Peter Msigwa: Maendeleo ya Kenya yanaonekana magumu

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
Jirani zetu Kenya ambao wamebadilisha vyama vya kuongoza serikali zaidi ya mara 2 wanaonekana kupiga hatua kubwa tu ya kimaendeleo.Bajeti ya Kenya iliyopitishwa inaonyesha kushusha ushuru na kodi kwenye bidhaa muhimu kwa ajili ya kuwawekea unafuu wa maisha wananchi wake huku ikiwekeza sana kwenye ukusanyaji wa fedha za kigeni.

Pamoja na kwamba Tanzania tunawazidi rasilimali Kenya lakini bado nchi ya Kenya imetenga bajeti ya mwaka 2015/2016 kiasi cha trilioni 47 kwa ajili ya maendeleo ya Elimu,Barabara,Kilimo,Afya n.k, huku ikiwa ina idadi ya watu milioni 38.Wakati huo huo,Tanzania imetenga bajeti ya mwaka 2015/2016 kiasi cha trilioni 22.5 kwa ajili ya uchaguzi mkuu na maendeleo huku idadi ya watanzania ikionyesha kuwa inakaribia milioni 50.

Watia nia wa Urais ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi October ambao wengi wao ni mawaziri na wengine walijiuzuru kwa kashfa, wanasema watainua uchumi wa taifa wakati huo wameshindwa kuinua uchumi wa Taifa hili la Tanzania wakiwa kama mawaziri na watendaji wakuu wa serikali ya CCM.Maendeleo ya Taifa hili hayawezi kuja kwa watu wa chama cha siasa kile kile,watu wale wale,wenye akili zile zile na wenye kufanya kazi kwa mazoea yale yale chini ya mfumo ule ule.

Hakuna mtanzania mwenye hisa ndani ya CCM na kuna haja kubwa tu ya kufanya mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Ni aibu kwa taifa lililojitawala kwa zaidi ya miaka 50 hadi toilet paper inatoka China huku vijana tukijibizana kwa majina ya timu Membe,mara team Lowassa,team Wasira n.k wakati huo hakuna hata kitu kilichotengenezwa Tanzania ambacho tunaweza kujivunia kuanzia mavazi yetu chini mpaka juu.Hivi utapaje ajira wakati hata nguo za ndani tu tunazovaa zinatengenezwa

China huku tukiwapigia chapuo watia nia wa CCM waliokaa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 na kuuwa viwanda vyote?
**Mabadiliko huanza na mimi na wewe,muda wa mabadiliko ni mwaka huu usisubiri mwaka 2020**
 
Mungu aturehemu tumekuwa taifa lenye watu wasiokuwa wabunifu na wenye kutokubali kubadilika.Haingii akilini kushabikia mtuhumiwa wa ufisadi na walioshindwa kutetea maliasili za taifa letu .Mungu atukumbuke watu wake
 
pm wa el ni chenge
waziri wa pesa rostam

that is cheap politics,both of them hakuna mwenye mpango wa kugombea ubunge mbona mnawashwa?si mtulie dawa iingie vizuri?mkisikia jina lowasa basi mnakuwa machizi,mbona ndo movie imeanza nyie subirini ni kesho kutwa tu muanze kuongea vizuri
 
Umesema kweli kabisa msigwa, swali kama sio ccm nani mwingine?
Mmeshindwa kujenga vyama vyenu vikawa vyama vya kitaifa kimuonekano nani atawaamini?
Yanayofanyika ccm mengi mno kwenu mnayafanya mnadhani wananchi hatuoni?
Ubaguzi, ukanda, udini, uchu wa madaraka kwenye vyama vyenu ndio usiseme,
Ndio maana wananchi wanaona bora uendelee kubaki na kichaa uliyemzoea, CCM kuliko kuleta kichaa mpya, UPINZANI
 
Yani huyu mchungaji yani Mungu ametupa kweli kweli yani Akili Kubwa ya Upinzani ndio mwongozo wa Akili ndogo ya maccm. Wana mbeya mpeni kura tena, sio mnampa sijui mbege sijui mwakamadebe madebe
 
Tatizo la Tanzania tunawapa uongozi watu kwa kigezo cha uzoefu badala ya utendaji!

Nakubaliana na wewe. Yatupaswa tuangalie hili kwanza lakini uadilifu kabla.

Lakini tusisahau, mtu kuwa CCM haimaanishi kuwa ni mtu mbaya,asiyefaa, na pia mtu kuwa Chadema haimaanishi kuwa ni mtu safi, anayefaa.hapana!! watu wazuri wapo vyama vyote na watu wabaya pia wapo vyama vyote.Tusijifunge kwenye vyama vyetu kuchagua kiongozi bora.Tuwaangalie wote, tuwapime wote,kisha tuchague aliye bora zaidi miongoni mwao.
 
Tutavuna tutakachopanda. Mtoa mada hongera sana! Ni ukweli usiofichika hii nchi sasa hivi inaongozwa kimazoea. Tunataka mapinduzi katika elimu na viwanda. Rais ajaye apige marufuku bidhaa zinazotengenezwa nje ambaz tuna uwezo wa kuzitengeneza hapa nchini.
 
tanzania haina ubavu wa kunusa hata nusu ya kenya kiuchumi,nyie jifananisheni na rwanda
 
Nadhani tukitafakari kwa undani hii kauli inavigusa hata vyama vyetu vya upinzani..!!Kama tangia mfumo wa vyama vingi wagombea ni walewale,hawataki ku raise watu wengi au damu changa kuleta challenge katika system,wengine uchaguzi ulio pita hawakushinda lakini wanataka round nyingine badala ya kupisha waje wengine kushika nafasi zao baada ya wao kufail...Hata hao tukiwapa nchi still mambo yatakuwa yaleyale sababu hata wao hawana muono mpya .
kama huwezi kujifunza kupitia weakness za unaemuona adui kwako ,kamwe huwezi kumshinda wala kuwa na ubavu wakupambana nae katika uwanja wa vita
 
tanzania haina ubavu wa kunusa hata nusu ya kenya kiuchumi,nyie jifananisheni na rwanda

Tanzania inao ubavu japo Kenya imetutangulia katika baadhi ya mambo, hamjatuacha katika hatua nyingi kiasi cha kutamba na hayo maneno yako..we all the same with different image on a certain angle
 
Ukiongelea rasilimaliwatu Tanzania walau 50 bora hautatenda haki kama ukimuacha nje Mh. Msigwa. Ni mtu mwenye upeo na anaamini anachokisema na kukitenda, ndio maana hata pale anapokosea hang'ang'anii propaganda bali anakubali kushindwa kiungwana. Naweza kuwashangaa watu wa Iringa mjini endapo atagombea ubunge kwa mara nyingine na wakashidwa kumsaidia kulinda kura. Pia naweza kuwashangaa CDM endapo hawatampitisha kugombea jimbo lake pale atakapoomba hiyo nafasi!
 
Kamanda kampeni hazijaanza subiri kidogo basi
 
Tanzania inao ubavu japo Kenya imetutangulia katika baadhi ya mambo, hamjatuacha katika hatua nyingi kiasi cha kutamba na hayo maneno yako..we all the same with different image on a certain angle

bajet yenu ndogo,watu wengi, bajeti ya kenya ni kubwa watu wachache, tanzania maneno mengi vitendo hakuna. eti tangu 2009 mliahidiwa kujengewa flyover kupunguza jam haya ziko wapi ? nairobi tumemaliza hiyo mambo kitambo sasa tunafocus train za under ground. dar es salaam haiifikii hata kisumu sembuse nairobi,wenzenu kisumu kuna fly over tano,nyie bakini na ahadi zenu kama vichaa. mi mtz naish hapa kenya
 
Jirani zetu Kenya ambao wamebadilisha vyama vya kuongoza serikali zaidi ya mara 2 wanaonekana kupiga hatua kubwa tu ya kimaendeleo.Bajeti ya Kenya iliyopitishwa inaonyesha kushusha ushuru na kodi kwenye bidhaa muhimu kwa ajili ya kuwawekea unafuu wa maisha wananchi wake huku ikiwekeza sana kwenye ukusanyaji wa fedha za kigeni.

Pamoja na kwamba Tanzania tunawazidi rasilimali Kenya lakini bado nchi ya Kenya imetenga bajeti ya mwaka 2015/2016 kiasi cha trilioni 47 kwa ajili ya maendeleo ya Elimu,Barabara,Kilimo,Afya n.k, huku ikiwa ina idadi ya watu milioni 38.Wakati huo huo,Tanzania imetenga bajeti ya mwaka 2015/2016 kiasi cha trilioni 22.5 kwa ajili ya uchaguzi mkuu na maendeleo huku idadi ya watanzania ikionyesha kuwa inakaribia milioni 50.

Watia nia wa Urais ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi October ambao wengi wao ni mawaziri na wengine walijiuzuru kwa kashfa, wanasema watainua uchumi wa taifa wakati huo wameshindwa kuinua uchumi wa Taifa hili la Tanzania wakiwa kama mawaziri na watendaji wakuu wa serikali ya CCM.Maendeleo ya Taifa hili hayawezi kuja kwa watu wa chama cha siasa kile kile,watu wale wale,wenye akili zile zile na wenye kufanya kazi kwa mazoea yale yale chini ya mfumo ule ule.

Hakuna mtanzania mwenye hisa ndani ya CCM na kuna haja kubwa tu ya kufanya mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Ni aibu kwa taifa lililojitawala kwa zaidi ya miaka 50 hadi toilet paper inatoka China huku vijana tukijibizana kwa majina ya timu Membe,mara team Lowassa,team Wasira n.k wakati huo hakuna hata kitu kilichotengenezwa Tanzania ambacho tunaweza kujivunia kuanzia mavazi yetu chini mpaka juu.Hivi utapaje ajira wakati hata nguo za ndani tu tunazovaa zinatengenezwa

China huku tukiwapigia chapuo watia nia wa CCM waliokaa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 na kuuwa viwanda vyote?
**Mabadiliko huanza na mimi na wewe,muda wa mabadiliko ni mwaka huu usisubiri mwaka 2020**
PISTO LERO
Haika huu ni bonge la ujumbe!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom