Pesa ninazo nisaidie wazo

Hilo Ndo tatizo kubwa sana kwa sisi watanzania, Ila mimi sitaki kuamini kwamba ulikopa Benk make benki ni lazima uwe na Mpango Kazi au Bsiness planing na some time uwe na Biashara kabisa na uwe na kila kitu kinacho takiwa kwa ajili ya Biashara.

Na kama kweli umekopa bila kujua utafanya nini basi inakula kwako mkuu, kwa sababu kabla hujakopa ni lazima ujirizishe kwamba Project unayo enda kuifanya inalipa, na kumbuka biashara si lele mama kuna kuyumba hata ndani ya miaka 3,

So mkuu unahitaji ushauri wa hali ya juu kwa huo mtaji wako

Yote yanawezekana KOMANDOO, anaweza akawa sehemu ya familia za watu kama kina Mhando wa Tanesco anakuja na mtaji wa 10m baada ya miezi minne anapewa tenda ya 800 milion
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Moony, mimi nipo kwenye NGO na inashughulika na masuala ya vijana, Naomba uniunganishe na hao watu wa NGO wanaoshughulika na kilimo. Tunadhani kilimo kinaweza saidia vijana kwenye ajira. Tupo Dar

Mara Songea, mara Dar sasa nishike lipi? Anyway nenda wizara ya kilimo kitengo cha tafiti watakupa msaada
 
Mara Songea, mara Dar sasa nishike lipi? Anyway nenda wizara ya kilimo kitengo cha tafiti watakupa msaada
Moony aliyepo Songea ni mtoa hoja mwenye milion 80. Mimi ni mwanaJF mwingine mwenye interest na kilimo. Sorry for confusion. Regards, Mpitagwa
 
Ukiwa hapo songea Kaskazini mashariki kuna eneo moja lipo around 100 km from songea kuna ardhi yeneye rutuba haihitaji mbolea, malinyi ,mahenge, mbingu kule wanalima vyakula vyote. kachukue ekari 500 kwa elfu hamsini tu ukishindwa anzia wilayani, pimisha pata hati weka miundombini kama umwagiliaji then nenda TIB wakupe trekta. kuhusu usafirishaji wa mazao ongea na mbunge wako wachnge barabara au kanunue msitu wa mbao popote then pasua.
 
utakapo kuja dsm nitafute tuongee mbili, tatu ninazo fuatilia. Ila usije na hela kwa kuwa ni kwa sababu ya maongezi. Unaweza kupata maarifa. nitaku pm namba yangu
 
utakapo kuja dsm nitafute tuongee mbili, tatu ninazo fuatilia. Ila usije na hela kwa kuwa ni kwa sababu ya maongezi. Unaweza kupata maarifa. nitaku pm namba yangu

unaogopa hela! Ungemwambia aje nazo tu
 
Chukua milion 20. Nenda Kidabaga au Kilolo. Nunua eka zako 100 kwa sh milion 5. Unabaki na milion 15. Milion kumi nunua miti laki moja na upande. Milioni 5 fanya ndio cost za kupanda e.t.c.

After 3 years utaanza kulipwa hela ya Carbon Exchange i.e. hewa makaa. Haitapungua milion 5 kwa mwaka na itakua ikipanda kila mwaka. Kwa sasa mti mmoja wa miaka 10 unathamani si chini ya Tshs 150,000/= (iwe pine au cyprus). Hii ina maana kwa miti laki 1 una Tshs 15,000,000,000 hio baba ni billion 15.

Ile 60 inayobaki nunua fuso tandem, kachukua class c beba mizigo dar songea pole pole. (ila endesha mwenyewe) kama bado uko hai after 15 years nafkiri you might even be able to pay for a ticket to heaven!
 
Kwa kuwa pesa yako ni ya mkopo, unahitaji biashara yenye uhakika. Siijui Songea vizuri so nitakupa usahuri wa kinachoweza kufanyika katika jiji la Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Pwani, Mwanza na Arusha.

Ingia katika moja wapo ya hiyo miji, prefferbly Dar es Salaam. Chukua mil. 50, tafuta viwanja 10 vya sh. mil 5 katika maeneo yenye potential ya kukua. immediately baada ya kununua anza kutafuta mteja wa sh. mil 8 kwa kiwanja.

Kiwanja cha mil. 5 unaweza kukiuza kwa mil. 8 bila matizo katika mwaka huohuo. Kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu ununue ukifanikiwa kuuza hata kwa mil. 7 faida ni asilimia 40. hakikisha hauuzi kwa chini ya sh. mil 6.5 kwa sababu hutaweza kurudisha mkopo.

Kitu kikubwa hakikisha haununui kiwanja chenye mgogoro wa aina yoyote kwa kufanya utafiti wa kutosha. Vilevile kuwa mwaminifu kwa wateja wako. Baada ya muda utafamika kuwa ni genuine realtor. Utaletewa wateja wengi mpaka utakimbia!

Biashara nyingine yenye profit margin kubwa na quick break even point ni biashara ya spare za magari. Hata hivyo hii biashara inahitaji uwe na ujuzi wa vifaa husika. Unaweza kutafuta mtu mwenye ujuzi wa ufundi, lakini startup bussiness inayotegemea expertise ya mtu mwingine ina nafasi kubwa ya kufail kuliko ile ambayo wewe mwenye unaweka passion in it...
 
Nina tsh 80m, niko Songea. Nianzishe mradi(miradi) gani ili niuage umasikini? Nisameheni kwa kukopa kabla ya kuwa na wazo kwanza. Ninatakiwa niwe nimezirudisha benki baada ya miaka 15 kuanzia sasa na 21%. wazo, tafadhali.

Zitumie tu kwa kuwa hao benki wazembe sana. Wala hawatakudai na wakikudai hawana grounds pia. Unawezaje kumkopesha mtu bila kujua anaenda kuzifanyia nini hizo hela?
 
Ile 60 inayobaki nunua fuso tandem, kachukua class c beba mizigo dar songea pole pole. (ila endesha mwenyewe) kama bado uko hai after 15 years nafkiri you might even be able to pay for a ticket to heaven!

Kwa kuendesha lorry? Na wale ''kwa sambi sako''!
 
Tafuta sehemu nzuri, ukipata jirani na stendi au eneo lenye watu wengi itakuwa vizuri, jenga gest house nzuri iwe na vyumba angalau siyo chini ya 15, weka na pub nzuri ya kisasa. Hakikisha unasimamia mwenyewe ili kila shilingi inayoingia uione, nakuhakikishia huo mkopo utaulipa vizuri kabisa tena kwa chini ya hiyo miaka 15.
Asikudanye mtu 80m ni hela ndefu amabyo ukiitumia vizuri hautarufi kwenye shida tena.
 
Sijamuona tena mwenye thread,ukute keshapata ticket to heaven already,ninyi mwabaki kuchangia tu mwenzenu keshasepa!
 
Back
Top Bottom