Petition: Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litangaze rasmi Siku ya Taifa ya Wanawake wenye Ulemavu

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,174
4,062
Wanawake wenye ulemavu wanakumbana na changamoto mara mbili, kukabiliana na ulemavu wao na mitazamo ya kijamii kwenye jinsia.

Wanawake wana uwezekano mkubwa wa kuwa na ulemavu kuliko wanaume. Na wanawake wenye ulemavu wana uwezekano mkubwa wa kukumbana na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa kingono kuliko wasio na ulemavu.

Kwa hiyo, tunawaomba ndugu, jamaa na marafiki, popote mlipo kuungana mkono nasi kuliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutangaza rasmi Siku ya Taifa ya Wanawake wenye Ulemavu.

Uwepo wa siku hii utasaidia:

- Kuongeza ujuzi wa jamii kuhusu haki za watu wenye ulemavu.
- Kuwawezesha wasichana na wanawake wenye ulemavu kupaza sauti zao.
- Kusaidia serikali na wadau wengine kujua changamoto wanazo kabiliana nazo ili kuwawezesha. wanawake wenye ulemavu.

Ingia hapa kupiga kura

1580462933980.png
 
Sawa, wanawake wenye ulemavu wamekuwa wakiachwa mara nyingi kwenye shughuli za maendeleo, labda wakipewa hiyo siku yao maalum itasaidia kukumbusha mambo mengi ya msingi.
 
Tanzania Still tuna mambo mengi sana Complex ya Kufanya kuliko hizo sherehe
 
Ni wazo zuri. Nimeshindwa kuvote kwa sababu inataka niingize taarifa zangu binafsi, hivyo naunga mkono hoja kwa maneno.
Ni kweli kabisa kuhusu kuingiza taarifa binafsi za mtu kwa ajili ya hili zoezi la ku-vote haijakaa sawa. Suala hapa kinachotakiwa ni vote (kura) tu hayo mengine hayana msaada sana kwenye hili zoezi. Nashauri wahusika kama wapo serious na hili zoezi wafanye hayo marekebisho labda kama ni zoezi feki ili kujua real identity za watu humu ndani ya jukwaa. Na kama ni zoezi feki wategemee pia kupata data/info feki.
 
Sidhani kama kuwa na siku maalum kutaleta tija yoyote, itakua sherehe tu na kusahaulika the very next day. Cha msingi ni, watu wenye ulemavu wawezeshwe bila kubagua jinsia na kusaidiwa na serikali katika kila ngazi ya maisha yao tofuauti na sasa ambapo walemavu wanaachwa wapambane na watu wengine bila kuzingatia hali zao. Wapeme tuition, medical, transportation and housing assistance.
 
kwani hakuna wanaume walemavu? Sema siku ya walemavu Tanzania, regardless of their gender
 
Idea nzuri sana hii
Kuna namna ya kudeal na haya mambo .

Reaerch and evidence of various phenomena still show that the birth of baby girl in Tanzanian society remains a challenges ...however when a girls becomes disabled the barriers are further exacerbated in the patriarchal society.

..wengine hufichwa ndani kama wafungwa wa mauaji,wengine hutupwa na kuuwawa ,hubakwa na kadhalika.

Changamoto bado ni nyingi na still wanawake walemavu wanaona kuwa sio type ya generation hii..hivo hukata tamaa.

Serikali ingetekeleza sera ya mwaka 2004 ya kuwapa walemavu elimu bure kuanzia primary had chuo kikuu...kuwapatia bima ya afya ..nk.

Zenye kujenga madhira sawa ya kushiriki ktk shughuli mblmbl za kijamii,kisiasa na uchumi.
 
Nionavyo mimi, kukosekan akwa usawa katika jamii zetu kwa watu wenye uhitaji inatokana na hizi kampeni za kuwaweka kuwa ni watu wenye kuhitaji msaada kila siku. Nitajaribu kupambanua kwa hoja zifuatazo;

1. Kampeni ya haki sawa, hii lengo lake ni kuhakikisha kuna usawa kati ya mwanamke na mwanume, shida ni kuwa hao wanaopigania haki za mwanamke ndio wanaomjengea mwanamke imani kuwa hajiwezi na ni tegemezi, kivipi? kumekuwa na asasi zisizo za kiserikali ambazo kazi yake ni kutoa huduma fulani kwa wanawake, kama kuwapa mitaji ambayo ni maalumu kwa wanawake pekee, hii kwa upande wangu naona bado inachangia wanawake kubaki na utegemezi wa kuwa watasaidiwa wawapo na hali ngumu, hivyo kuwafanya wasijibidiishe katika kufikia lengo la haki sawa.Inawanya wanaendelea kuishi wakiamini wao ni kundi maalumu na sio sawa na mwanaume kama inavyonadi sera yao.

2. Siku za watu wenye ulemavu. Katika siku hizi ndio utaon aTaasisi fulani zinatoa vifaa kwa walemavu wenye uhitaji. Suala la kujiuliza ni kuwa idadi ya walemavu wanofikiwa katika siku hizi ni asilimia ngapi ya walemavu wote wenye uhitaji? Nionavyo imi hakuna haja ya kuwa na siku ya walemavu kwani ndivyo mUngu amewaumba, badala yake iwepo mingo endelevu ya kuwawezesha kwa mahitaji mbalimbali. Katika hizi siku najua kuna watu wasio na haya maarufu kama wapigaji nao hujinufaisha. Mngetangaza mpangokazi wa namna gani mtawafikia wenye uhitaji na kuwasaidia lakini kutenga siku na kuewka bajeti ambazo wakati mwingine zinaishia kwenye MATUMBO YA WASIO WALENGWA inakera kwa kweli.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom