Naomba kufahamishwa hizi pete zenye rangi mbalimbali, maumbo na ukubwa mbalimbali;
1. Zinafanya kazi gani?
2. Zinatolewa na mamlaka gani?
3. Zina faida na hasara gani?
Kwa muda mrefu nimeona viongozi wengi wakubwa mf mgombea mmoja wa uraisi mwaka uliopita alikuwa na pete yenye alama ya fuvu, na pia nimemuona kiongozi mmoja wa dini akihojiwa TBC1 akiwa na pete tatu zenye muonekano tofauti. Pia wafanyabiashara wakubwa hasa wa asili za Ki_Asia wakiwa na pete zenye maumbo, mnyumbuliko na rangi tofauti.
Kama zinafaida kwa nini wasitufunze na sie waumini wao kuneemeka kupitia hayo mapete? Je, hizo pete zinafaida kiroho/kiuchumi kwa wavaaji au ni urembo tu? Kama ni urembo tu, kwa nini wasivae pete za ndoa pekee?
Elimu haina mipaka