Pamoja na kilimo cha mananasi ni mfuga kuku mzuri sanaMkuu usisahau kuwa licha ya Mradi wa NCHI,Mkulu ni Mkulima stadi,ana shamba kubwa sana la MANANASI,ameifanya biashara hii kwa takriban miaka miwili unusu na anashauri kuwa ni biashara yenye kurudisha faida kwa haraka sana!!Isitoshe Wataalam wa kigeni (Iranians,Asians,Canadians)wapo kwa kutoa ushauri wa Bure.
**Mwikimbi wala usiwe na hofu,JK anajifadhili mwenyewe!Akidunduliza kwenye Mradi wa NCHI na wa MANANASI,mwakani lazima na kwa Bi.Salma kupendeze tu.
jana nilipita sehemu inayoitwa msoga kama km kumi ukitokea chalinze, kwenda arusha. kuna kitongaji kinaitwa vicoba hapa ndo nyumbani kwa jk. kuna ujenzi wa majengo kama 14 yanajengwa pale. wenyeji wanasema inajengwa ikulu pale.
.......................
je ni nani anafadhili ujenzi wa ikulu mpyaa vicoba? kama ni serikali iko kwenye bajeti?
isije ikawa yale mambo ya mobutu seseko kuhamishia ikulu kule gbaolite!
mwenye information naomba annielimishe
Wakuu tuleteeni picha ya lile kasri la BM kule LUSHOTO
,Mshahara wa Raisi ni kiasi gani ? Marupurupu ni kiasi gani ? Posho ya safari ni kiasi gani ? Baada ya kuunga unga jiulize anaweza kujenga kwa kutumia mihele hiyo aka vijisenti ?
Ikiwa mbunge tu anaweza kujenga magolofa vipi Raisi asiweze kwa kutumia ujumla wa mshahara wake wa Mwaka mmoja tu awapo madarakani ? WaTz tunajua Raisi wetu anapokea ngapi kwa kipindi cha Mwaka mmoja tu ?
Mwanakijiji;
Yale majumba unaweza kuyapata hata kwa kamera ya kawaida ingawa yataonekana kwa mbali.
PM;
Nadhani pale karibu na mwembe kuna ka bango......au ngoja wiki hii nikienda Mkata nitacheck tena, Ila sijawahi kusoma bango lile. au nimechanganya? majumba yenyewe yapo kushoto kama unaelekea Segera juu mlimani au?
FP
mmj KWA MAJUUMBA YA CHALINZE NI RAHISI SANA ITABIDI KAMA KUNA MWANDISHI UNAMFAHAMU...AENDE NA KAMERA KUBWA..INAYOWEZA KUVUTA KM 1 AU 2....MAANA MAJENGO YA GOROFA WANAYOONGELEA HAPA YANAONEKANA KWA MBALI KILIMANI UKIWA UNASHUKA NA BARABARA.....KM 10 BAADA YA KUTOKA CHALINZE UKIELEKEA SEGERA......UPANDE WA KUSHOTO....UKIFIKIA USAWA HUO KUNA MITI MIKUBWA NA ACCESS ROAD TU,,..HUTAONA CHOCHOTE ..HII INALAZIMU KUWA NA KAMERA PROFFESSION...USIMAME UVUTE UPIGE....SASA NADHANI HILI NDILO LINALETA UGUMU AU HAO WAANDISHI WANAOGOPA SIJUI..LAKINI...UNAWEZA KUMPATA MMOJA AAKAKUTUMIA PICHA...
KWA HII YA MIGOMBANI ....IMEZUNGUSHIWA UKUTA MKUBWA ..NA ULINZI UPO...NADHANI PIA HII INAKUWA NGUMU KWA MTU KWENDA TU KUJIPIGIA PICHA BILA KUJULIKANA MOTIVE ..NA INAJULIKANA WAZI KUWA HIZI PICHA ZINATAFUTWA.....
.WAZEE KWELI JF WATU MBINU ZIPO....PAMOJA NA KUIJUA GOOGLE EARTH..JANA WAKATI MJJ ANAULIZA NAMNA YA KUPATA PICHA ..SIO MIMI WALA YEYE ALIYEKUMBUKA GOOGLE EARTH..
SIKONGE AMEMALIZA WAZEE......KAMALIZA KABISA NJIA YA VUMBI UPANDE WA KUSHOTO ...KULIA kuna KWA barabara KUU KUNA MSIKITI MPYA.......UNAANGALIANA NA BARABARA YA VUMBI........
Kumbe Subash Patel aliepo kwenye orodha ya mafisadi papa ni rafiki wa siku nyingi wa JK kama ni kweli tumekwisha,malalamiko tutapeleka wapi wakati viongozi wanashirikiana na wahujumu wa mali za umma wana JF na Watanzania mpo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!..HAYO MAJENGO TANGU MSINGI ULIPOANZA MARA TU ALIPOINGIA MADARAKANI TULILETA TAARIFA HAPA.....PALE NI MAKAZI YAKE BINAFSI...PALE NDIPO ASILI YA UKOO WAO..BAGAMOYO WALIHAMIA TU...!!!....ANAJENGA MAKUMBA PALE ILI UKOO WAKE WOTE UHAMIE PALE.....SANJALI NA HUO UJENZI PIA MAKAZI YAKE YA MIGOMBANI STREET ALIBOMOA NA KUNUNUA KIWANJA CHA JIRANI YAKE PALE ..NATAYARI JUMBA KUBWA LIMESIMAMA PALE...
UJENZI HUU NI NJE YA UJENZI AMBAO HUFANYWA NA SERIKALI KAMA STAHILI YA RETIREMENT PACKAGE AMBAO KWA KAWAIDA KIKWETE ATASTAHILI TENA KUJENGEWA NYUMBA NA OFISI SEHEMU ATAKAYOCHAGUA PALE ATAKAPOKARIBIA KUSTAAFU..MWAKA 2010.......AU KAMA BAHATI NBAYA HATAWEZA KUENDELEA NA MADARAKA KWA SABABU YOYOTE.......
ZILE NYUMBA ZA NATIONAL HOUSING PALE ZIMEJENGWA KATIKA MKAKATI WA KUHAMISHIA MAKAO MAKUU YA MKOA WA PWANI PALE CHALINZE ....BAAADA YA KUONEKANA WAZI KUWA KIBAHA HAICHANGAMKI AU INAKARIBIA KUMEZWA NA DAR ES SALAAM......
..MOJA YA WASIMAMIZI WA MRADI WA MAJUMBA YA KIKWETE NI RAFIKI YAKE WA TANGU ZAMANI ..BAGAMOYO...BWANA SUBASH PATEL,,,,,ambaye pia humsimamia baadhi ya kazi zake nyingine.........hivi karibuni kwa heshima ya kikwete bwana subash alikarabati shule ya msingi aliyesoma kikwete.....hapo kijijini.....
UKWELI NDIO HUO!
Wakuu heshima kwenu!
Nimefurahia michango mingi hapa, wakati bado natafakari hoja, nadhani sasa twaweza jua kwanini VITA ILE YA KUSHUGHULIKIA UFISADI UVCCM ilikuwa ngumu kiasi kwamba mpaka leo ile,kamati mtakuñbuka ilipewa sikwiki mbili kama sikosei,mpaka leo mimepiata miezi hakuna matokeo
Mimi simtetei jamaa lakini hili la nyumba analiweka wazi sana... wakati alipopewa kiwanja kule Dodoma na wanakijiji sijui ni wa Chamwino au la... sikumbuki sana.
Alisema asanteni sana kwa kiwanja lakini jamani munikubalie kwamba nitakawia kukiendeleza kwa kuwa bado nina ujenzi kule kwangu.
Tena akawachekesha kwamba halimashauri imuhurumie wasije chukua kiwanja chao.
Endeleeni na source ya fedha ya ujenzi, lakini kwake hajaficha hili.
historia ya estim construction co ltd
1988-1990 kampuni ya konoike ilipewa kazi ya kujenga mradi wa maji uitwao the great nakuru water supply project nchini kenya. mtu aitwaye girr mhindi aliajiriwa kama karani wa kawaida.
1990s konoike walihamia dsm kwenye mradi wa dsm road improvement program(drimp), wahamia hapa na bwana girr, huyu baadaye akaungana na mtanzania mmoja mhandisi mahiri aitwae paul j.sirito, wakaanzisha estim construction.(estim=establish and maintain). huyu girr akaja kumwondoa yule mtanzania akabaki mwenyewe.
hivyoo girr mohamed ndo mkurugenzi wa estim, shubash patel hapana.
estim ni kampuni inayobebwa sana na konoike construction na ina uadilifu wa kijapan. bahati mbaya wanasiasa wanashinda pale kwenye ofisi zake za mikocheni wakilia njaa. wengine wakiomba awajengee nyumba haswaa mary nagu
Hizi ni siri za taifa na kupiga picha maeneo kama hayo ni kuhatarisha usalama wa taifa. So.. well mlitaka Rais aishi kwenye kijibanda?