Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!


Sawa mama, lakini uje na verification ya taarifa hizo maana mtandao (internet) ni gate without gatekeeper. Kwenye mtandao kila mtu ni mwandishi, mhariri na mchapishaji.
 
Hawatweza hata siku moja kumkamata Kardinali pengo...
 

Nakuunga mkono sana mkuu tena pamoja na miguu, askofu Koda alijaribu kusema wanamuonea wivu kwa maendeleo mwisho wa siku kanisa lilimkamata live bila chenga na sasa yupo mafunzoni kuendelea kuisoma imani zaidi. Waache Jk na wezake siwanafikiri kwa urefu wa viatu vyao kumbe wenzao wanafikri beyond that. Big up man for good analysis.
 
Huwezi kulala kitanda kimoja na ng'e na usidungwe!@@@

.
Mmmmh. Unamaanisha wale top five kitaifa kabla hujamkuta Pinda mtu wa 6 kiwadhifa ni ng'e? Hebu tuweke wazi maana ya kauli hii mkuu, kwani utasaidia sana kuondoa utata wa tafsiri.
.
 
Sawa mama, lakini uje na verification ya taarifa hizo maana mtandao (internet) ni gate without gatekeeper. Kwenye mtandao kila mtu ni mwandishi, mhariri na mchapishaji.

suala la kunajis watoto hata intaneshno media wamelijadil,mfano BBC SWAHILI
 

wote ni binadam,je yule wa biafra c kiongoz wa kiroho?
 
[TABLE="width: 99%"]
[TR]
[TD]
Imeandikwa na Angela Semaya; Tarehe: 31st December 2011 @ 14:59
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo, amesema yeye si mfanyabiashara wa dawa za kulevya ila anatajwa kwa nia ya kunyamazishwa asizungumze ukweli.

Kardinali Pengo akizungumza na vijana katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Kawe jana alisema hajapata kuona wala kujua dawa za kulevya, lakini anajua anatajwa hivyo na wanaotaka anyamaze.

“Mimi mwenyewe nimewekwa katika orodha ya dawa za kulevya, naona kwenye vyombo vya habari, dawa zenyewe wala zisijui, lakini naendelea kuzungumza kwa sababu najua yanafanywa na wanaotaka kuninyamazisha … sitanyamaza ng’o,” alisema Pengo.

Alikuwa akiwaeleza vijana kuhusu utandawazi na kuwataka waache kuyumbishwa na kuamini kila wanachoona kimeandikwa kwenye mtandao.

Alisema mambo mengi ya ajabu yamekuwa yakiandikwa na kusemwa, lengo ikiwa ni kunyamazisha maaskofu na mapadri wasiendelee kufundisha ukweli, ili watu wachache wafaidike.

“Ni uzushi unaofanywa na watu kuharibu na kuchimbachimba Kanisa tusiseme ukweli, wachache waendelee kufaidika, naomba vijana msisombwe na hali hii, kwani watu hawa hawana woga ili mradi lengo lao la kuharibu Kanisa lifanikiwe … vijana mna uhai
ndani yenu na mna uwezo kama maaskari wa kupambana na waovu wa Kanisa,” alisema.

“Silaha ya vijana ni maisha yanayojua mnaamini kitu gani, msikubali kuyumbishwa na watu wanaotoa mambo vichwani mwao. Kama mnasikia natajwa, njooni mniulize, Baba mbona nimesikia habari fulani, badala ya kuyabeba na kushabikia…imani yenu si ya kutetereka, endeleeni kuwa imara watetereke wanaotaka tutetereke,” alisema.

Alisema vijana pia wamekuwa wakitumika kama vyombo katika biashara ya kulevya huku watu wachache wakitajirika na kwamba baadhi yao wanaokemea au kuzungumzia, wanapuuzwa au kuambiwa ndio wafanyabiashara wa dawa hizo, jambo ambalo nyuma yake halina ukweli wowote.

Kardinali Pengo alisema lengo ni kutaka kuwanyamazisha watu wanaosema ukweli ili wachache waendelee kutajirika na biashara hiyo kwa kuwatia hasara vijana.

Naye Mhashamu Askofu Salutaris Libena, ambaye aliongoza Ibada Takatifu, alisema vijana wamekutana ili kumshukuru Mungu na kumwomba neema .

Libena ambaye pia ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, aliwataka vijana kuingia mwaka mpya kwa kumjua na kumtukuza Mungu.

Mbali na vijana kushiriki ibada hiyo lakini pia zilikuwapo burudani mbalimbali za kwaya na ngoma, sambamba na vijana kupima kwa hiari damu kwa ajili ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Kila mwisho wa mwaka vijana kutoka makanisa mbalimbali ya Kanisa Katoliki hukutana kwa lengo la kumtukuza Mungu na kumshukuru kwa kumaliza mwaka.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
kanisa lina maadui wengi sana na maadui hao wameongezeka zaidi wakati huu wa propaganda za udini. Sheria ni msumeno kama kuna ushahidi unaojitosheleza kwamba pengo anauza madawa ya kulevya atiwe nguvuni na sheria ichukue mkondo wake. Viongozi wa dini hawako juu ya sheria.
 
What is wrong with Cardinal Pengo? Is water falling through cracks? Why taking a defensive position in public?
 

Na kuzungumza kwa mafumbo kwa bwana Pengo bila kutaja source ya habari zake je?
 
What is wrong witj Cardinal Pengo? Why does he take a defensive position? Is it a sign of being guilty? Just trying to think outside the box! He is my Cardinal and the red price whom I revere so much
 

bandika mama
 

Si kweli mbona lilishindwa kugundua maaskofu na mapadri walawiti watoto waliozagaa nchi nyingi mapema hadi likaingia aibu kubwa hadi kumfanya papa alie kuomba msamaha?
 
Utaratibu tuliojiwekea ni kwamba mtu ukitajwa tajwa basi unatakiwa kujivua gamba. Kwa hiyo Mhashamu Polycap Kardinali Pengo ametajwa tajwa kwenye madawa ya kulevya basi hana budi kujivua gamba asiendelee kulichafua kanisa la la mungu.
Utaratibu huo umejiwekea na nani? Kanisa katoliki au? Watu wengine bwana au umejiwekea na mkeo?
 
Inasikitisha sana kuona wanasiasa wa hii nchi hasa hasa wanamagamba wako tiyari kufanya chochote ili wabaki madarakani bila kujali athari ambazo zitawapata wananchi.Walaaniwe wana magamba!
 
Si kweli mbona lilishindwa kugundua maaskofu na mapadri walawiti watoto waliozagaa nchi nyingi mapema hadi likaingia aibu kubwa hadi kumfanya papa alie kuomba msamaha?
Kwanini aombe msamaha kama hajadhibitisha, huwa anahakiki akiona tuhuma za kweli ndo anaomba msamaha, bado inteligencial ya papa ni kubwa na kumbuka ni dunia nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…