Phillipe Coutinho awabwaga Neymar, Marcelo, Douglas Costa, Firmino kwa kushinda tuzo hii

xungura

JF-Expert Member
Jul 18, 2016
279
250
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Brazil , Philippe Coutinho amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Kibrazil ndani ya Bara la Ulaya kwa mwaka 2016.

Katika Kura hizo ambazo zimepigwa na mashabiki wa soka wa Kibrazil pamoja na wadau mbali mbali wa soka wa brazil wanaoishi bara la Ulaya Philippe Coutinho aliweza kupata asilimia 44% za kura zote ambazo zimepigwa .

Wachezaji wengine ambao walikuwa katika kinyang'anyiro hiko ni pamoja na Neymar Jr wa klabu ya Fc Barcelona ambaye ameshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 33% ya kura zote , Watatu ni Marcelo wa Klabu ya Real madrid Ambaye amepata asilimia 14% , Douglas Costa wa Bayern munich alipata asilimia 3% na Roberto Firmino wa Klabu ya Liverpool alifunga dimba katika Top-5 kwa kupata asilimia 2% ya kura zote .

Akiongea baada ya Kutangazwa kuwa mshindi , Phillippe Coutinho alisema kwamba

" Najisikia faraja kwa heshima hii , natumai ni mwanzo mzuri wa kuongeza kiwango changu zaidi ya hapa , Wote ni bora ila ni Jitihada zimenifanya niwe hapa "
YNWA.
 
PNC

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
7,934
2,000
Kiukweli amestaili binafs nampongeza sababu huyu ni mkweli na alishasema wachezaji wake bora ni MSN
 
xungura

JF-Expert Member
Jul 18, 2016
279
250
Namkubali maana ni mchezaji mwenye nidhamu na ana kujua kuuchezea mpira hasa magoli yake ya mbali.
 
Lizarazu

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
6,151
2,000
Mimi sio mliverpool lakin kwa huyu dogo hands down.

Dogo amekuwa na mwaka mzuri sana, nakumbuka alivyomsafirisha Peter cech pale Emirate kidogo amvunje bandama.

He's my favorite brazilian player right now.
 
Hansss

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,371
2,000
lini anarud rasmi dimban maana firminho km anapotea hivi bila cout
 
nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
3,957
2,000
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Brazil , Philippe Coutinho amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Kibrazil ndani ya Bara la Ulaya kwa mwaka 2016.

Katika Kura hizo ambazo zimepigwa na mashabiki wa soka wa Kibrazil pamoja na wadau mbali mbali wa soka wa brazil wanaoishi bara la Ulaya Philippe Coutinho aliweza kupata asilimia 44% za kura zote ambazo zimepigwa .

Wachezaji wengine ambao walikuwa katika kinyang'anyiro hiko ni pamoja na Neymar Jr wa klabu ya Fc Barcelona ambaye ameshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 33% ya kura zote , Watatu ni Marcelo wa Klabu ya Real madrid Ambaye amepata asilimia 14% , Douglas Costa wa Bayern munich alipata asilimia 3% na Roberto Firmino wa Klabu ya Liverpool alifunga dimba katika Top-5 kwa kupata asilimia 2% ya kura zote .

Akiongea baada ya Kutangazwa kuwa mshindi , Phillippe Coutinho alisema kwamba

" Najisikia faraja kwa heshima hii , natumai ni mwanzo mzuri wa kuongeza kiwango changu zaidi ya hapa , Wote ni bora ila ni Jitihada zimenifanya niwe hapa "
YNWA.
taarifa kama hizi bila link/source au picha yoyote ni sawa na tuzo hewa tuu!
 
nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
3,957
2,000
kwa lipi hasa?? au chenga??

hizi tuzo zingine ni kichefuchefu bhana!

hiyo perfomance yake imeisaidia nn liverfool??
 
jacjaz

JF-Expert Member
Sep 7, 2011
438
250
kwa lipi hasa?? au chenga??

hizi tuzo zingine ni kichefuchefu bhana!

hiyo perfomance yake imeisaidia nn liverfool??
Huo wivu kijana. Sionkila tuzo sina msaada kwenye timu. Watu wamepiga kura kwa mitazamo yao,kwa kuangalia wachezaji wa Brazil ulaya. Sasa mtu kupata kura nyingi kwako inakusumbua nin?? Kama vipi nasisi tuanzishe zetu za kupigia kura waTZ wanaocheza ulaya,mshindi lazma atapatikana tu.
 
Pung'o boy

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
686
500
kwa lipi hasa?? au chenga??

hizi tuzo zingine ni kichefuchefu bhana!

hiyo perfomance yake imeisaidia nn liverfool??
Endelea kula pop corn tu mambo ya mpira huyawezii, huoni msaada wa coutinho kwa Liverpool?? Alivyoumia liver akapoteza game 2 na moja akatoka draw kabla team haijakaa sawaa, baada ya kuondoka suarez coutinho ndio amekua messiah pale liver bila yeye team haipaform vizurii... Kwa sasa tunaweza sema coutinho ndio mchezaji bora Liverpool na ligi ya uingereza kwa ujumla
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom