Jamani sitaki kuamini kuwa wahusika ndo wameridhia picha yao irushwe mitandaoni ila picha itakuwa imeokotwa mahali na inarushwa tuu bila wahusika kujua.
Au itakuwa wamepiga picha kwa mpiga picha kule coco beach sasa hawajatokea tena kufuata picha yao na hawajailipia na kwa hasira wapiga picha ndo wanazirusha mitandaoni kuwakomoa.
Au itakuwa alipigwa na rafiki yake sasa wamegombana anaamua kumrusha mtandaoni ili kumkera au kumkomoa. Japo wamefanya haya hadharani kweupe ila ninauhakika hata kama hawa wahusiuka wana fb account huwezi kuta wamerusha picha hii kwenye wall zao vinginevyo watakuwa hawana soni looh, ni mtazamo wangu tuu.