**~** penzi la clara **~** | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

**~** penzi la clara **~**

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 18, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  SEHEMU YA KWANZA:

  Tangu utotoni nilijuwa kuwa nimejaliwa uzuri wa maumbile na sura. Nikiwa mtoto wa kike wa pekee na wa mwisho wa Mzee Erasto Malyamkono (mtaani alijulikana kama Mzee Mswahili) nilikuwa nimedekezwa nikadekeka. Kaka zangu walikuwa wakinichunga utadhani mboni ya jicho vile, na hakuna kitu nilichotamani ambacho sikukipata. Nilijitahidi kuitunza heshima yangu na heshima ya familia hususan maswala ya wanaume. Nilimaliza kidato cha nne kule Bwiru Mwanza na baadaye kujiunga na shule ya Masista wa Damu Takatifu kule Kifungilo Lushoto. Hadi naanza kidato cha tano nilikuwa bado bikira.

  Kabla ya hapo vijana wengi kule mtaani maeneo ya Isamilo walikuwa wakinitaka na kunifukuzia. Nawakumbuka kina Maiko, John, Almasi na Mugisha (alikuwa na umbo kubwa na kakichwa kidogo, utadhani hana shingo) wa pale magorofa ya Benki jinsi walivyokuwa wakinisarandia. Nilikuwa mcheshi na sikuwa na maringo yoyote. Yangu yalikuwa ni maneno na ahadi kem kem, lakini kuwavulia chupi la!! Nilikula vi pesa vyao vya sangara n(a kujinoma kwa tuzawadi twao.) Mademu wengi pale mtaani walinichukia sana, na hawakuficha wivu wao. Wengi waliokuwa wakinitaka walikuwa ni watoto wa wakubwa (miongoni mwao walikuwemo mtoto wa Jaji maarufu na mwingine alikuwa ni mtoto wa RPC). Namkumbuka mhindi mmoja ambaye naye alikuwa akinifukuzia ile mbaya. Nilijiona mimi ni malkia wa mbingu nikiitetemesha nchi kila nipitapo.

  Ilikuwa ni huko Lushoto ndiko nilikopata kwa mara ya kwanza kuonja joto la mapenzi. Ilikuwa ni likizo ya pili ndipo nilipokutana na Petro J Shekitondo (Alipenda kuitwa PJ). Basi letu lilisimama pale Mombo kwa ajili ya kujipatia chakula kabla ya kuendelea na safari yetu hadi Moshi. Yeye alikuwa ni mfanyakazi katika Hoteli ya Usambara, mojawapo ya hoteli mashuhuri pale Mombo. Nilikuwa nimekaa kwenye meza moja na marafiki zangu wawili; Sakina Mwanakibili (mtoto wa Mbunge) na Grace Chambi (mtoto wa Katibu wa Wizara, ambaye boyfriend wake alikuwa Mbunge mmoja).

  Tukiwa tunapeana gumzo, tulikatishwa mazungumzo yetu na kijana mrefu, aliyevalia suruali ya jeans na T-Shirt yenye maandishi ya “Daytona Beach” Kifuani. Alikuwa ni mtanashati na sote watatu tulijikuta tukipoteza mtiririko wa mawazo kwa sekunde.

  “Habari zenu” Alitusalimia kwa sauti nzito yenye upole
  “Powa” Tulimjibu kwa pamoja huku tukijifanya hatumjali “Mko tayari kuagiza chochote” Alituuliza tena akituangalia kwa kutupokeza.
  “Tupe dakika chache” Nilisema kwa niaba ya wenzangu, ambao waliafiki kwani muda wote huo tulikuwa tukipiga gumzo wala hatukuaangalia ile menu ubaoni.
  “Clara” Grace aliniita
  “Nini” Nilimjibu
  “Mbona unamuangalia kaka wa watu utadhani unataka kummeza!” Aliniambia
  “Hamna kitu, nilikuwa mbali tu” Nilimjibu, laiti wangejua ni umbali gani nilikuwa!!
  “aha!” Walihamaki wote wawili kana kwamba hawakuamini maneno yangu. Aliporudi tena alijitambulisha kwetu kwa jina na kuchukua oda zetu.

  Tulikula kwa haraka haraka kwani tulianza kusikia honi ya basi letu ikianza kulia. Kama kawaida tuliangalia alipokaa dereva na demu mmoja wakila, hatukuwa na haraka. Tulipomaliza kula tulijiandaa kuondoka. Kabla hata hatujafika nje tukasikia mtu akituita.
  “Samahani kina dada” Alikuwa ni PJ Shekitondo.
  “Nini tena” Tulimuuliza tukishangaa labda tumesahau kitu.
  “Dada wewe” akinionyesha mimi, “naomba nikuulize kitu” alisema. Tukasogea chemba. Akaja karibu yangu kiasi cha kusikia joto la mwili wake na akasogea kuninong’oneza jambo.
  “Tangu uingie hapa hotelini macho yangu yalikuwa kwako, natamani tufahamiane” Aliniambia na sauti kakamavu ilivunja vunja kila vizuio nilivyokuwa navyo. Sikuamini kuwa mwanamme anaweza kunigusa kihisia namna hiyo.
  “Mbona basi letu liko karibu kuondoka” Nilimjibu kwa aibu na kudengua kidogo
  “Si unasoma Kifungilo” Alinijibu kumbe alishajua mimi ni Mwanafunzi.
  “Umejuaje? Kwani tuna alama kwenye paji?” Nilimjibu kwa aibu.
  “Nimeshawahi kukuona mlipokuja Mazinde Juu kwa debate” Alinijibu. Dereva wa basi alitoka nje na kuelekea kwenye basi. Nikajua nilazime niamue haraka.
  “Sikiliza John” Nilimwambia, “Ninarudi tena shuleni mwezi ujao katikati, labda tuwasiliane wakati huo au vipi?” Nilimwambia.
  “Poa tu” Alinijibu.

  Alichukua kipande cha karatasi na kuandika namba yake ya simu na kuniambia kuwa siku nikiwa njiani kurudi nimpigie ili tukutane. Nilimwahidi kuwa nitampigia simu wakati nikirudi toka likizo. Nilikimbilia kupanda basi. Rafiki zangu waliniangalia kwa mshangao jinsi uso wangu ulivyong’ara kwa aibu na soni. Wakataka niwasimulie yaliyotokea. Nilisubiri kwa hamu siku ya kurudi toka likizo.

  ***

  Jinsi nilivyongojea kwa hamu likizo iishe. Nilikuwa najisomea vitabu, kuangalia TVs (hasa Oprah) na MTV n.k. Hata hivyo mawazo yangu yalikuwa kwa PJ tu. Sijui itakuwaje nikimuona, sijui bado atanionyesha kunitaka... nilifikiri nguo nitakazovaa na kama niweke nywele rasta au kalikiti. Kwa uchafu wangu wa mawazo nimwazia akiwa uchi mbele yangu!!, je nanihi yake kubwa kiasi gani!! Sijui niiguse au la. Mara nyingi nilijikuta nikijichekea mwenyewe. Katika hayo yote ilibidi nikubali mwenyewe kuwa sikuwa na utaalamu katika fani hiyo. Sijawahi kufanya mapenzi na mwanamume yeyote. Nilihisi kutetemeka kwani labda PJ anafikiri mimi nimeshawahi kuwa na mwanamume na hivyo atatarajia nimwonyeshe vitu vya nguvu kitandani. Itakuwaje basi nikiboronga? Nikatamani siku za zamani ambapo mabinti walikuwa wanakwenda unyago na kufunzwa na kufundwa!! Sijui nianzie wapi, nilijiwazia. Niseme wazi kuwa mambo mengi ya mapenzi nilijifunza toka gazeti la “Heko” kwenye darasa lake la Mapenzi na vitabu vingi vya mapenzi. Hata hivyo niligundua kuwa hakuna kitu mbadala zaidi ya kujifunza kwa vitendo. Nikaamua kuwa nitaenda kumwona dada Bupe.

  Bupe alikuwa ni miongoni mwa kina dada waliochangamkia biashara ya mapenzi. Nilitambulishwa kwake na wanafunzi wenzangu wakati tukisoma Bwiru. Baadhi ya wanafunzi wa Bwiru walikuwa wanaunganishwa na Bupe na vibosile wa Mwanza na walikuwa wakikutana nyumbani kwa da Bupe pale Pasiansi si mbali sana na ule uwanja wa ndege wa Mwanza. Dada Bupe alikuwa ni kama anawamiliki wasichana hao. Kila mwisho wa wiki tunapopata ruhusa ya kwenda mjini, wengi walikuwa wanaishia kwa Bupe. Nilipopewa nafasi hiyo mimi nilikataa na sikurudi tena. Lakini nikimuwazia PJ nikagundua kuwa hakuna mtu mwingine anayeweza kunisaidia zaidi ya dada Bupe. Nilifunga safari siku ya Alhamisi na kupanda vi- Express yaani daladala za Mwanza hadi Pasiansi. Kwa vile ilikuwa ni wakati wa likizo, sikutarajia kukuta “wageni wengi pale”. Kulikuwapo na gari moja Toyota lenye nembo ya “Jimbo Kuu la Mwanza” limeegeshwa uani. Nilipobisha hodi, si mwingine aliyefungua mlango ila dada Bupe. Sikutaka kujua gari la Jimbo linafanya nini kwa kungwi.

  “Karibu, nikusaidie nini?” Alijibu bila kuonyesha kama ananikumbua au la.
  “Shikamoo da Bupe” Nilimsalimu nikipiga goti langu kidogo kwa mtindo wa Kisukuma.
  “We acha kunizeesha, mambo vipi?” Badala ya kuitikia “marahaba” aliniyeyushia kiaina. Siku hiyo alikuwa amevalia kaptula ya khaki iliyomkaa vyema na alivalia T-shirt ya rangi nyekundu yenye maandishi ya kumetameta yasemayo “Playgirl”.
  “Hunikumbuki, da Bupe” nilimuuliza. Tulikuwa bado tumesimama mlangoni.
  “Nikumbushe basi usiniambie wewe ni ndugu yangu” Alisema akicheka.

  Nilimkumbusha jinsi nilivyokutana naye kwa mara ya kwanza wakati nikisoma Bwiru kama miaka michache tu iliyopita. Akataka kujua kilichonileta hapo kwake, nilimweleza kinaganaga jinsi nilivyojikuta niko njia panda. Nilimuomba msaada wa ushauri wake. Akanikaribisha ndani, kwenye sebule iliyopambwa vizuri kwa makochi ya kifahari na samani za kila aina.

  “Yaani unataka nikufundishe kufanya mapenzi” Aliniuliza
  “Ndiyo, na zaidi jinsi ya kumridhisha mwanamme” Nilimwambia
  “Ok, nitakufundisha itakugharimu lakini” Aliniambia
  “Shilingi ngapi?” Nilimuuliza
  “Shilingi eflu ishirini tu” Aliniambia bila hata ya kupoteza pumzi. Nilikubali.

  Akaniambia kuwa nirudi na hizo fedha kesho yake, na niwe tayari kwa somo la kwanza litakalohusisha mimi kuvunjwa bikira yangu. Nilirudi nyumbani nikijisia afueni lakini mwenye wasiwasi. Sikujua kama uamuzi wangu ulikuwa ni wa busara au la. Hata hivyo nikajisemea moyoni, “maji ukiyavulia nguo, huna budo uyaoge”. Nimeyavulia nguo, niko tayari kuyaoga.

  XXX ITAENDELEA XXX
   
 2. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ...........Ahsante kwa hadithi, l'll be right back.
   
 3. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Asante Mzee... This is Friday, unatuacha na hamu....
   
 4. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante Mwanakijiji hadithi imeanza kwa utamu!
   
 5. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji umeshawahi kuishi Isamilo?!
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Jamani Mwanakijiji na hadithi zako hongera sana kazi nzuri..natamani siku moja uniazime kichwa chako
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  nimepita pita mitaa hiyo..
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  halafu mimi mwenyewe nibakie wapi? LOL.. halafu utakifanya nini, nisije kuta kichwa changu kinapelekwa Ujerumani na wajanja fulani.. halafu kirudishwe TZ baada ya miaka 100
   
 9. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,082
  Trophy Points: 280
  hii hadithi ulishawahi kuitoa zamani sana zaidi ya miaka mitano iliyopita naikumbuka vizuri sana maana kichwa yangu ikiona kitu uwa kusahau ni shida maana nina GB Milioni 10 kichwani
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hata mie nakumbuka niliwahi kuipitia mitaa fulani lakini ni vyema akaendelea kutuwekea kumbukumbu hata kwa wale ambao hawajasoma waendelee kupata uhondo..

  FD unakumbuka hadithi za dada Chiku?
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ni kweli si mpya.. ila nimeufanyia mwisho wake mabadiliko kidogo..
   
 12. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,082
  Trophy Points: 280
  nazikumbuka vizuri tena kuna hadithi moja walikutana mwanakjj na da chiku ukiisoma lazima abdalah asimame dede
  halafu kuna hadithi moja ya mwanakijiji kuhusu UMISETA yaani kwa tuliopitia UMISETA ndio yale yale tuliyokuwa tunafanya
   
 13. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,082
  Trophy Points: 280
  nimezimiss sana zile hadithi nakumbuka nilizi-save ila laptonga langu liliingia HIV ikazila zote lol
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Vere Good kumbe unakumbuka vizuri...ngoja tuendelee kuburudika na Mwanakijiji ..
  Keep it up MMKJJ
   
 15. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hadithi nzuri sana.....mwanakijiji thanx.
   
 16. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,481
  Likes Received: 2,082
  Trophy Points: 280
  kwenye section ya kumbukumbu me ni zaidi ya Dr. Magufuli
   
 17. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji nikurudishe nyuma kidogo.
  ile story iliyokwisha ya 'MSALITI'
  Inavyoanza inaonekana yule mwanaume msaliti alikuwa anasimulia.
  Swali langu, alisimulia akiwa kaburini au? kwani inaonyesha aliuawa kwa kisu siku aliyofumaniwa so alipataje nafasi ya kusimulia?
  story zako ni Kali sana mkuu.
  Hongera sana bro.
   
 18. l

  lina kiwelu Member

  #18
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh, nashukuru kwa story yako. It is so interesting!!!
   
 19. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu asksante kwa mtundiko huu, kwa wale ambao hatukupata nafasi ya kuiona hiyo ya mwanzo naamini hatutakuwa tumeachwa sana. Hongera sana.
   
 20. valex

  valex Member

  #20
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 18, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wow nomeipendamo hadithi hii
  habari yako bana!
  valex
   
Loading...