Picha: Bilioni 10 za Rais Magufuli kwa Hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) zakamilisha kazi

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Ujenzi wa majengo 20 yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya wanafunzi 3,840 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo kila jengo lina ghorofa tatu umekamilika baada ya kuchukua muda wa miezi minane.

Suala kubwa nililojifunza katika siasa za Tanzania ni kuwa na kiongozi shupavu anayesimamia kile anachokiamini na kukiamua bila kujali kelele za wanasiasa wanafiki na wale wasioamini.

Ikumbukwe kuwa kuna wakandarasi walitaka kulipwa bilioni 100 katika mradi huu.

Kuna wengine walileta thread hapa na kuwaaminisha baadhi ya wana JF kuwa wataleta gharama kamili ya ujenzi lakini mpaka sasa ''wameingia mitini'' kwa sababu uwongo wao ulitumia lifti kuwafikia walengwa lakini kwa sasa ukweli unafika kwa kutumia ngazi.

Kama ukipenda kuwasoma wanafiki na wasioamini pitia/gonga LINK==> Ujenzi wa flats 20 za ghorofa nne kwa Tsh bilioni 10 ni uwongo

Picha hizi pia zinatoa fundisho kwa wasioamini ambao pia wameainishwa kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu ndani ya Quran na Biblia.

Kwa wale wanaojua Quran wanaweza kuelewa maana ya maneno yangu kupitia verse 44 ya Surah Fussilat (41).

Kwa wale wanaojua Biblia wanaweza kuelewa maana ya hoja yangu kupitia Yohana 20:24.

Kuna msemo usemao, Kama hujui kusoma, hata picha huwezi kutazama?

Focus and perseverance is what separates winners from losers.

Rais Magufuli is always the winner.

C6Y4mVSWAAAmRiR.jpg

C6Zv2e6WcAIwrby.jpg

C6Zv8BbXQAAryhq.jpg

C6Zv_w2WMAA8-fS.jpg

C6ZwBikWMAAhggo.jpg

C6Y4rXJWQAEoYRf.jpg
 
Mkuu hatupingi kazi tuna hoji gharama kama ni kweli majengo yote hayo yametumia bl10. Kama unakumbuka wiki iliopita benki kuu walifungua ofisi Mtwara ya ghorofa tatu na gharama ilikuwa bl 38 sasa how come kijiji hicho kigharimu 10bl.
 
Sasa wewe MsemaUongo ni ushahidi gani umeleta hapa kuonesha hayo majengo yamejengwa kwa bil 10. Wewe umetuwekea tu picha za majengo. Kwani wskosoaji walisems hayo majengo hayatakamilika? Ukosoaji ulijikita kwenye gharsma na ubora! Tudhbitishie basi kwamba hayo majengo yamejengwa kwa bil 10 tu! Kuhusu ubora ni suala la kusubiri time will tell! Kumbuka tuliambiwa pia hayo msjengo yana uwezo wa kubeba ghorofa nyingine mbili!
 
Fikra za kimaskini na za kwanini fulani afanikiwe ndio hizi.
Ujenzi wa majengo 20 yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya wanafunzi 3,840 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo kila jengo lina ghorofa nne umekamilika baada ya kuchukua muda wa miezi minane.

Suala kubwa nililojifunza katika siasa za Tanzania ni kuwa na kiongozi shupavu anayesimamia kile anachokiamini na kukiamua bila kujali kelele za wanasiasa wanafiki na wale wasioamini.

Kuna wengine walileta thread hapa na kuwaaminisha baadhi ya wana JF kuwa wataleta gharama kamili ya ujenzi lakini mpaka sasa wameingia mitini kwa sababu uwongo wao ulitumia lifti kuwafikia walengwa lakini kwa sasa ukweli unafika kwa kutumia ngazi.

Kama ukipenda kuwasoma wanafiki na wasioamini pitia/gonga LINK==> Ujenzi wa flats 20 za ghorofa nne kwa Tsh bilioni 10 ni uwongo

Picha hizi pia zinatoa fundisho kwa wasioamini ambao pia wameainishwa kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu ndani ya Quran na Biblia.

Kwa wale wanaojua Quran wanaweza kuelewa maana ya maneno yangu kupitia verse 44 ya Surah Fussilat (41).

Kwa wale wanaojua Biblia wanaweza kuelewa maana ya hoja yangu kupitia Yohana 20:24.

Kuna msemo usemao, Kama hujui kusoma, hata picha huwezi kutazama?

Focus and perseverance is what separates winners from losers.

C6Y4mVSWAAAmRiR.jpg

C6Zv2e6WcAIwrby.jpg

C6Zv8BbXQAAryhq.jpg

C6Zv_w2WMAA8-fS.jpg

C6ZwBikWMAAhggo.jpg

C6Y4rXJWQAEoYRf.jpg
Hongera JPM, kumbe milioni 500 inaweza kujenga ghorofa la maana
 
Back
Top Bottom