Pesa ya kijinga uliyowahi kuipiga.

Pesa ya kijinga uliyowahi kuipiga.

Lundavi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2016
Posts
328
Reaction score
326
Unajua kuna wakati mtu unaweza kuingiza pesa kijinga sana kwa mtu ambae hajui kitu fulani ambacho ni chepesi sana kwako. Kwa mfano kwangu mimi kipindi simu zinaingia kule kwetu kijijini nilikuwa nawapiga buku mbili mpaka tano kurekebisha simu ambayo imewekwa silent au vibration bila mwenye simu kujua. Je vipi upande wako, pesa gani ya kijinga umewahi kuipiga?
 
Nilinunuliwa na ccm kujiunga nao, nikakubali lakini kula yangu ilienda chadema, nilikula milioni mia mbili za bure
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] hongera kwa bingo ulilolipiga
 
Nilipiga mabilioni ya kikwete ya enzi zile, nikajenga nyumba mupyaaa maeneo ya kimara mwisho...
 
Yani kufunga madishi nimepiga hela ila sio kijinga kivile
 
Nakumbuka mwaka 2004 nmemaliza A-level kuna shangazi yangu alikuwa kanunua gari sasa siku moja betri ikawa imekufa akaniita kuniambia gari mbovu ivutwe iende gereji nikaipeleka mtaa wa pili baadae nkamwambia inahitajija laki 7 mzee nikanunua betri mpya nikarudisha gari kwake
 
Unajua kuna wakati mtu unaweza kuingiza pesa kijinga sana kwa mtu ambae hajui kitu fulani ambacho ni chepesi sana kwako. Kwa mfano kwangu mimi kipindi simu zinaingia kule kwetu kijijini nilikuwa nawapiga buku mbili mpaka tano kurekebisha simu ambayo imewekwa silent au vibration bila mwenye simu kujua. Je vipi upande wako, pesa gani ya kijinga umewahi kuipiga?
Mkuu wizi huo.
 
Mtoa mada unaonekana usivo na huruma kwa wanakijiji wenzako. Mm mtaani ninapoishi naletewa smart phone zenye shida ya seting kwa software na narekebisha siwadai hata theluthi ya thumuni ya nyerere na nyengine zina shida yenye kusumbua haswa ila nikimaliza ni Ahsante shukran.

Hali hii imenifanya nionekane mkarimu kwa majirani kiasi mtu akienda shamba kwao akirudi hadi jogoo analetwa kama ahsante na nikipata hitilafu ya umeme jirani sijamwita anakuja na anarekebisha tatizo hadi electrical bulb na socket plug zinawekwa mwenyewe sipo.

Nnachojaribu kukufahamisha sio kila nafasi unayoiona inaruhusu kupata hela ni fursa kwako fikiria vizuri, kuna upande mwengine wa thamani kiuchumi unaitwa "non monetary value" ambao pia vijana haswa waungwana tunahitajika kufahamu, kutoa msaada ukapata ahsante na shukran ni bora zaidi ya elfu mbilimbili ama tano.

Mihela ya CCM ikitokea tuile.
 
2015 kuna mbunge mmoja wa jimbo x mkoa wa songwe kwa sasa ni rc alitupa mil.10 watu wawili ili tuzigawe kwa wanaccm wampigie kura za maoni tulikula 9.4 m, tuligaw laki sita tu tuliwanunulia ulanzi na kimpumu wazee
 
Very gud, hizi ndio hela za bure maana hazina hata shahidi ama mkataba wa kupeana.
 
Lundavi jifunze mwenzangu umeona kitulano alivyopiga hela za bure sio kuwaibia na kuwadhulumu wanakijiji wenzako kwa ukosefu wa kutokujua mambo ya kiteknolojia ya kisasa, watakapoelewa watakuona wewe ni waovyo sana
 
Ilikuwa zamani Mkuu, nilkuwa nabangaiza za matumizi shule.
 
Lundavi jifunze mwenzangu umeona kitulano alivyopiga hela za bure sio kuwaibia na kuwadhulumu wanakijiji wenzako kwa ukosefu wa kutokujua mambo ya kiteknolojia ya kisasa, watakapoelewa watakuona wewe ni waovyo sana
Sie tunakula za wanaccm wenzetu mazuzu,eti jitu tumelichagua 2010 tokea tulichague haliji jimboni inafika karibia na uchaguzi linaunda eti kamati ya ushindi eti nimetenga mil 150 za ushindi eti hakikisheni kura zote kwangu sie tuliovaa ngozi ya kondoo kumbe mbwa mwitu mimate mwaaah,Tunamshukuru Mungu tulizitafuna.Nasikia anakuja tena kugombea 2020 aje tu watu tumalizie nyumba zetu kupaua
 
Nilipiga pesa kwenye taasisi nyeti........ hii, sio upigaji, ila katika kupigiana mahesabu kwa kichwa nilimtajia bei ya ajabu kama mara mia zaidi.
Tulifanya kazi mchana ule na siku ya pili jamaa akaja kuchukua kazi yake, wakati anatoa ile hela hadi nilikuwa natetemeka ukizingatia ile hela ilikotoka!
 
2015 kuna mbunge mmoja wa jimbo x mkoa wa songwe kwa sasa ni rc alitupa mil.10 watu wawili ili tuzigawe kwa wanaccm wampigie kura za maoni tulikula 9.4 m, tuligaw laki sita tu tuliwanunulia ulanzi na kimpumu wazee
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Nzuri hiyo hizo pesa za CCM za kula tu ndo wanafanya vyuma vimekaza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom