Pesa za boom zina nini jamani?

Laki tano ya chuo hasa ya boom sio pesa kabisa ndani ya week 1 au 2 unakuwa mweupee peee, sijui zina nini zile pesa aisee.
Tumieni kodi zetu vizuri
Very soon itakua zamu yenu kuja kuteseka mpaka mkae kwenye ramani sio leo wala kesho.

Anza kuandaa talaka ya demu wako maana kilichoko mbele ni kigumu kuliko ulivyowahi kuvishuhudia maishani kwako.
 
wanachuo mnakula msosi hill park .. halafu hela za bumu zitoshe.. cafeteria zenu wanauza cheap mnaona hapafai
Hill park noma sana
Miaka hiyo nikiwa mshamba mshamba kutoka Maneromango nikaingia kunywa chai pale

Namaliza chai na andazi mbili nadaiwa karibu 3,000.

Ushamba mzigo sana kumbe kuna Yombo, Daruso, Cafe I na Cafe II na kule kwa walalahoi CoET
 
Day 1
Kubeti- 1000
Chai- 1500
launch - 2000
Maji- 1000
Dinar- 2500
Maji- 1000
Total 10000Tzs

10000*30 =300000TZS , Only Per month

Other expenses
- Copy
- kuhonga
- Nauli
- Michango

Kuwa na subra kijana ni kawaida sana
Mm nimekaa nje kuna baadhi ya gharama nimeziespace mfano:
Maji ya kunywa pamoja na lunch pamoja na breakfast vyote ni ghetto. Sasa mwingine nenda hill park au Coet upande Wa staff....
 
Dah umenikumbusha Enzi nasoma nillienda chuo na kama 1.5m Ya Matumizi kutoka home kufika huko nikapewa Boom Kubwa Lile La Mwanzo Wa Semista 710k Asee Nilikuwa Najiona Mtu Mzito Sana Nikavuta Mrembo White Mwaka Wa Tatu Gheto Flat Screen Na Sabufa Kubwa Baby Wangu Niamchukulia Iphone 5s enzi Izo Na Bata Mbil Tatu Kuja Kushituka Hivi Pesa Imeisha Yote Ahahaaahhaa
 
Boom in mipango tu!! Mfano mimi nipo mwaia Wa 2 ila kwenye akaunti yangu bado inasoma 460k. Na nimepanga nje sio kukaa hostel. Ukielewa maisha unayotaka kuishi mbona boom linabakiza chenji kabsa....
Kila siku movie mlimani city, shopping aura mall then lunch marry brown halafu unataka pesa za boom zisiwe na majini????
Hahaa ...kila week century cinema..daily samaki samaki ... halafu wana shangaa pesa kuwa na majini !!!!
 
Hahaa ...kila week century cinema..daily samaki samaki ... halafu wana shangaa pesa kuwa na majini !!!!
Eti unakutana na Jamaa anamtoa demu wake shopping anasema waende Mr. Price!!! Humo ndani pensi tu unaikuta inauzwa 30k bado hujanunua T-shirt nayo unaambiwa 55k. Hujauliza viatu hapo!!!!!
Lazma pesa ziwe na majini kwa maana jini Wa kwanza ni matumizi ya ovyo ovyo.
 
Back
Top Bottom