Philip Mangula vs Dr. Willibrod Slaa

Nani mkali kati ya MANGULA na DR. SLAA?

  • MANGULA

    Votes: 7 5.3%
  • DR. SLAA

    Votes: 126 94.7%

  • Total voters
    133
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
msendekwa slaa kaijenga CDM peke yake?

Hapana, si peke yake. Ila mchango wake, tangu akiwa bungeni, kisha kukubali kugombea Urais na kutumikia chama kama Katibu mkuu(ambaye ndiye mtendaji mkuu wa chama) kumeijenga mno CDM, na bila shaka unajua alikuwa na mvuto sana kwa wapiga kura, hd kupata zile kura 2ml(excluding uchakachuzi). Na sasa zile kura ndo zinaendelea kugeuzwa kuwa wanachama. Ikumbukwe hakuna Mgombea wa chama pinzani aliyewahi pata kura 2ml na zaidi kabla ya Dr.
 
Unalinganisha Kilimanjaro na Kichuguu. Sijui kama Mangura anajua hata sura ya komputa
 
 

Kikwete hakushinda 80 % kwa ajili ya Mangula .................... that time Kikwete alikuwa anapendwa kila mahali na kila mtu probably except me. Kuna threads humu ndani ambazo zilidai kuwa jamaa alitaka JK atoshwe ili ajipigie pass mwenyewe lakini haikuwezekana. Hata Mkapa alishindwa kumtosa JK hivyo ikabidi ajiunge naye na kuunza kumpigia kampeni.

Kumlinganisha Mangula na Slaa ni sawa na kulinganisha maji na mafuta!!!
 

Kikwete alikuwa na kadi ya CUF wangemtosa CUF ingechukua nchi kupitia umaarufu wa Kikwete!
 
Kikwete alikuwa na kadi ya CUF wangemtosa CUF ingechukua nchi kupitia umaarufu wa Kikwete!

Nape analijua hilo??? Maana amemkomalia Slaa wakati hata yeye ameshindwa kuthibitisha kama hana kadi ya CCJ halafu anadai watu wadhibitishe!! Inaelekea CCM kuwa ana kadi za upinzani ni kitu cha kawaida sana!! ....................Wanajuana kwa vilemba!!!
 
mazingira magumu kudidimiza akina ZZK??? MANGULA kaongoza akili za watu 6,000,000 vp huyo babu yenu??

Kijana tumia akili yako sawa sawa.Ushabiki mwingine bila kufikiri unadidimiza hadi uwezo wako wakuchambua mambo.Kama umepitia shule hata kama ni darasa la saba huwezi kuja na pumba kama hii.

 
japo post si yangu naomba nikwambie tuache ushabiki wa kiroho huwezi kumlinganisha mangula na slaa kwanza mangula aliongoza CCM kama taasisi na wanachama wengi huwez kumlinganisha na slaa anaeongoza kampuni jadili kisomi mkuu

Mkuu mtz one,

Nilikuwa nataka nikujibu, lakini nilivyoona tarehe uliyongia hapa JF - hususan nikikumbuka kuwa wakati huo nilikuwa Kijijini nacheua biriani na pombe ya Komoni, nikaamua kukukalia Kimya.

Hivi umekaribishwa kweli humu?

Cc- Molemo
 
Last edited by a moderator:



Bora ungesema Pr. Lipumba v/c Dr. Slaa kungekuwa na uwiano kidogo. Hizo kura 5/115 kwenye pool ni Ritz, Faiza, Pasco, Shonza, Juliana na Prezoo..
 
Mangula vs Mh Dr W.P Slaa? mmekosa vya kutuletea hapa?
Ungeuliza nani mkali kati ya Mangula vs Mulugo? Ningejibu
 
mangula nafikiri ni zaidi coz ameongoza CCM taifa zima na kama tujuavyo CCM na CDM ni mlima na kichuguu huwezi kusema slaa anamzidi mangula vinginevyo ni utashi wako binafsi

Hivi nataka kujuzwa juu ya hili. " aliyepata div 1.7 pale st. Francis au Feza na Yule aliyepata div 2 Shule za kata zenye walimu watatu na vyumba viwili za madarasa YUPI MWENYE IQ KUBWA?
 
Dr. Slaa ukimlinganisha na Mangula ni sawa na kuilinganisha tembo na sisimizi
 
Huyu miwngine ndiye architecture wa kuiba kura Zimbwabwe na hata kipindi fulani cha uchaguzi katika nchi kadhaaa hivyo Tazama hata vimemo vingi sana EPA viliandikwa na yeye hivyo ni mtu wa ajabu kidogo hana lolote lile
 

Rob

Umeleta uzi ambao ni skeleton and to that effect umeacha wachangiaji wajaribu ku-stuff it with flesh no matter it's fresh or stinking or filth. Ndio maana hapa baada ya kujadili issues watu wanachangia matusi. Ulipashwa utupatie vigezo vya kuwapima na hapo tupate kupiga kura. Magula kama katibu mkuu wa CCM wa wakati ule na Slaa katibu mkuu wa sasa these are two characters diametrically opposed. CCM kimekuwa ni chama dola na baadae chama kinachosaidiwa na dola kwa namna yoyote ile iwe kwa lazima au kwa wahusika wanaotegeneza dola kujikomba. Magula amekuwa katibu mkuu kwa wakati ule na kiongoza wananachama ambao wachangiaji wanasema 6million. Great, let us put ourselves in their shoes. Lakini wakumbuke kuwa sio Mangula aliyewatafuta weingi waliingia kwa mapenzi yao na wengine ikiwa ni kwa ajali ya kihistoria ili wapate kusoma au wapate passports.

Dr.Slaa anaongoza chama ambacho kimestruggle desperately from the scratch. Unapata wanachama wengine si kwa mapenzi ya dhati ya hitikadi yako bali kwa sababu wameshindwa kupata upenyo CCM. Wanakuja CDM kwa sababu lazima wawe na chama tena kinachokua ili wapate kwenda point B. Wengine ni mamluki. Panahitajika mtu wa kuweza kuwatambua hawa wote na kuweza kutoa uongozi na sanctions. Je, Dr.Slaa ameweza kuwatambua hawa na kuweza kutoa reliable leadership and sanctions when needed. Hapa huwezi kumlinganisha na Mangula. Sote ni mashuhuda na tunaona anavyojitahidi bila kuchoka.

CDM ina hitikadi yake na haioni aibu kujitambulisha kwayo. CCM hatujui mpaka kesho wana hitikadi ipi. Wanasema ujamaa na kujitegemea. Hivi ni kweli? Mwasisi wake Mwalimu Nyerere alisema walipokutana Zanzibar wakalivunja Azimio la Arusha ahalafu wakarudi kimyakimya. Waliua blue print halafu wakaanza kuendesha mambo kivyao vyao na wala sio kibepari maana kusema kibepari ni kuwatukana wanaofuata siasa ya kibepari ambayo ni sociala market economy ambapo soko linawajibika kwa watu. Sisi hapa tunawajibika kwa soko ambapo kuna wanaogelea kwenye utajiri wakati kuna wengi jirani ambao wako katika umasikini wa kupindukia.

Rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma imekuwa ni kama sera ndani ya CCM. Rejea EPA na jinsi pesa hiyo ilivyotumika katika uchaguzi wa 2005. Ni kipindi ambacho CCM ilishindwa kuisimamia serikali na matokeo yake viongozi wa serikali wakashiriki uporaji rejea ubinafsishaji wa mashirika ya umma usiokuwa na maslahi, mikataba laghai ya madini na viongozi kufanya biashara wakiwa madarakani (Kiwira na Mkapa).

Nisaidie kwa kusema labda tuweke vigezo tuwapime kwa yafuatayo:-

1.kusimamia sera
2.kubuni na kutekeleza mikakati endelevu
3.kuchukia, kukemea na kuzuia rushwa na mianya ya rushwa
3.kutekeleza kwa vitendo hitikadi ya chama
4.kufanya maamuzi kwa mujibu wa katiba ya chama
5. kuzuia na kukemea aina yoyote yamakundi

Nawasilisha
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…