suala la biashara ya madawa ya kulevya au kulawiti watoto au kunajisi au jinai yoyote ila kamwe sio swala la kidini ni purely swala la kisheria, so Mwadhama Pengo ametajwa kuhusika na biashara hiyo haramu kwa mujibu wa sheria zetu, haitoshi tu kumtaja au kumtuhumu hapana, vyombo vinavohusika pamoja na waliomtaja wafanye uchunguzi wa kina wapate ushahidi wa kutosha then afikushwe mahakamani kujibu tuhuma hizo akishindwa ahukumiwe kwa mujibu wa sheria zilizopo, yeye kuwa kardinali hana kinga ya kutokufikishwa mahakamani na kamwe kanisa katoliki kalikuwahi kuhubiri watu watumie au waswambaze madawa ya kulevya wala maovu mengine yoyote. Kwa upande wa pili Mwadhama ni kiongozi wa kanisa katoliki Tanzania ambayo ni dhamana kubwa sana, kuhusishwa na madawa ya kulevya sii tuhuma ndogo, anatakiwa adhibitishe beyond doubt kuwa hahusiki, lakini hiyo haitoshi waliomchafua anatakiwa awatafute kwa kushirikiana na vyombo vinavohusika wafikishwe mbele ya sheria ili kumsafisha lakini pia kulisafisha kanisa ambalo kwa karibuni limekuwa kwenye kashfa nyingi sana.Niliwahi kumsikia Rais akisema viongozi wa dini wanajihusisha na madawa ya kulevya, hivi rais huyu aliapa kulinda na kutetea katiba yetu?? kama ndio mbona haitetei kwa kushindwa kuwafikisha watuhumiwa wa madawa kwenye vyombo vya sheria maana anawajua??