GE2025 Peter Msigwa akiomba kura kwa wajumbe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Simon Msigwa, ameomba kura za maoni kutoka kwa wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu.

Mchungaji Msigwa, ambaye kwa sasa ni mwanachama halali wa CCM, amesema licha ya kuwa upande wa upinzani kwa muda mrefu, alifanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wa Iringa Mjini.

Hata hivyo, alikiri kuwa aliwahi kukutana na changamoto nyingi kutokana na mazingira ya kisiasa ya wakati huo.

“Japo nilikuwa kama mtoto wa kambo, niliwatumikia kwa moyo mmoja na kuwaletea maendeleo. Nikiwa upande wa upinzani nilipambana kuhakikisha wananchi wanapata huduma.

Sasa nikiwa ndani ya CCM, naamini nitafanya zaidi kwa kushirikiana moja kwa moja na Serikali,” alisema Msigwa mbele ya wajumbe.

Mbali na Msigwa, wagombea wengine wanaowania tiketi ya CCM kwa nafasi ya ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini ni: Fadhili Ngajilo , Wakili Moses Ambindwile , Islam Huwel
Nguvu Chengula

Wagombea wote wameendelea kujinadi mbele ya wajumbe wa kata mbalimbali ndani ya jimbo hilo, wakieleza dira, dhamira na mikakati yao ya kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wa Iringa Mjini endapo watapewa nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Source Millard Ayo
 
Msigwa apishe wengine zama zake za kuwa mbunge zimepita, wajumbe wachague mwingine
 
Hivi pale bungeni kuna nini? Yaani mtu akishakuwa mbunge akilini mwake kunajengeka picha ya kwamba yeye ndio ana title deed ya kuwa muwakilishi Jimbo husika miaka na miaka. Msigwa aachie wengine nao nafasi hiyo maisha sio ubunge tu ajikite katika taaluma yake unless otherwise aseme yeye ni wale wachungaji wa mshahara.
 
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mchungaji Peter Simon Msigwa, ameomba kura za maoni kutoka kwa wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kupata ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu.

Mchungaji Msigwa, ambaye kwa sasa ni mwanachama halali wa CCM, amesema licha ya kuwa upande wa upinzani kwa muda mrefu, alifanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wa Iringa Mjini.

Hata hivyo, alikiri kuwa aliwahi kukutana na changamoto nyingi kutokana na mazingira ya kisiasa ya wakati huo.

“Japo nilikuwa kama mtoto wa kambo, niliwatumikia kwa moyo mmoja na kuwaletea maendeleo. Nikiwa upande wa upinzani nilipambana kuhakikisha wananchi wanapata huduma.

Sasa nikiwa ndani ya CCM, naamini nitafanya zaidi kwa kushirikiana moja kwa moja na Serikali,” alisema Msigwa mbele ya wajumbe.

Mbali na Msigwa, wagombea wengine wanaowania tiketi ya CCM kwa nafasi ya ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini ni: Fadhili Ngajilo , Wakili Moses Ambindwile , Islam Huwel
Nguvu Chengula

Wagombea wote wameendelea kujinadi mbele ya wajumbe wa kata mbalimbali ndani ya jimbo hilo, wakieleza dira, dhamira na mikakati yao ya kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wa Iringa Mjini endapo watapewa nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi.

View attachment 3425574
Source Millard Ayo
nieleeshe, hawa si wamepenya juzi. Leo tena wako kweny kinyanganyilo? Baada ya hapa ni wapi tena?
 
Back
Top Bottom