Nionavyo mimi, kukosekan akwa usawa katika jamii zetu kwa watu wenye uhitaji inatokana na hizi kampeni za kuwaweka kuwa ni watu wenye kuhitaji msaada kila siku. Nitajaribu kupambanua kwa hoja zifuatazo;
1. Kampeni ya haki sawa, hii lengo lake ni kuhakikisha kuna usawa kati ya mwanamke na mwanume, shida ni kuwa hao wanaopigania haki za mwanamke ndio wanaomjengea mwanamke imani kuwa hajiwezi na ni tegemezi, kivipi? kumekuwa na asasi zisizo za kiserikali ambazo kazi yake ni kutoa huduma fulani kwa wanawake, kama kuwapa mitaji ambayo ni maalumu kwa wanawake pekee, hii kwa upande wangu naona bado inachangia wanawake kubaki na utegemezi wa kuwa watasaidiwa wawapo na hali ngumu, hivyo kuwafanya wasijibidiishe katika kufikia lengo la haki sawa.Inawanya wanaendelea kuishi wakiamini wao ni kundi maalumu na sio sawa na mwanaume kama inavyonadi sera yao.
2. Siku za watu wenye ulemavu. Katika siku hizi ndio utaon aTaasisi fulani zinatoa vifaa kwa walemavu wenye uhitaji. Suala la kujiuliza ni kuwa idadi ya walemavu wanofikiwa katika siku hizi ni asilimia ngapi ya walemavu wote wenye uhitaji? Nionavyo imi hakuna haja ya kuwa na siku ya walemavu kwani ndivyo mUngu amewaumba, badala yake iwepo mingo endelevu ya kuwawezesha kwa mahitaji mbalimbali. Katika hizi siku najua kuna watu wasio na haya maarufu kama wapigaji nao hujinufaisha. Mngetangaza mpangokazi wa namna gani mtawafikia wenye uhitaji na kuwasaidia lakini kutenga siku na kuewka bajeti ambazo wakati mwingine zinaishia kwenye MATUMBO YA WASIO WALENGWA inakera kwa kweli.