Pepo la ngono lina jinsia mbili

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
Achana na jini mahaba nazungumzia pepo...jini mahaba hutulizana sehemu moja na kwa sehemu kubwa jinsia yake ni kiumeni...kamwe huwezi kukuta jini mahaba lina pepo la ngono...

Jini mahaba linachukia uchafu, linachukia jhanaba, linapenda sana usafi, halipendi kuchanganya ama kuchangia penzi na mtu...Hivyo basi jini mahaba si pepo la ngono na kamwe viwili hivi haviwezi kuchangamana

Jini mahaba kiasili humuingia mtu mwanamke kwa utashi na uchaguzi binafsi ,kwa hisia za mapenzi na hamu ya ngono...lina wivu uliopitiliza..na ni binafsi sana....Ni wachache mno hurogewa jini mahaba... Na hili roho likimuingia mtu ni ngumu mno kumtoka..si rahisi hata kidogo kupata tiba ya kibinadamu ya kuweza kumtoa jini mahaba mwilini mwa mtu...

Pepo la ngono sasa....Hili ni habari nyingine kabisa, halichagui halibagui...hili ni chubwichubwi tuu popote kambi....ni mojawapo ya maroho machafu mabaya...hili haliangalii uso hata kama ni ndugu wa damu litatembea naye Miele kwa mbele....halijali sana yatokanayo!

Namna ya kuingiwa na pepo la ngono ziko mbili
Moja ni kutupiwa na mtu uliyemzingua kwenye mahusiano ama kulaaniwa ngono na mzazi au ndugu wa karibu sana kutokana na jambo baya sana ulilofanya kwenye familia....Maranyingi ikiwa ni kubaka ama kughilibu kingono

Pili ni kutokana na kuwa kiruka njia macho juu au chovya chovya nyingi...mapepo yanatembea na watu ...I mean watu wana mapepo mbalimbali ndani yao, sasa ukiwa mhangaikaji sana unavutia hayo madude kwa namna ya pekee kabisa.... kwani hujawahi kusikia mtu anaitwa fulani majanaba? Kitonga? Maharagwe ya Mbeya? Nknk

Mapepo ya ngono ni hatari sana kwakuwa kadiri unavyofanya ama kufanywa ndio kadiri hamu inavyozidi...yaani unajikuta unataka zaidi na zaidi....Na sababu ni moja tuu, pepo la ngono chakula chake ni manii...

Pepo la ngono lina jinsia mbili halibagui
Pepo la ngono halibagui dini,halibagui imani halibagui kabila, cheo umaarufu wala umri..... usishangae unapomkuta mtoto wa miaka 12 tayari chupi iko mkononi...hilo ni pepo

Pepo la ngono ni tofauti kabisa na jini mahaba kwenye kuweka makazi mahali...wakati jini mahaba likikomaa na kiwanja kimoja pepo la ngono lina tabia ya kukinai na kuondoka, ndio maana kuna watu unaona leo hii wametulia tuli kwenye mahusiano yao hawahangaiki tena!
 
Back
Top Bottom