Picha: Bilioni 10 za Rais Magufuli kwa Hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) zakamilisha kazi

Baada ya mwaka mmoja ya majengo hayo kukaliwa na wanafunzi, hayatakuwa katika ubora unaoonekana kwenye hizo picha.

Uchafu utakuwa kila kona ya majengo, maji yanaweza kuwa hayatoki mabombani, na mambo mengine mengi yenye kutoa picha ni jinsi gani tusivyoweza kutunza cha kwetu.
 
Ukiwa chadema kwa miaka zaidi ya 20 mpaka sasa mmepanga Ufipa licha ukubwa wa ruzuku na mmerdihika bila kumuhoji mbowe Unadhani utaamini Magufuli anaweza kujenga hostels hizi kwa muda mfupi? Wakati mwingine itabidi tu tuwaeleweni mlivyo
Kuna watu kama hawatabadilika katika utawala wa Rais Magufuli basi mazingira yatawabadilisha kwa nguvu.

Hawaamini kama majengo yamejengwa kwa bajeti iliyotajwa na kukamilika kwa miezi minane.
 
Nguvu yao kwa sasa iko Dodoma kuhakikisha katiba ya chama haibadilishwi.
Watawezaaaa!
 
Unajua tatizo humu JF watu tunachangia kila mtu na Upande wake.... Hebu tuchangie kama wasomi JPM Anapiga kazi xana na ana uchungu ila na mapungufu yake yapo.... Hebu tupige taswira haya majengo yangejengwa na serikali ya Kikwete nahisi wangekuwa wanamalizia msingi saivi, na yangejengwa kwa gharama kubwa.... Na wapinzani wanayo mazuri lakini na mabaya yapo rukuki.. TuComment kwa facts kama wasomi tuachane na upepo wa kisiasa.
 
Title is misleading... Hizo hela ni za wanainchi na siyo magufuli.
Nampa hongera kwa kuhakikisha zimetumika vizuri.
 
Hapo ndio penye utata. Jengo hilo la ghorofa 4, yaani ukiweka na ground floor unakuwa na floors 5 tunaambiwa limekamilika kwa gharama ya shilingi milioni 500. Basi ujenzi ni mwepesi siku hizi...
Tukiwaambia mnaibiwa mnabisha.
 
wataalam gani mkuu wa kuweka mfuko mmoja 48000. wakati unauzwa 15,mpaka 16
Hakuna contractor au QS anayeweza kuweka bei ya cement mfuko shilingi 48,000 hizo ni nadharia ....unajua kwenye ujenzi kuna standard construction costs per m2 ......huwa zinarange humo humo.
 
Mkuu hatupingi kazi tuna hoji gharama kama ni kweli majengo yote hayo yametumia bl10. Kama unakumbuka wiki iliopita benki kuu walifungua ofisi Mtwara ya ghorofa tatu na gharama ilikuwa bl 38 sasa how come kijiji hicho kigharimu 10bl.
Haya ndiyo mambo yanatakiwa kujadiliwa Bungeni!!!
 
Engineer G Sam upo wapi ulete mrejesho,kuingia mitini kwa msomi kama wewe kunatia mashaka.Njoo ka B0Q uthibitishe hata kama ni sawa pesa iliotumika ni B10,itasaidia kujenga hoja kwenye sekta ya ujenzi
Huyo ni mpiga porojo tu.

Jaribu kufuatilia thread zake na kuzichunguza vizuri utagundua ni porojo tu za kisiasa ambazo zinawafaa wenye fikra duni.
 
Kuna watu kama hawatabadilika katika utawala wa Rais Magufuli basi mazingira yatawabadilisha kwa nguvu.

Hawaamini kama majengo yamejengwa kwa bajeti iliyotajwa na kukamilika kwa miezi minane.
Yule mhindi bilionea alitoa pesa zijengwe ofisi na chuo cha kuandaa makada na akaahidi kuwapa floor moja katika jengo lake. Hojini huko pesa zimeenda wapi? Chezea hao jamaaa weyeee
 
Back
Top Bottom