Pengo: Polisi wanafuga wahalifu

Pengo: Polisi wanafuga wahalifu

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
By The Citizen Reporter|Dar es Salaam, Wednesday, 27 March 2013

Polycarp Cardinal Pengo yesterday accused the Police Force of failing to maintain law and order and prevent the killing of innocent people.
The head of the Catholic Church in Tanzania said in his Easter greetings that the government had an obligation to safeguard peace, and scoffed at assertions that "hooligans" were behind the recent spate of high-profile killings in the country.

"People are losing their lives, people are losing their property. The government should never keep quiet and think that religious leaders are better placed to deal with this worrying situation," he said.

He said religious leaders neither had the personnel nor power to arrest people who are wreaking havoc in society, adding that was the government's responsibility.

He said the government seemed reluctant to act as if it did not exist.
Cardinal Pengo recalled last month's assassination of Father Evarist Mushi in Zanzibar, saying police were quiet on progress made in investigations so far.

"I cannot say that I am satisfied with investigations into the killing of the priest...Tanzanians deserve to know what progress has been made in investigations.
"Neither I, Bishop Augustino Shao (of Zanzibar) nor any other religious leader has an update on the investigations. The authorities are silent," Cardinal Pengo added.

He said it was ominous when authorities charged with ensuring that the country remained peaceful were at the forefront of breaching that very peace.

Cardinal Pengo called for the need to have an open dialogue between the Muslim and Christian communities, and take measures to prevent further incidents.

But police spokesperson Advera Senso said yesterday that investigations into the killing of Father Mushi were continuing.
She appealed to the public to volunteer information that could lead to the arrest of the killers.

Following the priest's killing, the government, which called the assassination an act of terrorism, enlisted the help of the Federal Bureau of Investigation of the United States.

A sketch of one of the killers was released earlier this month. The portrait was based on eyewitness accounts.

Father Mushi was gunned down on February 17 as he was driving to mass at St Teresia Church on the outskirts of Zanzibar town.

Eyewitnesses said two people riding on a motorcycle called the priest by name and shot him three times when he opened the driver's window.
In February, a pastor with the Tanzania Assemblies of God (TAG), Rev Mathayo Kachila, was beheaded in Buseresere Town, Geita Region, during clashes blamed on religious conflict.

Last December, Catholic priest Ambrose Mkenda was shot and seriously wounded in Zanzibar.

Last year various churches in both Zanzibar and Tanzania Mainland were ransacked and burnt in incidents that stunned Christians and Muslims alike.

Dozens of people were arrested and charged in connection with the acts, which were condemned by political and religious leaders.

Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amelitupia lawama Jeshi la Polisi kwa kile alichosema kwamba limeshindwa kuzuia vitendo vya uvunjifu wa amani na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Kadhalika kiongozi huyo alihoji ulipofikia upepelezi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Zanzibar aliyepigwa risasi mwezi uliopita huku akisema, "Siwezi kusema naridhika au siridhiki lakini tulitegema kwamba polisi wangetegua kitendawili cha wauaji wa padri huyo."

Kardinali Pengo alisema Serikali haipaswi kusema wanaovuruga amani ni wahuni wakati hilo ni jukumu lake kuhakikisha inadumisha amani. Pengo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa salamu za Pasaka.

"Watu wanaharibiwa mali zao, watu wanapoteza uhai wao, Serikali haiwezi kukaa pembeni na kufikiri ni kauli za viongozi wa dini peke yao, viongozi wa dini hawana jeshi au hawawezi kukamata watu, Serikali ndiyo wana jukumu hilo kuhakikisha wanaingilia kati," alisema Pengo na kuongeza:"Wengine wanasema si mapambano ya dini ya Kikristu na Waislamu ila ni wahuni wachache wanajichukulia madaraka, lakini lolote liwavyo Serikali haiwezi kukwepa majukumu yake, hatuwezi kutegemea nchi itawaliwe na wahuni kama vile Serikali haipo."

Kuhusu Padri Mushi aliyepigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akijiandaa kwenda kwenye misa huko Zanzibar, Pengo alisema:

"Watanzania tungeambiwa zimechukuliwa hatua zipi na aliyehusika na mauaji hayo ni nani, lakini hali inayoonekana sasa hatujui."
Aliongeza: "Siyo mimi wala Askofu wa Zanzibar (Augostino Shao) au askofu yeyote anaweza kukwambia kuwa kuna mtu amekamatwa, ila inaonekana kama mambo yanataka kuisha kimyakimya na kufanya hivyo haiwezi kuwa chimbuko la amani."

Kardinali Pengo alisema vyombo vya kulinda amani vinapokuwa chimbuko la kuharibu amani kwa vyovyote nchi yoyote duniani haiwezi kuendelea. Alisema kunahitajika kukutanishwa kwa pande zote mbili za Wakristu na Waislamu, lakini akatoa angalizo kwa kubainisha mambo mawili ambayo yanahitajika kuzingatiwa ili kufikia mwafaka.

Alisema pande zote mbili watu wakitaka kujadiliana ni lazima kila upande uwe tayari kujadiliana na kupokea ukweli sambamba na kusema ukweli na siyo kupotosha ukweli kwa masilahi binafsi.

"Pili kila upande uwe na mawazo kwamba upande wa pili una nia njema, lazima watu wawe tayari kuwasiliana kuwa upande wa pili una nia njema, lakini kinyume na hapo itakuwa bure na kudanganyana na mambo yataendelea kuwa mabaya zaidi," alisema Kardinali Pengo.

Kuhusu kuwapo kwa taarifa kwamba katika mkesha wa Pasaka kuna watu watafanya vurugu, alisema haogopi kwani vyombo vya usalama vina jukumu la kuhakikisha raia wanakuwa salama."Mimi kazi yangu si kujiandaa kushika bunduki kwani Serikali wana jukumu la kulinda amani iwe kanisani au msikitini.

"Wanatakiwa kuchukulia mazungumzo hayo ‘serious' (makini) kwani baada ya Padri Ambrose kujeruhiwa kwa risasi walisema wataendelea na kweli ikatokea Padri Mushi akauawa. Mimi sitaacha kwenda kanisani hata kama nitaambiwa nitauawa na kama kufa nife katika kanisa langu," alisema.

Polisi wanena
Msemaji Mkuu wa Polisi, Advera Senso alisema upelelezi wa tukio la kifo cha Padri Mushi unaedelea na kuwaomba wananchi kusubiri kujua kinachoendelea.

"Kunapotokea tukio la aina yoyote lile polisi ndiyo jukumu lao kujua chanzo na hatua za kuchukua. Tunaomba watu tuwaachie wanaohusika ili kuweza kufanya kazi hiyo vizuri na tutawaeleza kinachoendelea upelelezi utakapokamilika," alisema Senso.

Kuhusu uvumi wa matukio ya uhalifu wakati wa Pasaka, Senso alisema wanafuatilia taarifa hizo.

"Tunawaomba wananchi ambao wanajua ni kina nani wanaeneza taarifa hizo, watupe ushirikiano ili tuwachukulie hatua kutokana na kutoa taarifa za kuhatarisha usalama wa wananchi," alisema Senso.

Pia Novemba mwaka jana, Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Fadhili Soraga alimwagiwa Tindikali na watu wasiojulika wakati akifanya mazoezi kwenye Viwanja vya Mwanakwerekwe.

Mapema mwezi ulipita, Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (TAG) mkoani Geita, Mathayo Kachila aliuawa katika ugomvi wa kugombea kuchinja, katika tukio ambalo watu sita walijeruhiwa vibaya kwa mapanga.

Source:Gazeti la Mwananchi.
 
Kweli kabisa, hapo hapo utasikia wakiibuka wanaziomba taasisi za dini ziombee amani ya nchi.
 
Cardinal Pengo called for the need to have an open dialogue between the Muslim and Christian communities, and take measures to prevent further incidents.

sijawahi kukubaliana na pengo hata siku moja ila leo kwa mara ya kwanza nasema yes. kwenye red hapo ameongea point. watanzania tujua amani ya nchi yetu ipo mikononi kwa dini hizi mbili. wala sio ccm, chadema au cuf inayoweza kuleta amani. ni ukweli uliodhahiri kuwa hata uhai wa chadema kwa asilimia kubwa unategemea ukristo vile vile kwa cuf kinyume chake.
hatutaki bakwata peke yao wala wakatoliki peke yao. bali taasisi zote zihusishwe na sio kundi la watu bali watu wachache wenye uelewa. wajadili mambo kwa kuangalia kizazi cha leo na kijacho. kusiwepo na seggregation ila kila mwenye wazo ato akiwemo shekh Ilunga, atoe dukuduku zake zote hapo ili zipatiwe suluhisho, na baada ya hao kauli kama zake zifikie mwisho.
binafsi naona kama vile hili wazo limechelewa. lilitakiwa liwepi miaka 30 iliyopita. tumeona mengi ya mwembechai, zenji, buseresere na kwingeneko basi liwe funzo kwetu.
WELL SAID ASKOFU PENGO.
 
Nilisoma mahala kuwa kuna mchungaji wa assemblies church alitekwa na hajajulikana alipo.
Serikali yetu sikivu. Inasikiliza lakini kutenda haiwezi katu. INASIKILIZA just like everybody else. Ngoja sasa Pinda arudi na tamko, hakawii kulia machozi na kusisistiza naye ni mkatoliki na amesikitishwa mno mno!
Crass!
 
A point of correction: PENGO IS IN NO WAY THE HEAD OF THE CATHOLIC CHURCH IN TANZANIA. Canon law does not stipulate that a person becomes the head of the church in a particular country by being created a CARDINAL.

We have HEADS of local churches (BISHOPS OF PARTICULAR DIOCESES) and the church's spokesperson in Tanzania who is THE PRESIDENT of Tanzania Episcopal Conference. Presently is Rt Rev Tarcisius Ngalalekumtwa the Bishop of the Catholic Diocese of Iringa.

Be well versed before you write awkwardly!
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuelezwa hatua zilizochukuliwa kwa watuhumiwa waliohusika na matukio ya kudhuru viongozi wa kidini visiwani Zanzibar.

Kauli ya Pengo inakuja huku mapadre wawili wa Kanisa Katoliki wakiwa wameshambuliwa kwa risasi pamoja na Katibu wa Mufti wa Zanzibar naye akimwagiwa tindikali usoni na watu wasiofahamika.

Katibu huyo wa mufti alimwagiwa tindikali hiyo Novemba mwaka jana, huku Padre Ambrose Mkenda akijeruhiwa kwa risasi Desemba 26 mwaka huo, na mapema mwaka huu, Padre Evarist Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi.

Pamoja na Jeshi la Polisi nchini kuunda kikosi maalumu kuchunguza matukio hayo, hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu uchunguzi huo jambo ambalo linamtia shaka Kardinali Pengo kutokana na ukimya huo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa salamu za Pasaka, Kardinali Pengo alisema kuwa kuchoma makanisa, kubomoa na kuharibu nyumba za ibada ni hali isiyoridhisha.

“Tumeishi Waislamu na Wakristo kwa muda mrefu bila kukwazana wala kugombana, napatwa na wasiwasi ikiwa hali hii imeanza kujitokeza sasa na watu wanadai ni kundi la wahuni, serikali haiwezi ikaepa majukumu yake,” alisema.

Aliongeza kuwa ama wawe wahuni au watu wengine, serikali haiwezi kutawaliwa na wahuni.

Alisema kuwa wanahitaji kukutana na viongozi wa pande zote mbili ikiwemo serikali ili kupata ufumbuzi wa yaliyotokea.

“Serikali haiwezi kukaa pembeni, pale tutakapokutana tunahitaji mawasiliano na majadiliano. Wanaofanya vitendo hivyo hawana jeshi, sasa ni muhimu kukutana wote na lazima watu wawe tayari kupokea ukweli na kusema ukweli, lakini pia kila upande uwe na mawazo kuwa upande wa pili una nia njema, amani haiji kwa mapambano wala mtutu wa bunduki,” alisema.

Kardinali Pengo alisema kuwa serikali ina jukumu la kulinda amani na kuchukulia hatua mazungumzo yoyote yanayotolewa hasa yakiwa ya vitisho.

Kuhusu madai ya baadhi ya watu kupokea ujumbe wa vitisho kuhusiana na ibada ya Pasaka, alisema: “Sitaacha kwenda kanisani kama kufa nife nikiwa kanisani hiyo ni juu ya serikali.”
 
hakuna kitu kama hicho,rudia kuisoma hiyo mdau,
Yule mchungaji ametoweka,na hakuna uthibitisho kama ameuawa au amejificha,,,,,
 
Ni kweli lakini tusisahau na yule shekhe aliuawa kwa kupigwa mapanga kipindi sambasamba na mauaji ya padri Mushi.Nashangaa huyu hatajwi au kundi lake halijali kilichotokea? Nashauri mtu anaemua ugomvi wa watoto wa2 asimkamate mkono m1wapo na kumpa nafasi mwenzake kupata nafasi kuendelea kurusha makonde,CJUI NIMEELEWEKA?
 
Mwaka 2015 si vibaya Pengo akachukua maamuzi ya kugombea nafas ya kisiasa,it seems siasa anaziweza sana kuliko utumishi wa mungu,
Mtikila ameweza yeye atashindwaje?
 
Ni kweli lakini tusisahau na yule shekhe aliuawa kwa kupigwa mapanga kipindi sambasamba na mauaji ya padri Mushi.Nashangaa huyu hatajwi au kundi lake halijali kilichotokea? Nashauri mtu anaemua ugomvi wa watoto wa2 asimkamate mkono m1wapo na kumpa nafasi mwenzake kupata nafasi kuendelea kurusha makonde,CJUI NIMEELEWEKA?

umeeleweka ila Pengo na wafuasi wake hawatakuelewa,maana yule ni Shekh na hao waliodhuliwa na kuuawa ni MAPADiRI
 
Ni kweli lakini tusisahau na yule shekhe aliuawa kwa kupigwa mapanga kipindi sambasamba na mauaji ya padri Mushi.Nashangaa huyu hatajwi au kundi lake halijali kilichotokea? Nashauri mtu anaemua ugomvi wa watoto wa2 asimkamate mkono m1wapo na kumpa nafasi mwenzake kupata nafasi kuendelea kurusha makonde,CJUI NIMEELEWEKA?

Yule alikuwa imam, mkuu! Na aliuawa na wezi wake wa nazi!
 
Police haven't failed. It's too early to accuse them of that.
What you dont know, like a dark night, Waliohubiri kuwauwa mapadre, wakatengeneza kanda, hadi wakatangaza kwenye mitandao ya u tube hawakuwahi kukamatwa, ya Wilfred imewekwa siku moja tu kwenye mtandao na akakamatwa, Usitumie kichwa kufuga nywele bibie.
 
A point of correction: PENGO IS IN NO WAY THE HEAD OF THE CATHOLIC CHURCH IN TANZANIA. Canon law does not stipulate that a person becomes the head of the church in a particular country by being created a CARDINAL.

We have HEADS of local churches (BISHOPS OF PARTICULAR DIOCESES) and the church's spokesperson in Tanzania who is THE PRESIDENT of Tanzania Episcopal Conference. Presently is Rt Rev Tarcisius Ngalalekumtwa the Bishop of the Catholic Diocese of Iringa.

Be well versed before you write awkwardly!

Well said.
Wengi wanapotoka wanaposema Mkuu wa Kanisa katoliki Tanzania ni Kardinali Pengo, si hivyo. Cheo chake ni heshima aliyo nayo kuingia katika timu ya baraza la Pope kule Vatican. Tanzania haina Mkuu wa kanisa tanzania, ila kila jimbo lina mamlaka yake na kila jimbo linawajibika kwa Pope ndio maana kila baada ya miaka mitano kila askofu huenda Vatican kukutana na Pope.
 
Back
Top Bottom