Peniela (Story ya kijasusi)

Kwa mimi niliechelewa kuisoma imenilazimu kuitafutia season 5 humu JF baada ya kusoma season 1-4 huko kwenye Ngano app
 
SEASON 1
SEHEMU YA PILI
MTUNZI : PATRICK CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Tayari mtuhumiwa amekwisha ingizwa mahakamani na aliyekuwa akisubiriwa ni jaji anayeisikiliza kesi ile aweze kuingia na kuisoma hukumu.Wakati wakimsubiri Jaji aingie,Jason Patrick mwanasheria anayemtetea Penny alikuwa akibadilishana mawili matatu na mteja wake .
“ Jason,kabla hukumu haijaanza ninaomba nikwambie kitu.” Akanyamaza kidogo na kuendelea.

“ Nakushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia.
Umenisimamia katika kesi hii kwa kila namna ulivyoweza.Naju
a chochote kinaweza kikatokea siku ya leo hivyo nakuomba endapo ikitokea nikakutwa na hatia na kufungwa kifungo cha maisha au kifo uhakikishe yale yote niliyokuandikia katika karatasi unayatimiza.Wewe ni zaidi ya rafiki.Wewe ni ndugu yangu pekee ninayekutambua.Ninakukabidhi kila kilicho changu endapo mambo yataenda kinyume na matarajio yetu." Akasema Penny huku machozi yakimtoka

“ Penny naomba usikate tamaa hata kidogo.Nimepambana vya kutosha kuhakikisha kwamba tunashinda kesi hii lakini kama mambo yataenda tofauti na matarajio yetu hautakuwa ni mwisho.Nitapambana hadi nihakikishe haki imepatikana.” Akasema Jason na mara jaji akaingia.Wakati Jaji akiingia Penny akamnong’oneza Jason sikioni
“ I didn’t do it.I didn’t kill him”
“ I know Penny and I believe you” akasema Jason na mara mahakama ikaanza.”
ENDELEA…………………………..

Masaa manne yamekwisha katika sasa toka Jaji Elibariki alipoanza kuisoma hukumu .Ndani ya chumba cha mahakama kulikuwa na ukimya mkubwa kila mtu akifuatilia kwa umakini mkubwa kila alichokisema Jaji.Baada ya maelezo marefu kuhusiana na mwenendo mzima wa kesi ,hatimaye ukafika wakati wa kuhitimisha hukumu,wakati ambao ni mgumu kwa kila mtu mle mahakamani.Mke wa rais Dr Flora Joakin alishikana mikono na wanae Flaviana na Anna wakipeana moyo.Familia ya Edson halikadhalika walikuwa katika wasi wasi mkubwa kwani hakuna aliyejua jaji anakwenda kusema nini.

Toka alipoingia ndani ya chumba cha mahakama,Anna mtoto wa rais amekuwa akimtazama kwa hasira Peniela aliyekaa ndani ya kizimba kilichokuwa mbele kabisa ya mahakama.

“ Leo ndiyo siku yako ya mwisho kahaba wewe,mdanida waume za watu.Ndani ya muda mfupi ujao utayaanza maisha mapya gerezani paka wewe.Nilikuahidi kwamba utaozea gerezani na sasa utayaamini maneno yangu.Mwangalie kwanza alivyopauka na kukondeana kama muwa.” Akawaza Anna akiendelea kumtazama Penny kwa hasira
“ Ulinitenganisha na Edson mwanaume niliyempenda kuliko wote duniani.Urafiki wetu ulianza toka utotoni lakini ulivuruga kila kitu na mwishowe Edson akaniacha.Ninakuchukia wewe mwanamke na na laiti ningekuwa na uwezo ningekukata masikio “ Anna aliendelea kuwaza na akashindwa kuyazuia machozi kumtoka .Kitendo cha kumuona tena Peniela kilimrejeshea taswira ya Edson mwanaume aliywahi kumpena kupindukia.Akainama na kufuta machozi

Wakati kila mtu moyo ukimuenda mbio akisubiri maamuzi ya Jaji,Peniela alikuwa amefumba macho michirizi ya machozi ikionekana mashavuni pake.Alikuwa akiomba.

“ Ee Mungu baba,wewe ndiye mwenye uwezo wa kuona kila kitu hadi ndani ya mioyo yetu.Baba unafahamu sijatenda kosa hili ninaloshtakiwa nalo.Nimeteseka gerezani kwa mwaka mzima na hakuna anayeonekana kuniamini kwamba sikumuua Edson.Baba imetosha sasa na ninaomba kwa mapenzi yako itolewe hukumu ya haki”
Jason mwanasheria wake alikuwa amemuelekezea macho akimtazama na kumuonea huruma sana.

“ She’s Innocent.She didn’t kill him.Please Lord help her” akawaza Jason.Penny aliendelea kuyafumba macho yake machozi yakiendelea kumtoka na mikono yake akiwa ameifumbata kifuani .Jaji Elibariki aliendelea kumalizia kuisoma hukumu yake
Taratibu Penny alihisi miguu yake inaisha nguvu pale Jaji alipotamka kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kuithibitishia mahakama kwamba Penny alimuua Edson licha ya kuwasilisha ushahidi na vielelezo vingi.Jaji Elibariki alikwenda mbali zaidi na kuainisha namna ushahidi uliotolewa mahakamani ulivyokosa nguvu ya kuweza kumtia hatiani mshtakiwa kwa hiyo kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa anamuachia huru Penny.Alipotamka tu maneno hayo Penny akaanguka na kupoteza fahamu.

**********

Mtu wa kwanza kumtambua baada ya kurejewa na fahamu akiwa hospitalini alikuwa ni Jason mwanasheria wake.Mara tu alipopoteza fahamu baada ya Jaji kumuachia huru ,Penny alikimbizwa katika hospitali ya karibu kwa ajili ya huduma ya kwanza.

“ Jason ..!.akasema Penny kwa sauti dhaifu huku akitaka kuinuka lakini akashindwa mwili haukuwa na nguvu.
“ Penny relax ..!!!..Endelea kupumzika…” kabla hajamaliza sentensi yake Penny akapoteza tena fahamu.

“ Amepatwa na mstuko mkubwa huyu binti.Tunahitaji kumuweka hapa kwa muda tuendelee kumuangalia” akashauri daktari.
Jason Patrick mwanasheria anayemtetea Penny hata naye bado alikuwa katika kutoamini kama ni kweli Penny ameachiwa huru.Alifanya kazi kubwa ya kumtetea Penny lakini ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka ulikuwa mzito na uliotosha kabisa kumtia hatiani mteja wake.

Alimshukuru Mungu kwa muujiza ule mkubwa.Alimshuk
uru vile vile jaji Elibariki kwa maamuzi yale ya haki.
“ Haki imetendeka.Jaji Elibariki ameweka historia kwa kutoa hukumu ambayo wengi hawakuitegemea” akawaza Jason na mara daktari akamfuata na kumwambia kwamba kuna kundi la waandishi wa habari nje wanaohitaji kuongea na Penny.Akatoka na kwenda kukutana nao na kuwataarifu kwamba Penny hakuwa tayari kuongea na waandishi wa habari kwa wakati huo.

**********

Jaji Elibariki alipomaliza kutoa hukumu yake akatoka ndani ya mahakama huku nyuma yake akiacha vilio na mshangao kwa wengi hasa wale wa upande wa Edson.Asilimia kubwa ya wale waliokuwa waki fuatilia kesi ile waliamini kwamba lazima mahakama ingemkuta na hatia Penny. Flaviana mke wa Jaji Elibariki alikuwa amesimama amejishika kiuno asiamini kile kilichokuwa kimetokea

“ How could you do this to us Eli…!! Akasema kwa sauti ndogo na kupandwa na hasira alipomtazama mdogo wake Anna ambaye alikuwa ameanguka chini ameishiwa nguvu .Familia ya Edson nao hawakuamini kilichokuwa kimetokea.Walik

umbatiana na kulia kwa pamoja .Hawakuamini kama ni kweli mtu anayesadikiwa kumuua mtoto wao ameachiwa huru.
Dr Flora Joakim mke wa rais akakumbatiana na mama wa Edson na kumfariji akimuhakikishia kwamba huo haukuwa mwisho.Watapambana hadi haki ipatikane.

**********

Kitambaa cha mkononi cha jaji Elibariki kilikuwa kimeloa jasho lililokuwa linamtiririka kwa wingi licha ya ofisi hiyo kuwa na kipoza hewa.
“ I did it !!..” akasema kwa sauti ndogo
“ Nashukuru nimemaliza kesi.Penny hakuwa na hatia.Hakumuua Edson.” Akawaza huku akiendelea kujifuta jasho
“ Nimetoa hukumu ambayo wengi hawakuitarajia.Wengi waliamini lazima Penny angekutwa na hatia na kupewa adhabu kali akiwemo rais na familia yake.

Hata mke wangu akiwa ni sehemu ya familia ya rais naye alitegemea nimpatie Penny adhabu kali sana.Nimekwenda kinyume na matakwa yao kwa hiyo toka sasa nitaonekana msaliti na inanibidi kujiandaa kwa matatizo yatakayonikuta lakini sintoogopa kitu chochote kile kitakachonitokea kwa kuitenda vyema kazi yangu na wala sintafanya kazi kwa shinikizo la mtu au kikundi cha watu.Si rais wala mtu mwingine yeyote atakayenishinikiza nifanye atakavyo yeye” akawaza Elibariki na kujifuta jasho ,akainuka na kwenda dirishani akachungulia nje.

“Niliziona sura za familia ya mke wangu namna zilivyobadilika baada ya kutangaza kwamba Penny yuko huru.After today we’ll never be the same again” akawaza na mara sura ya Penny ikamjia, akatabasamu
“ Moyo wangu una furaha kwa kumrejeshea tena uhuru wake Penny ambaye ameteseka mwaka mzima gerezani bila hatia.Nisingeitendea haki taaluma hii kama ningekubali shinikizo la kumfunga maisha gerezani.”

Akainuka na kuanza kuzunguka zunguka mle ofisini
“ Kuna kitu nimekuwa nikijiuliza kwa mida mrefu bila kupata majibu.Ni kwa nini kumekuwa na shinikizo kubwa la kutaka Penny afungwe au ahukumiwe kifo? Toka ndani ya moyo wangu ninaamini kabisa Penny si muuaji wa Edson .Swali linakuja kama si yeye nani alimuua Edson? Akajiuliza Jaji Elibariki na kuvuta pumzi ndefu.Lilikuwa ni swali gumu lisilo na jawabu
“ Maswali haya ni magumu lakini yanahitaji majawabu.

Kesi tayari imekwisha lakini kuna kila ulazima wa kwenda mbali zaidi na kutafuta majibu ya maswali haya.Ninaamini kuna jambo linajificha hapa na bila kupata majibu ya maswali haya basi maisha ya Penny hayatakuwa salama.Kumuachia huru pekee haitoshi inabidi kuhakikisha pia na usalama wake baada ya kuwa huru.Atakuwa huru tukimpata muuaji wa Edson bila hivyo Penny atauawa tu” Akainuka na kwenda tena dirishani akachungulia nje

“ Sielewi ni kwa nini ninataka kujiingiza katika jambo kama hili ambalo ninajua lazima litaniletea matatizo makubwa lakini nafsi inanituma lazima nifanye hivi kwa ajili ya usalama wa Penny.Sina taaluma ya kuchunguza na kumpata muuaji lakini nitatumia kila mbinu ili niweze kufanikisha suala hili.I must dig deeper” akawaza Elibariki.

************

Ni saa tatu za usiku ,chupa ya mvinyo iliendelea kushuka taratibu.Toka aliporudi nyumbani Jaji Elibariki alikuwa amejifungia chumbani kwake akiendelea kupata mvinyo huku akitazama mpira katika runinga kubwa iliyokuwamo humo chumbani.Kazi kubwa aliyokuwa nayo usiku huu ni kupokea simu toka kwa watu mbali mbali marafiki zake waliokuwa wakimpongeza kwa hukumu ile ya kihistoria.

Wakati akiongea na mmoja wa rafiki zake simu nyingine ikaita,akatazama mpigaji alikuwa ni baba mkwe wake,Profesa Joshua Joakim rasi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

“ Kazi imeanza” akawaza na kumuomba samahani Yule rafiki yake aliyekuwa akiongea naye na kuichukua simu ile iliyokuwa ikiita akabonyeza kitufe cha kupokelea.

“ Hallo mzee” akasema Jaji Elibariki.Zikapita kama sekunde kadhaa akasikia sauti ya rais.Haikuwa ile sauti yake aliyoizoea kuisikia
Paniela
 
Back
Top Bottom