Peniela (Story ya kijasusi)

EASON 2
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

ENDELEA………………………
Shughuli ya kuizika miili ya vijana sita waliopoteza maisha katika shambulio la kumuokoa mke wa Dr Michael ilimalizika saa kumi na moja na dakika ishirini na tatu.Mtu wa mwisho ambaye ni Aron mkibala alizikwa katika makaburi ya mkoroshini.Baada ya shughuli ile kukamilika vijana wote wa Team SC41 walitakiwa wakutane makao makuu
Wakati yote haya yakiendelea ,Josh kijana ambaye kwa muda mrefu amekuwa mlinzi wa John Mwaulaya alikuwa katika ofisi ya Osmund akikitafuta kile alichotumiwa na John.Si rahisi kuingia katika ofisi ya Osmund lakini Josh alifanikiwa kuingia katika ofisi hiyo kwa msaada mkubwa wa John Mwaulaya aliyempatia kadi maalum ya kufungulia mlangowa ofisi hiyo pamoja na namba za siri za kufungulia kompyuta ya Osmund.Baada ya kupata kile alichokuwa anakitafuta ,akatoka na kurejea katika makazi ya John mwaulaya
“ Mzee nimefanikiwa ulichonituma.Nimekwisha pata taarifa zote kuhusiana na Dr Burke kwa hiyo usijali nitaifanya kazi yako kikamilifu” akasema Josh
“ Ahsante sana Josh.Ahsante sana kwa kuendelea kuwa mtiifu.Nitakufanyia jambo kubwa kabla ya pumzi zangu kukatika” akasema John
“ Mzee tafadhali usiwaze kuhusiana na masuala hayo ya kifo.Be strong John.You can fight this”akasema Josh
“ I was as strong as a lion but now I’m very weak and I cant fight anymore.I cant fight this Josh .I’m going to die soon.” Akasema John Mwaulaya na kufumba macho na kwa mbali michirizi ya machozi ikaonekana machoni pake.Josh akamuonea huruma mzee yule aliyekuwa amelala pale kitandani ambaye ndiye aliyemuingiza katika Team SC41
“ John what can I do for you? Akauliza Josh
“ Leave me alone for now” akasema John na Josh akatoka mle chumbani na kumuacha John peke yake
“ Nilizoea kuzitoa roho za watu.Sikujua kama siku moja na mimi nitakufa.I’m so scared of death”akawaza John
“ Nimefanya mambo mengi sana mabaya katika kipindi chote cha masha yangu na zaidi baada ya kujiung a na TeamSC41 .Nimeua watu wengi,nimetesa watu wengi lakini ni kitu kimoja tu ambacho nina uhakika nilikifanya sawa.Sikumuua Peniela.Alikuwa mtoto mdogo na hakuwa na kosa lolote” akaendelea kuwaza John na sura ya Peniela ikamjia akatabasamu
“ Ni msichana mzuri sana lakini kuna kitu kimoja nimekikosea .Nilikosea sana kumuingza katika Team SC41.Japokuwa anapata kila kitu anachokihitaji lakini hana furaha ya maisha .Siku nilipomuingiza Team SC41 niliyaharibu maisha na ndoto zake zote.Peniela amekuwa akitumika katika mambo mengi ya hatari na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yake.Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba mwili wake mzuri umekuwa ukitumika kama silaha ya Team SC41 katika kufanikisha mambo mengi.Inaniuma sana kuyaharibu maisha yake namna hii” John akauma meno kwa uchungu
“ It’s not too late.kabla sijakata pumzi lazima nihakikishe kwamba Peniela amekuwa na maisha ya kawaida kama wasichana wengine.lazima nimuondoe katika Team SC41 .Lazima nihakikshe anaishi maisha ya kawaida.” Akawaza John na kumbukumbu zikamrejesha mbali siku Peniela alipomaliza elimu yake ya msingi
Ni siku ya mahafali ya darasa la saba katika shule ya St Patrick shule ambayo husoma watoto wa matajiri ..Peniela akiwa ni miongoni mwa wahitimu alikuwa na furaha isiyo kifani.Katika miaka yote saba aliyoitumia katika elimu yake ya msingi Peniela amekuwa ni mmoja kati ya wanafunzi hodari sana na mwenye kutiliwa mfano katika bidii ya masomo darasani,michezo,tabia njema na hata usafi.Kwa upande wa maisha ,japokuwa ni mtoto yatima lakini alikuwa akiisha maisha mazuri mno..Aliwezeshwa kupata kila alichokihitaji .sKulikuwa na gari maalum ya kumpeleka shuleni kila siku asubuhi nakumrejesha nyumbani,alipelekwa kila mahala alikotaka kwenda.Watu wengi hawakuamini kama Peniela ni mtoto yatima kutokana na maisha aliyokuwa akiishi.Peniela alitamani sana siku moja akutane na mtu yule ambaye amekuwa akimuwezesha kuishi maisha ya namna ile.Alijiona ni mtoto mwenye bahati kubwa kumpata mfadhili wa aina ile ambaye alimuwezesha kuishi maisha ya hali ya juu kiasi kile.Kila siku alikuwa akimlilia mama Bernadetha amuwezeshe kumkutanisha na huyo mfadhili wake ili aonane naye na amfahamu kwa sura lakini hadi anamaliza darasa la saba hakuwa amefanikiwa kukutana naye
Saa nne za asubuhi John Mwaulaya akiwa katika gari lake la kifahari aliwasili St Patrick school ili kuhudhuria sherehe za mahafali.Alikuwa na furaha usiyo kifani kwa Peniela kumaliza elimu yake ya msingi
“ She’s growing up so fast.Ni juzi tu alianza darasa la kwanza na leo tayari amemamliza darasa la saba ,Dah ! miaka inakimbia sana” akawaza John akishuka katika gari lake la kifahari na kuungana na watu wengine waliokuwa wamekuja katika mahafali haya
Sherehe zilikwenda vizuri na kabla ya sherehe kumalizika Bi Bernadetha akamuomba Peniela waongozane kuelekea sehemu Fulani kuna kitu anataka akamuonyeshe.Peniela aliingia katika gari wakaondoka bila kujua walikuwa wanaelekea wapi.
Safari yao iliwafikisha katika jumba moja kubwa lenye uzuri wa kipekee.Mlinzi alifungua geti wakaingia ndani.Uso wa Peniela ukapambwa na tabasamu la mshangao baada ya kuishuhudia mandhari ya kuvutia sana iliyokuwemo mle ndani.
Watu wanne walikuwa wamesimama katika mlango wa kuingilia sebuleni.Wote walikuwa na nyuso zenye tabasamu.
“ mama Bernadetha hapa ni wapi? Nani anaishi hapaauni hoteli ? Akauliza Peniela
“ Peniela sikuwa nimekwambai toka mwanzo nilitaka nikushangaze kidogo.Hi si hoteli mwanagu.Hii ni nyumba ya kuishi.Kuanzia dakika hii ni nyumba hii ni yako.Mfadhili wako amekuzawadia i kama zawadi yake kwako kwa kuhitimu elimu ya msingi na kuanzia le o utaishi hapa.Leo utayaanza maisha mapya Penny.” Akasema Bi Bernadetha na kumuacha Peniela akiwa na mshangao
“ mama Bernadetha ! akasema Penny kwa mshangao
“ Peniala najua umestuka sana na hata mimi nilistuka sana lakini na nimeumia sana kwamba hatutakuwa pamoja ,kwani wewe ni mtoto ambaye nimekuzoea sana na ninakupenda mno lakini haya ni matakwa ya mfadhili wako kwamba anataka aanze kukujengea maisha ya kujitegemea.Pamojana hayo naomba usijali Penny mimi bado nitaendelea kuwa mama yako na nitaendelea kuwa karibu nawe kwani nafahamu bado unahitaji sana msaada wangu” akasema Bi Bernadetha kisha wakakumbatiana na Peniela.
Walishuka katika gari na kuelekea ndani ,Bi Bernadetha akamtambulisha Peniela kwa watumishi ambao watakuwa wakimsaidia katika maisha yake ndani ya jumba lile.Alikuwepo mtumishi wa kazi za ndani,mpishi,na mtumishi mwingine ni wa kumsaidia peniela katika kazi zake ndongondogo na vile vile alikuwepo pia dereva wake maalum.Wote walifurahi kukutana na Peniela.Wakamzungusha Penny katika jumba lote na alifurahi sana
“ Mama bernadetha huyu mfadhili wangu anayenifanyia mambo haya makubwa ni nani? Kwa nini hutaki kunikutanisha naye ili nimfahamu na kumshukuru? Watu wa namna hii ni nadra sana kupatikana siku hizi.” Akasema Peniela baada ya kumaliza kutembezwa katika jumba lote
“ Peniela usijali siku moja utakunana na mfadhili wako na utamfahamu.Hata naye ana hamu sana ya kukutana nawe lakini ni mwingi wa safari za nje ya nchi” akasema Bi Bernadetha.
Peniela aliyaanza maisha mapya ndaniya jumba lile kubwa .Alijiona ni kama malkia.Saa tatu za usiku akiwa amejilaza katika kitanda kikubwa chumbani kwake simu iliyokuwa mezani ikaita akainuka na kuipokea.
“ Halow” akasema
“ hallow Peniela” ikasema sauti nzito ya kiume upande wa pili wa simu
“ Ninaongea na nani? Akauliza Peniela
“ Unaongea na John.Mimi ndiye mfadhili wako.”
Peniela akapatwa na furaha ya ajabu sana kwa kuisikia sauti ya mtu ambaye amekuwa akitamani kumuona kwa miaka mingi.
“ Baba John nakushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia.Sina neno zuri la kuweza kukushukru ila ninakuombea kwa Mungu akupe Baraka nyingi na mafanikio katika shughuli zako” akasema Penny huku akilengwa na machozi kwa hisia kali
“ Peniela nashukuru kwa Baraka zako lakini naomba tu ufahamu kwamba kukosa wazazi si kigezo cha kukufanya uishi maisha ya shida.Unastahili kuishi maisha mazuri kama watoto wengine na hicho ndicho ninachojitahidi kukifanya kuhakikisha kwamba maisha yako yanakuwa mazuri.Umeionaje nyumba yako? Inakufaa?
“ baba John,sina cha kusema ,kila kitu ni kizuri .Siamini kama hata mimi yatima leo hii ninaweza kuishi ndaniya jumba kubwa na zuri kama hili.Mungu akubariki sana baba” akasema Penny
“ Penny kuna picha moja kubwa ya bahari ukutani umeiona?
“ Ndiyo baba nimeiona”
“ Ok nenda kaitoe ile picha na nyuma yake utakuta kuna kasiki lina namba kisha lifungue kasiki hilo kwa namba hizi” akasema John na kumtajia Peniela namba za kufungulia kasiki lile.Peniela akafanya kama alivyoelekezwa
“ Tayari baba nimelifungua”
“ Ok Vizuri .Ndani ya kasiki hilo kuna hati ya nyumba na kadi ya gari ,kadi ya benki na nyaraka nyinginezo .Kila kitu kina jina lako.” Akasema John
“ Baba ahsante sana lakini nina kitu kimoja bado kinanisumbua sana akili yangu”
“ Kitugani Peniela?
“ Ninataka kukuona.Moyo wangu utakuwa na furaha kubwa kama nikikuona.Tafadhali baba naomba uniruhusu nikuone, walau niione sura yako” akaomba Peniela.John akacheka kidogo nakusema
“Usijali Peniela siku moja tutaonana.Nitakuwa nikiwasiliana nawe kila siku kujua maendeleo yako.Kwa heri peniela” John akakata simu
Kumbu kumbu ile ikayafanya macho ya John yaloe machozi.
“ She was so beautiful na maisha yake yalikuwa na furaha sana .Lazima nimrudishie furaha yake aliyokuwa nayo wakati ule.Lazima nimuondoe teamSC 41” Akawaza John

******

Mathew,Anitha na Noah walikuwa katika chumba chao cha kazi.Pamoja nao alikuwepo mtaalamu wa program za kompyuta Arnold ambaye walikuwa wakimshikilia .Wote macho yao yalikuwa katika simu iliyokuwepo mezani wakisubiri simu kutoka kwa watu ambao walitakiwa kukutana na Arnold jioni ile.Simu nyingi zilikuwa zikipigwa na kila simu iliyopigwa Arnold alidai haikuwa yenyewe
“ Arnold una hakika hao jamaa watapiga? Akauliza Mathew baada ya kuona muda unazidi kuyoyoma na hakuna simu yoyote iliyopigwa
“ Watapiga tu,makubalinao yetu ni kwamba leo hii lazima niwapatie mzigo wao na wao wanilipe fedha zangu zilizobaki.Kama nilivyowaambia kwamba tulikubaliana kukutana kuanzia saa moja za jioni leo “
Waliendelea kusubiri na ilipotimu saa kumi na mbili na dakika ishirini na tatu simu ikapigwa na Arnold akaitambua kwamba ,ni ya wale jamaa.Wote wakatega masikio .Arnold akabonyeza kitufe cha kupokelea
“ Hallow “ akasema
“ Arnold .Kila kitu kiko tayari? Ikauliza sautiya upande wa pili
“ Ndiyo kila kitu kiko tayari.Ninasubiri maelekezo yenu”akasema Arnold
“ Ok Vizuri .Tukutane Triple S casino ghorofa ya tatu kaunta C.Jitahidi hadi saa moja na robo uwe umewasili ”akasema yule jamaa
“sawa nitafika kabla ya muda huo” akajibu Arnold na simu ikakatwa
“haya kumekucha “ akasema Mathew
“ sasa tunaelekea tena kazini.Noah wewe kwa kuwa bado haujapona vizuri jeraha lako utabaki hapa na nitaongozana na Anitha.”
“ sawa hakuna shida Mathew” akajibu Noah
“ Anitha kila kitu ulikiweka sawa katika ile tablet? Akauliza Mathew
“ Kila kitu kiko tayari.”akasema Anitha kisha Mathew akamgeukia Arnold
“ Arnold tunakwenda sote huko Casino na utawakabidhi hao jamaa kifaa chao lakini nakuonya tutakuwa karibu tukifuatilia kila kinachoendelea kwa hiyo usijaribu kwa namna yoyote ile kuwatamkia kitu chochote kwamba tunawafuatilia.Wakabidhi kifaa chao kisha utatuachia sisi kazi ya kuendelea kuwafuatilia.Ukienda kinyume na tunachokuamuru fahamu kwamba jua la kesho hutaliona.Tumeelewana Arnold? Akauliza Mathew kwa ukali
“Tumeelewana ndugu zangu.Ntafanya kama mlivyoniamuru lakini kuna mambo bado nahitaji kuyafahamu,ninyi ni akina nani? Na hawa jamaa walionipa hii kazi mnawafahamu? Akauliza Arnold
“ Watu hawa waliokupa hii kazi hatuwafahamu lakini tunahitaji k uwafahamu ni akina nani na ndiyo maana tunawafuatilia Ili tuwafahamu na vile vile tufahamu ni kitu gani wnachokitafuta kwa Eva.”akasema Mathew
“Nina wasi wasi kama hawa jamaa ni watu wabaya wanaweza wakanifanyia kitu kibaya au hata kuniua mara tu nitakapowakabidhi kifaa chao “akasema Arnold
“Usijali Arnold sisi tutakuwepo karibu tunakufuatilia na tutakulinda” akasema Mathew
Noah akamchukua Arnold na kumpeleka bafuni akaoga kisha akapewa suti moja ya Mathew akavaa na kujiweka tayari kwa safari ya kuelekea Triple S casino.Baada ya dakika kumi wote walikuwa tayari wakaingia garini na kuondoka wakimuacha Noah peke yake nyumbani
Dakika kumi tu toka akina Mathew waondoke jaji Elibariki akawasili na kumkuta Noah peke yake .
“ Mathew ametoka kuna mahala amekwenda ila amesema hatachelewa sana kurudi na amesema ukifika umsubiri” akasema Noah Jaji Elibariki akajiegemeza katika sofa na kuvuta pumzi ndefu. Alionekana ni mchovu na mwingi wa mawazo
“ Bado sielewi ni kwa nini rais anakubali kudanganywa na wasaidizi wake kiasi hiki ? Kwa nini amekataa kuikubali taarifa yangu ya ukweli? Kitu gani kinaendelea ndani ya Ikulu? Lazima tufanye uchunguzi wa kina tubaini kinachoendelea ndani ya jengo lile.” Jaji Elibariki akastuliwa toka mawazo nina simu yake iliyokuwa ikiita.Akaichomoa toka mfuko wa koti na kutazama mpigaji alikuwa ni mkewe Flaviana
“ Hallow Flaviana”akasema
“Eli uko wapi? Mbona sikuoni hapa? Nimetuma watu wakutafute lakini wamekukosa.Ninakuhitaji kukuona” akasema Flaviana.Elibariki akafikiri kidogo na kusema
“ Flaviana nimetoka kidogo .Mzee amenichefua sana leo”
“ Unaweza ukaja kidogo tukaonana Eli?
“ Niko mbali kdogo.Kunanini?
“ Nataka tuongee kuhusiana na lile suala”
“ Hakuna cha kuongea Flaviana.Hakuna kati yenu anayetaka kuniamini .Hakuna anayetaka kuiamini taarifa niliyowapa.Nyote mnakubaliana na alichokisema baba yenu”
“ Eli si kwamba hatukuamini lakini mambo haya yanachanganya sana .Hapa nilipo nimechanganyikiwa na sijui nielekee upande upi”
“ Flavina ni wewe ndiye uliyeniambia nikusaidie kutafuta kilichomuua mama yako na nilifanya ulivyoniomba.Hujui ni mambo gani yaliyotokea hadi taarifa ile ikapatikana.lakini pamoja na hayo sikulazimishi wewe wala yeyote katika familia yenu akubaliane na mimi lakini siku moja ukweli utadhihiri” akasema jaji Elibariki
“ Eli tafadhali naomba tuachane na hili suala kwani limekuwa gumu sana.Vyovyote vile itakavyokuwa mama yangu amekwisha fariki na hatafufuka.Jambo la msingi nililoamua mimi ni kuachana kabisa na suala hili.Kama mama aliuawa basi waliofanya hivyo siku moja watahukumiwa mbele za haki.” Akasema Flaviana
“ Flaviana mimi ni jaji wa Mahakama kuu na siku zote kazi yangu ni kuhakikisha haki imetendeka.Siwezi kuliacha suala hili hadi nifike nalo mwisho na ukweli lazima ujulikane” akasema jaji Elibariki
“ Eli tafadhali nakuomba usiliendeleze tena suala hili kwani tayari baba amekwisha lifunga. .Liache kama lilivyo”
“ Hapana Flavina siwezi kuliacha hivi hivi.Baba yako amenidharau sana na kuniona kama kitu kisicho na thamani yoyote.Nataka nimdhihirishie kwamba siku zote huwa na simama katika haki na ukweli.Sintalala usingizi hadi nimdhihirishie kwamba nilikuwa sahihi na siku zote huwa niko sahihi”akasema jaji Elibariki
“Eli tafadhali naomba kabla hujafanya chochote naomba kwanza tuonane.Please Eli “ akasema Flaviana
“ Ok ninakuja” akasema Elibariki na kukata simu
Wakati Flavina na jaji Elibariki wakiongea simuni,maongezi yao yalikuwa yanasikika katika gari moja jeusi aina ya Ford lililokuwa na watu watatu ndani, kupitia katika chombo Fulani kilichokuwa kimeunagnishwa na simu ya Flaviana bila ya yeye kujua wakati alipopoteza fahamu mchana na kupakiwa katika gari la wagonjwa na kukimbizwa hospitali.Flaviana hakufahamu chochote kuhusiana na simu yake kuunganishwa na chombo maalum ambacho kingeweza kunasa maongezi yoyote ambayo angeongea kupitia simu yake.Mara tu simu ilipokatwa mmoja wa wale jamaa watatu akachukua simu na kuzitafuta namba za Dr Kigomba akapiga
“ Hallow Austin.Kuna habari gani? Ikauliza sauti ya upande wa pili ya Dr Kigomba
“Dr Kigomba tumefanikiwa kunasa maongezi kati ya Flaviana na mumewe.Nina kutumia sasa hivi uyasikilize halafu utuambie nini cha kufanya” akasema Austin na kisha akamtumia Dr Kigomba maongezi yale ya Flaviana na Jaji Elibariki ambayo tayari yalikwisha rekodiwa katika kompyuta.
Dr Kigomba aliyasikiliza kwa makini maongezi yale kati ya Flaviana na mumewe akayarudia kuyasikiliza tena halafu akampigia simu Dr Joshua na kumuomba waonane.Baada ya dakika kumi wakakutana.
“Kuna nini Kigomba? Akauliza Dr Joshua.Dr Kigomba akatoa simu yake na kumpa Dr Joshua asikilize maongezi yale.Akasikiliza na kuyarudia tena kisha akamgeukia Dr Kigomba
“ Dr Kigomba nilikueleza toka mapema kwamba huyu jamaa ni hatari sana.Kama alivyomwambia mkewe kwamba hatalala hadi ahakikishe ametulipua.” akasema Dr Joshua
“ Unashauri nini Dr Joshua” akauliza Dr Kigomba
“ Muondoeni haraka iwezekanavyo.Ila kumbuka kwamba umakini mkubwa unahitajika katika jambo hili ili kuwafanya watu wasiwe na aina yoyote ya shaka.”akasema Dr Kigomba
“ What about an accident? akauliza Dr Kigomba
“ Yes ! do it.Make it looks like real” akasema Dr Joshua
“ Ok Mr President.Hivi sasa Elibariki yuko njiani anakuja na kazi itafanyika usiku wa leo” akasema Dr Kigomba

TUKUTANE TENA SEHEMU IJAYO…
 
sijajua mnachokilalamika ni nn wakuu jana nilisema kuwa kama nitapata mda ule ule usiku nitaongeza 5 but nilizongwa na mambo nikashindwa na niliwaambia kuwa kama nitashindwa basi tukutane saa 2 usiku wazee??

mbali na JF kuna maisha mengine ndio maana kila mtu aningia kwa mda wake anapopata mda wengine kutwa mnashinda kwenye pc au na sim mkononi mkiperuz sababu shughuli mnazozifanya zinaruhusu ila ss wengine ni ngum sana wakuu.tuvumiliane.mwanzo nilijitahidi sana lkn now time zinanibana
Ok
 
PENIELA SEASON 3

SEHEMU YA 20

ILIPOISHAI SEHEMU ILIYOPITA
“Nimestushwa sana Kigomba kwa taarifa hizi.Ngoja nizungumze na mkuu wa polisi nifahamu kama kuna hatua yoyote imefikiwa kuchunguza waliomuua Amos.Kigomba kwa mara ya kwanza nimeogopa sana.Kama Amos ameuawa basi watu walionfaya hivyo wako karibu sana kutufikia na sisi pia.Please make sure hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kutuunganisha sisi na Amos.Kigomba this is a very serious matter and take it very seriously.Nitakupigia baada ya masaa mawili kujua kinachoendelea na tutaongea zaidi”
“ sawa Mr President lakini wa mujibu wa taarifa za polisi watu waliofanya mauaji hayo wameondoka na kompyuta na simu ya Amos.” “Kigomba something is going on.Kuna kitu kinatafutwa kwa Amos.We need to hurry.Tunatakiwa tuimalize biashara yetu haraka iwekanavyo .Ntakupigia tena baadae kidogo”akasema Dr Joshua na kukata simu.


ENDELEA…………………….

“ Vifo vilivyotokea mfululizo vimemuogopesha sana Dr Joshua nandiyo maana anataka kuitoa package hiyo haraka kwani ana wasiwasi kwamba kuna watu wengine wanaoitolea macho package hiyo.Kwa maelezo yake mwenyewe alikiri kwamba anataka makabidhiano yafanyike haraka pindi tu akirejea kutoka afrila ya kusini kwani tayari pesa imekiwsha ingizwa katika akaunti zao za sri walizofungua nje ya nchi.Amemtaja Hussein kwamba atawasili kesho jioni na huyu inaonekana ndiye ambaye anakuja kukabidhwa package hiyo.Kwahiyo jamani ile kazi yetu ya msingi iko mbioni kukamilika.Umakini wa hali ya juu sana unahitajika.Tutakaa na kulijadili hilo baadae kidogo lakini kwa sasa tuanze kumuandaa Peniela kwa ajili ya kwenda kuonana na Deus Mkozumi.” Akasema Mathew kisha akamuomba jaji Elibariki aongozane naye wakaelekea katika chumba alimo Rosemary.Mara tu walipoingia mle chumbani Rosemary akastuka sana baada ya kumuona jaji Elibariki “I know you !! akasema Rose. “ unanifahamu? Akauliza jaji Elibariki.Hakutegemea kama Rose angemtambua
“ Elibariki ,right? Jaji Elibariki..Ninakufahamu sana.Kumbe na wewe uko na hawa mashetani.Who are you guys? Akauliza Rose akishangaa sana kumuona jaj Elibariki pale. Mathew akafungua mlango uliokuwa pembeni na ndani ya chumba kile kukaonekana vifaa mbalimbali akatoa kiti cha magurudumu na kukisogeza karibu na kitanda alicholazwa Rose.Akamfungua pingu na kumuomba Elibariki amsaidiea kumuinua Rose wakamuweka katika kile kiti.
“ Mnanipeleka wapi? Akauliza Rose.Mathew akakisukuma kiti kile hadi chumbani kwake halafu akaenda katika kisanduku Fulani kilichokuwa ukutani kilichokuwa na muundo kama simu akabonyeza namba kadhaa na mara kabati kubwa la vitabu likasogea pembeni na ukaonekana mlango.Mathew akaufungua ule mlango nakulionekana kuna ngazi za kushuka chini.Mathew akamuamuru Elibariki amfuate waksshuka ngazi kuelekea chini..Elibariki na Rose wakabaki wanashangaa.
“ who are you ? Hii nyumba ya chini ni kwa ajili gani?akauliza Rose lakini Mathew hakumjibu kitu..Waliingia katika chumba kimoja kikubwa kilichokuwa na kitanda kikubwa meza ya kulia chakula,meza ya kusomea,kabati kubwa la nguo bila kusahau Luninga kubwa iliyokuwa ukutani.Wakamnyanyua Rose na kumuweka kitandani.
“ Rose suala lako uliloliomba tunalishughulikia na litakapokuwa tayari tutakutaarifu lakini mpaka wakati huo this will be your new home.Hii ni nyumba iliyoko chini ya ardhi .Nobody will know you are here.Usihofu sisi si watu makatili kama unavyodhani lakini huwa tunalazimika kuwa wakali kwa watu kama ninyi ambao mnashirikiana na magaidi.Kwa sasa pumzikanitakuwa na maongezi nawe baadae” Akasema Mathew huku akimfunga pingu za mikono na miguu.
“ Mpaka lini mtaendelea kunifunga pingu hizi ? akauliza kwa ukali Rose
“ Mpaka hapo tutakapopata kila tunachokihitaji toka kwako”akasema Mathew.
“ tafadhali naomba msinifunge namna hii,.Mnanitesa sana.Vipi kama nikihitaji kujisaidia “ akaomba Rose
“ Jisaidie hapo hapo.You deserve to be in chain mpaka hapo rais atakaporejea na hatujui atarejea lini yawezekana ikawa ni kesho,wiki ijayo,baada ya miezi au hata mwaka “ akasema Mathew na kisha wakatoka mle chumbani wakimuacha Rose akiangua kilio
“ Mathew umejiandaa sana.Sikutegema kama nyumba yako inaweza kuwa na mambo mengi ya siri namna hii”akasema Elibariki
“ Kutokana na kazi ninayoifanya,nimelazimika kutengeneza nyumb aiwe namna hii ili kuniwezesha kufanya kazi zangu bila wasiwasi.”akasema Mathew wakati wakipanda ngazi kurejea sebuleni.Wakaelekea ofisini alikuwemo Anitha peke yake.
“ peniela yuko wapi? akauliza Mathew
“ Nimempeleka chumbani anajaribu mavazi,can you check on her Mathew if she’s ready ? kuna kitu ninamalizia katika komyuta hapa”akaomba Anitha..Mathew akatoka na kuelekea katika chumba cha Anitha akaufungua mlango na kuchungulia ndani.Akapatwa na mstuko wa ghafla kwa alichokiona ndani..Peniela alikuwa amegeukia katika kioo akijipodoa.Alikuwa na nguo za ndani pekee.
“ ouh my gosh ! akasema Mathew kwa sauti ndogo na kubaki anamkodolea macho binti Yule mwenye uzuri usioelezeka..
“ Ndiyo maana kumbe wanaume wanachanganyikiwa kwa ajili yake.She’s hot !!
akawaza huku akiwa amejisahau kabisa akiendelea kumtazama Peniela..Kupitia kioo cha kujitazamia Peniela alimuona Mathew namna alivyostuka baada ya kumkuta katika hali ile.Hakutaka kumstua akamuacha aendelee kumtazama. kwa makusudi akainama kujipaka mafuta miguuni.Mathew akaufunga mlango na kusimama pale nje kwa sekunde kadhaa
“ Dah ! Kitu gani kimeniambia nije huku chumbani hadi nimekutana na mambo haya? Nimekwisha mzoea Anitha mara nyingi tu huwa ninamshuhudia akiwa mtupu lakini hakuna chochote kinachonitokea ila kwa peniela imekuwa tofauti kabisa.Nimepata msisimko wa ajabu.This woman have got smething special to attract men” akawaza na kupiga hatua za haraka haraka kuelekea chumbani kwake kwani tayari ikulu kulikwisha kasirika na mambo yalikwisha haribika..Haraka haraka akaingia bafuni akaoga na kubadili nguo kisha akafungua kasiki lake ambalo huhifadhia vifaa mbalimbali na silaha akachagua vitu ambavyo wangevihitaji kwa usiku ule na kutoka akaeleka ofisini ambako Anitha alikuwa anamalizia kuweka sawa program kadhaa katika kompyuta yake..
“ is everything ready? akauliza Mathew
“ Nimeshamaliza kuweka kila kitu tayari.” Akasema Anitha. Na mara akatokea Peniela akiwa katika gauni jeusi la Anitha lililomkaa vyema sana.
“ dah ! Peniela !! Huyu mwanamke amebarikiwa uzuri wa ajabu sana.Sikuwahi kuifahamu siri yake ya kuwadatisha wanaume kiasi hiki leo nimegundua.Mtoto huyu akiwa hana nguo huwezi amini ni binadamu wa kawaida.She looks like an angel”akawaza Mathew huku akimtazama Peniela
“ hello Mathew How do I look?akauliza Penela
“ You look wonderful..unafanana sana na malaika” akasema Mathew na wote wakacheka.
“ Anitha mimi niko tayari sasa ni zamu yako kuniandaa”akasema Peniela.Anitha akafungua kisanduku kidogo akatoa vidude Fulani vinne kama vispika vidogo akachukua kimoja na kukipachika sikioni kwa Peniela halafu kingine akampatia Mathew na kingine akaweka katika sikio lake
“Hivi ni vifaa vya mawasiliano ambavyo vitawezesha kuwasiliana .Kupitia vifaahivi tutasikia kila utakakachokiongea na Deus na sisi tutakuongoza nini ukiseme .Usifanye chochote bila ya maelekezo yetu.”akasema Anitha halafu akafungua kiboksi kidogo akatoa kijiua kidogo cheusi akakipachika katika sehemu ya titi la kulia .
“ Hili ukilitazama ni kama ua linaloongeza urembo katika nguo uliyovaa lakini kidude hiki katikati ya ua kinachoonekana kama pini ya ua ni kamera ambayo ndiyo itatuwezesha sisi kutazama kila kitu kitakachofanyika ukiwa na Deus.Kwa kujaribu Mathew mpeleke chumbani kwa Naomi akaongee naye jambo lolote ili tuijaribu kamera” .Akasema Anitha
“ Lets us go.I’ll show you the room” akasema Mathew na kumuongoza Peniela kueleka katika chumba cha Naomi akagonga mlango Naomi akafungua Peniela akaingia Kila walichokiongea Peniela na Naomi kikaonekana katika kompyta ndogo ya Anitha
“ Kila kitu kinakwenda vizuri .kwa upande wangu nimemaliza”akasemaAnitha.Mathew akamfuata Peniela chumbani kwa Naomi akamtaarifu kwamba kila kitu tayari na wanaweza wakaondoka halafu akaongea na Naomi akamfahamisha kwamba wanatoka kidogo kuna mahala wanaelekea na watarejea baadae kisha akatoka hadi katika nyumba yake ya magari akatoa gari moja ambao hulitumia mara chache sana.Mle ndani alikuwa na magari sita
“ hili ndilo gari analostahili kulitumia Peniela leo.Anastahili gari kama hili.She’s ana angel”akawaza Mathew akilijaribu gari.Aliporidhika liko vizuri akarejea ndani.
“ Kila kitu tayari we can leave now.Elibariki utaangalia kila kitu hapa ndani.Utamuangalia Naomi na endapo kuna tatizo lolote utatujulisha mara moja kwa kutumia simu ile ofisini” akasema Mathew
“ Mathew tafadhali kuwa makini sana.Take good care of peniela. “ akasisitiza Elibariki “ I will” akasema Mathew.Elibariki na peniela wakakumbatiana kwa muda
“ Please be carefull Peniela.”akasema Elibariki
“ I will Eli” akajibu Peniela akumbusu Elibariki kisha akaongozana na Mathew na anitha kueleka nje.Peniela akaingia katika gari aliloandaliwa na kutangulia.Mathew na Anitha wakafuata nyuma yake.Elibariki akafunga geti na kurejea ndani akajilaza sofani. Mawazo mengi kuhusiana na kinachoendelea.
“ Sikuwahi kuota kama siku moja maisha yangu yanaweza yakabadilika na kuwa hivi..Mtu niliyekuwa ninaheshimika leo hii nimejificha humu ndani ninasakwa kila kona ya nchi..” Mara Elibariki akastuliwa toka mawazoni na mtu aliyeingia pale sebuleni alikuwa ni Naomi.
“ Hallow” akasema Naomi
“umenistua sana ,nilikuwa nimezama katika mawazo mengi.”akasema jaji Elibariki.
‘” Pole..”akajibu Naomi huku akicheka kidogo kisha akaenda kuketi sofani
“ Wamekwenda wapi akina Peniela?akauliza Naomi
“ Kuna mahala wamekwenda na watarejea muda si mrefu sana.Kuna kitu unahitaji? Chakula tayari kipo jikoni.Mfumo wa hapa ukihisi njaa unakwenda mwenyewe jikoni unatafuta chakula unachokitaka unakula.Vyakula vingi vya hapa ni vya maboksi .Ndani ya nyumba hii watu wanafanya kazi muda wote kiasi kwamba hawakumbuki hata kula kwa hiyo kama unahisi njaa tafadhali nenda jikoni utaangalia wewe mwenyewe unataka kula kitu gani” akasema jaji Elibariki.
“ Nadhani nyumba hii mnahitaji sana mtu wa kuwasaidia,kuwapikia n.k.Sura zote zinaonekana sura za kazi .Kesho nitakwenda kununua mahitaji ya ndani.Hamuwezi mkafanyakazi mkasahau kula..Anyway tuachane na hayo wewe ni jaji si ndiyo?
“ Ndiyo mimi ni jaji wa mahakama kuu.naitwa jaji Elibariki.”
“ Nimefurahi kukufahamu.Mbona hukuambatana na akina Mathew? Akauliza Naomi
“ Sitakiwi kuonekana huko nje”akajibu Elbariki kwa ufupi
“ Unatafutwa? Ulifanya nini?
“ Ni hadithi ndefu sana ambayo siwezi kukuelezea kwa sasa” akajibu Elibariki.Kikapita kimya kifupi Naomi akauliza
“ Mke wako anafahamu kama unaishi hapa?
“ Sina mke” akajibu Elibariki
“ Huna mke? Naomi akashangaa
“ Ndiyo sina mke kwa sasa.She’s dead”akasema Elibariki.
“ Pole sana jaji .Sikulifahamu hilo.” Akasema naomi
“ yah ni mapenzi ya Mungu.”
" Kwa hiyo una mpango gani hivi sasa kuhus maisha yako? Hufikirii kuoa tena?bado kijana sana” Akauliza Naomi
“ kwa sasa ni mapema sana kusema chochote kuhusu mpango wa kuoa tena kwa sababu hata mke wangu bado hajazikwa” akasema Elibaliki na kumstua sana Naomi
“Ina maana amefariki si muda mrefu?
" Asubuhi ya leo” akajibu Elibariki “leo ?!! Naomi akazidi kushangaa “Ndiyo .”
“ Kwa hiyo huruhusiwi hata kuhudhuria msiba? “ kama nilivyokwambia awali kwamba siruhusiwi kabisa hata kuonekana huko nje.Ninasakwa kila kona”
“Ulifanya nini?
“ni hadthi ndefu sana .Nitakusimulia siku nyingine.”
“ jamani pole sana jaji.Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.” Akasema Naomi na kuinuka akelekea jikoni akafungu fungua makabati kuangalia kuna kitu gani ambacho wanaweza kula kwa usiku ule
“ Kweli hii ni nyumba ya watu wa kazi .Vyakula vyao vyote ni vile vya makopo.Nataka nimtengenezee jaji Chakula aweze kula..Kwa hali aliyo nayo anatakiwa apate chakula ili awe na nguvu.Namuonea huruma sana yule kaka.Kufiwa si jambo dogo” akawaza Naomi huku akiwasha jiko na kuanza kutengeneza chakula.
“ Ninamshukuru sana Mathew kwa kuniweka huru kasi hiki.Nitafurahi sana kama nikiendelea kukaa hapa kwake siku zote.Ninahisi amani sana nikiwa ndani ya numba hii.Mathew ni mtu mzuri na ana moyo wa huruma.Hata watu anaofanya nao kazi vile vile ni watu wazuri sana.” Akawaza Naomi na mara akamkmbuka Elibariki
“He’s so handsome…sijui kwa nini ametokea kunivutia sana yule jaji...Nitajitahidi nijenge ukaribu naye..” akaendelea kuwaza Baada ya kama dakika kumi na tano chakula kikawa tayari akabeba sahani mbili na kwenda nazo sebuleni.
‘” jaji karibu chakula” akasema “ Wow Naomi kumbe ni mpishi mzuri .Chakula kinanukia sana.lakini hata hivyo ahsante sina hamu ya kula.” Akasema jaji Elibariki
“ jaji lazima ule chakula ili upate nguvu ya kukabiliana na wakati huu mgumu ulio nao” akasema Naomi
“ Naomi najitahidi sana kujilazimisha lakini chakula hakipiti.” Akasema Elibarii
“ sawa jaji naomba nikulishe mimi kwa mkono wangu kitapita tu”akasema Naomi na kwenda kukaa karibu na jaji Elibariki akachukua kijiko na kumuwekea jaji Elibariki chakula mdomoni.Elibariki akacheka kidogo kisha akasema
“ Ahsante sana Naomi.naomba niendelee kula mwenyewe.” Akasema jaji Elibariki
“ hapana jaji.Kaa utulie .Nataka nihakkishe umekula chakula chote hiki umekimaliza” akasema Naomi na kuendelea na zoezi lake na akahakikisha Elibariki amemaliza chakula chote
“ nashukuru sana mdogo wangu kwa chakula.Bila wewe nisingekuwa na nguvu ya kutia chochote tumboni.”akasema jaji Elibariki. Waliendelea kukaa pale sebuleni wakitazama filamu kisha Naomi akasema
“ Its bored in here.twende tukakae pale katika bwawa la kuogelea” Jaji Elibariki hakupenda kwenda nje lakin Naomi akamshika mkono akamvuta naakakubali kuinuka wakaeleka katika bwawa la kuogelea ,. “ Unajua kuogelea? .” akauliza Naomi
“ ndiyo ninaweza lakini nina muda mrefu sana sijaogelea”
“ Ok let’s swim.” “Not today naom......“ Kabla hajamalizia sentensi yake Naomi akamsukumia Elibariki ndani ya maji naye akajitupia majini na kuzama chini kisha akaibuka na kumfuata Elibariki aliyekuwa amejiegemeza katika kingo za bwawa lile
“ Naomi mbona we mtundu sana.Nimekwambia leo sijisikii kuogelea” akasema jaji Elibariki
“ najua una matatizo jaji hata mimi nina matatizo yangu tenamakubwa tu lakini pamoja na matatizo tuliyonayo ninataka uchangamke na uondoe mawazo.Maisha lazima yaendelee.”akasema Naomi na kumsogelea Elibariki.Wakaangaliana usoni kwa sekunde kadhaa.halafu kiuchokozi akaupeleka mkono wake kunako ikulu ya Elibariki
“ Naomi unafanya nini?
“ Shhhhh !!!.akasema Naomi
“ watu wote hawapo tuko peke yetu hakuna ubaya kama tukistarehe nakupunguza mawazo tuliyo nayo.” Akasema Naomi huku akiendelea kumchezea Elibariki maungoni

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………….
Good
 
Huu uzi umetoka mwaka ambao nilikuwa naanza first year pale Teku baada ya kumaliza Diploma ya Uhasibu pale SEKOMU nikiwa nimetoka kupata stashahada ya useremala pale Nyerere Memorial
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom