondari kutoka kijiji cha Nthangathiri, Kaunti ya Embu, alijitia kitanzi ndani ya nyumba yake baada ya mpenzi wake wa pembeni kumtema.

Marehemu aliyetambulishwa na polisi kama Dennis Mwaniki Njeru, 32, almaarufu kama Mukono, alipatikana amelala kwenye kitanda chake na barua aliyoandika kando yake.

Kulingana na polisi, marehemu alikuwa anavuja povu kupitia pua lake huku kemikali inayoshukiwa kuwa dawa ya kuua wadudu ikipatikana humo vilevile.

“Ni mwalimu kutoka Mbeere Kaskazini lakini anafunza katika shule ya Sekondari iliyopo Kaunti ya Kirinyaga, alipatikana akiwa amekufa nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umeonyesha alijtoa uhai,” alisema.

Kwenye kijikaratasi hicho, mwendazake alisema alichukua uamuzi huo baada ya mpenziwe kumkataa.

“Naweza nikaonekana mjinga lakini nimefungua moyo wangu kuhusu kinachoniumiza kwa watu 17 lakini hakuna aliyezungumza nami, acha tukutane mbinguni. Nimemsihi mpenzi wangu lakini yote yameambulia patupu. Nawapenda nyote,” alisema kupitia barua hiyo.

Bw Njeru vilevile ameacha maagizo kuhusu jinsi anavyotaka kuzikwa.

Ameagiza afisa mkuu katika Bunge la Kaunti pamoja na diwani wa eneo hilo kuongoza mipango ya mazishi yake.

Aidha, alisema azikwe Sikukuu ya Wapendanao almaarufu kama Valentine ambapo mpenzi wake anapaswa kusoma wosia.
 
1.jpg
 
Hayo maneno katika barua yake kuna cha kujifunza. Mtu akikueleza shida yake mpe muda wa kumsikiliza, hata kama ni jambo lisilovutia kusikiliza.
Mwisho mpe moyo, hata kama unaona ni ujinga anaofanya.
Na mm nitajinyonga Juu yako Nifaa
Umetoa ushauri mzuri sana.Ni bora ukampa mda na kama humpendi unamtafutia sababu ambayo ukimwacha hata umia.Kuna watu wameachwa kwa kashfa bila hata sababu ama mtu unamuona anamtu mwingine yaan unapigwa chini ujijue mwenyewe.
 
MWALIMU wa shule ya sekondari kutoka kijiji cha Nthangathiri, Kaunti ya Embu, alijitia kitanzi ndani ya nyumba yake baada ya mpenzi wake wa pembeni kumtema.

Marehemu aliyetambulishwa na polisi kama Dennis Mwaniki Njeru, 32, almaarufu kama Mukono, alipatikana amelala kwenye kitanda chake na barua aliyoandika kando yake.

Kulingana na polisi, marehemu alikuwa anavuja povu kupitia pua lake huku kemikali inayoshukiwa kuwa dawa ya kuua wadudu ikipatikana humo vilevile.

“Ni mwalimu kutoka Mbeere Kaskazini lakini anafunza katika shule ya Sekondari iliyopo Kaunti ya Kirinyaga, alipatikana akiwa amekufa nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umeonyesha alijtoa uhai,” alisema.

Kwenye kijikaratasi hicho, mwendazake alisema alichukua uamuzi huo baada ya mpenziwe kumkataa.

“Naweza nikaonekana mjinga lakini nimefungua moyo wangu kuhusu kinachoniumiza kwa watu 17 lakini hakuna aliyezungumza nami, acha tukutane mbinguni. Nimemsihi mpenzi wangu lakini yote yameambulia patupu. Nawapenda nyote,” alisema kupitia barua hiyo.

Bw Njeru vilevile ameacha maagizo kuhusu jinsi anavyotaka kuzikwa.

Ameagiza afisa mkuu katika Bunge la Kaunti pamoja na diwani wa eneo hilo kuongoza mipango ya mazishi yake.

Aidha, alisema azikwe Sikukuu ya Wapendanao almaarufu kama Valentine ambapo mpenzi wake anapaswa kusoma wosia.
Maaskari na walimu ndio wanaongoza kujiua kwa visa vya mapenzi, kwanini?
 
Waongezeni majukumu hawa walimu wanamuda mwingi sana wa free hadi wanawaza mapenzi kupitiliza..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom