Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,504
- 28,691
Kwasasa mpira umebadilika sana tofauti na enzi za kina Ferguson, Arsene Wenger n.k miaka ya 2000s.
Moja ya watu walioleta mapinduzi ya soka ni Pep Guardiolaz, huyu ana wanafunzi wake wengi sana aliokaa nao na wanaoiga uchezaji wake, kina Xavi Hernandez, Mikel Arteta, Erik Ten hag, n.k
Moja ya mapinduzi aliyoleta ni progressive football kuanzia kwa GK, Overload au Outnumbered kila eneo
Leo nitazungumzia Overload, hakuna kitu nakipenda ninapoangalia mpira na kufurahia ninapoona OVERLOAD, yaani hapa kila eneo unakuta umezidiwa, hiiinakuwaje? Fatana nami uone.
Timu nyingi huwa tunaona zinaingia na mifumo kama 4-3-3,4-4-2,4-2-3-1,3-4-3, n.k.
Hii kwa kawaida ni mifumo inatumika kuzuia, au timu ikishaingia uwanjani ikazuia kwa mfumo mwingine na kushambulia kwa mfumo mwingine.
Mifumo ya kushambulia imekuwa ikitumika kama 2-3-5, 3-1-6, 2-3-3-2, n.k.
Sasa twende pamoja ukaone jinsi Overload, hasa Pep Guardiola anavyoitumia pia makocha Kama Xavi, Arteta ,Erik Tan hag , Graham Potter jinsi wanavyocheza.
Ikiwa timu pinzani watacheza na mabeki wa 5, Guardiola atacheza na wachezaji 6 mbele.
Ikiwa timu pinzani itacheza na wachezaji wawili kwenye safu yao ya mbele(e.g 4-4-2,4-2-2-2,3-5-2,n.k) basi Guardiola utamuona atacheza na walinzi 3 (hivyo 3-1-6).
Ikiwa timu hiyo itacheza 5-4-1 (hivyo mchezaji mmoja katika safu yake ya mbele) Guardiola atacheza 2-2-6.
Man City walipocheza na Bournemouth , Bournemouth walilinda kwa shepu ya 5-4-1.
Manchester City walishambulia kwa uchezaji katika umbo la 2-2-6.
DM wa 2 ili kuwazidi idadi ya CF na 6 kwenye mstari wa mbele ili kuwazidi mabeki wao wa 5.
Angalia hapa,
CMs na Wingers/Full Backs kazi yao ni kuwezesha OVERLOAD katika maeneo mbalimbali.
Mfano mwingine huu hapa;
Nott’m Forest ililinda kwa 5-3-2 ilipocheza na Man City, Guardiola akaseti timu yake katika mfumo wa 3-1-6. Umbo hili linafanana sana na
3-Diamond-3.
Unaweza kuona jinsi wachezaji wa City wa kati wanavyoweza kuwazidi wachezaji wa Forest wa 5 na viungo wao wa 3.
CM ya kati (10) anakuwa huru ku OVERLOAD na kufanya yake.
Twende mfano Mwingine;
Mech ya Manchester City vs Man United.
Manchester Utd walijilinda kwa 4-2-3-1 lakini winga mmoja au AM ndio walitumika kupress CBs za City.
City walicheza 2-3-5 wakiwa na mabeki wa pembeni ili kuzuia mashambulizi ya kukabiliana ya Man U, lakini kama umegundua cha kwanza kama mpinzani atakubonyeza na mchezaji mmoja, basi unawekewa mabeki wawili ili waweze kufanya buildup watoke nyuma (hapa ndipo Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na GK mwenye uwezo mguuni)
Shepu hii ya 2-3-5 ilimpa nafasi katika kiungo wa chini siku hiyo ambaye alikuwa Gundogan (DM) kupeleka mipira kwa Haaland pia KDB na B.Silva kushambulia au kutumia half spaces.
OVERLOAD EVERYWHERE
Mechi ya Arsenal vs Spurs ni mfano wangu wa mwisho.
Conte aliingia na 3-4-3, lakini akawa anacheza kwa 5-4-1.
Arteta akaiseti timu yake kwenye shepu ya 2-3-5, kwanza kuweza kutoka nyuma kwa buildup ya 2v1, halafu kwenye Midfield anaongezeka Zinchenko na kuungana na Xhaka Partey na kufanya 3v2, sababu hawa wingbacks wanatolewa au kuondolewa na winga mbili za pembeni(Saka & Martinell) ambazo watacheza kwa kutanua uwanja hivo wingbacks Emerson Loyal na Perisic inabidi wawafate, na kuacha viungo wao wawili dhidi ya watatu wa Arsenal.
OVERLOAD EVERYWHERE
Note: HII OVERLOAD INAHITAJI WACHEZAJI MAALUM SIYO KILA MCHEZAJI ANAWEZA KUTEKELEZA MAJUKUMU HAYO.