mkuu.naomba tu uvune ulichokipanda.....hiyo mimba usiitoe......mlee na mtoto azaliwe.....muda ukifika mueleze mkeo ukweli....ingawa itauma lakini hiyo ndiyo hali halisi.......
Jumuia imezingatia kuwa kwa umri wako ungetakiwa uwe umeshalipatia ufumbuzi mapema sana.....kwani ni jambo jepesi ambalo hata wavulana huwa wanalimaliza kimya kimya...........mkuu,ultimatum umeitoa mapema sana mkuu,hivi hakuna ushauri sahihi naoweza kuupata kutoka katika jumuiya yetu hii kabla ya kunipa ultimatum?huoni kwamba jumuiya inanitenga bado mapema?
Seriously nahitaji ushauri, kwa akina baba wenzangu uzoefu wenu utanisaidia sana, kwa akina mama pia siyo mbaya kama una la kusema.
Kiongozi, tulia ulee familia yako. Wanawake hawaishi duniani na kila unaepishana nae njiani ni mzuri sana. Your kids need you, your family needs you. Ukibeba maradhi yasiyotibika utawaacha watoto wadogo na yatima na ndio mwanzo wa laana ndani ya nyumba yako.
Kuhusu hiyo mimba, ilee na mwambie huyo mchepuko kuwa utamhudumia mtoto coz ni wako, lakini kuhusu mahusiano tafadhali achana nae. Haya mambo hayaishi, yapo siku zote.
USHAURI WANGU;
1_Chukua maamuzi ya kumuacha huyo mchepuko kwa sababu upo kwenye ndoa na huwezi kumuoa kama mke wa pili.
2_Kapime magonjwa usije kumuambukiza mkeo ,mkaacha watoto yatima buree.
3_Tulia katika ndoa. Ukishaingia kwenye ndoa hakuna excuse kuwa ulikosea kuchagua.
I WISH YOU A HAPPY MARRIAGE
Jumuia imezingatia kuwa kwa umri wako ungetakiwa uwe umeshalipatia ufumbuzi mapema sana.....kwani ni jambo jepesi ambalo hata wavulana huwa wanalimaliza kimya kimya...........
Vijana tunaangamia kwa kukosa maarifa.
Mtoa maada umeikosea nafsi yako,umemkosea mkeo, umemkosea pia Mungu wako aliyeibariki nyumba yako na ndoa yako.
Vp kabla hujajiingiza kwenye mahusiano na huo mchepuko uliwahi kujiuliza haya maswali?
> kwann aliyezaa naye hajamuoa?
> inamaana wanaume woote hapo anapoishi hawajamuona? Kwann mpaka sasa bado ni single mom?
Kaka unaweza kujifarii kuwa mwanamke ni mzuri kumbe kuna wanyamwez wamekaa pemben wanakucheki tu jins ulivyojiingiza chakike.
Sometime wanaume tumekuwa chanzo cha migogoro. Hvi mkeo akipata hizo taarifa nayeye akaamua kukuletea mimba utalalamika?
thanx mkuu, i take 100% of your advice,usisite kunishauri endapo utapata mawazo mazuri zaidi ya haya
nashukuru mkuu,kuna tatizo lingine hapa ambalo nashindwa nilisolve vipi,ana ujauzito tayari wa miezi 2 sasa.
Sawa kijana onyesha uanamume wako kwa kufanya maamuzi magumu...sasa......i take the blame mr chairman,let me try to right the wrong
Kwa mfano we ndo ungekuwa mke wangu, afu usikie nimezaa na Heaven on Earth utanifanyaje kwa mfano?
Au tuoane kabisa??
thanx,naomba niendelee kuufanyia kazi ushauri wako but kama utapata mwingine bora zaidi ya huu tafadhali sana usisite kunishauri
Babu lazma niumie kiukweli lakini hakuna maumivu yanayokaa milele kuna muda maumivu yataisha na maisha yataendelea........lakini kutoa hukumu kwa mtoto ambae hana kosa lolote hilo unalionaje....?
mwisho wa siku nitakusamehe kama mme....mana ni sawa na mtoto wako wa kike kuzalia nyumbani....utamfanyeje?
Mmmmh mbona mtihani huu kiufupi ndio kashakuganda huyo....
Vipi moyo wako unasemaje kwani?
Asante sana sister kwa jibu lenye hekima ya juu sana. Ubarikiwe sana. Kama tungekuwa na wanawake wengi wa hivi hakika migogoro kwenye familia na ndoa ingekuwa inatatulika kirahisi.
Wanaume pia tupunguze au tusiendekeze tamaa, kumbuka wazuri wanazaliwa kila siku je utapenda wote?? Mwisho wa siku unajikuta umepoteza mali, heshima, nguvu za mwili na hata utulivu wa kufanya masuala mengine muhimu.
siyo kwamba sina msimamo farkhina,much as am in love with her,kuna maamuz ambayo siyo rahisi kama kuchinja kuku vile,yataka moyo kuwa na familia mbili,at the same time how do i part ways with her na tayari yuko preg?ndiyo maana nikaomba the best advice how to deal with this situation