Pengo: Nimesamehe

HApo ndipo mahakama ya kadhi ilipo tufikisha. Waisilamu na wakristo hawaelewani, wakristo kwa wakristo hawaelewani ni matusi kwenda mbele.

Mie nauliza, hawa waislamu na wakristu/wakristo kwa ujumla wao ni asilimia ngapi ya watanzania? Kwani hakuna imani tofauti na hizo hapa nchini?
 
Naogopa kusema ninachohisi kumkuta gwajima ,
Mh sijui kama mapambazuko tutazungumza.
 
I trust Satanic Verses are true and very real.Lets see who more or less Lucifer first Born?
 

niwemugizi huyuhuyu jembe au????
 

Where is TEC mentioned in the canon law?
 
Tatizo watu wametekwa na siasa, hawataki kuambiwa ukweli hata kidogo. Mahaba ya siasa ndio yanayowafanya wamtukane Pengo na kuona kakosea alichokisema. Pengo kama Kardinali wa kanisa Katoliki Tanzania, hawezi kuona mambo yanaenda kinyume halafu akakaa kimya, haiwezekani.

Kanisa halijafikia hatua ya kufanya maamuzi kwa niaba ya waumini wake, kanisa halijafikia hatua ya kulazimisha watu katika suala linalohitaji haki na uhuru wa mtu. Kumwambia mtu lazima akapige kura ya hapana hiyo si sawa hata kidogo, na hata kumwambia mtu lazima akapige kura ya ndiyo nayo si sawa hata kidogo.

Mtu anapaswa kupiga kura kwa mujibu wa maamuzi na matakwa yake binafsi na si kulazimishwa. Ni sahaihi kuwaelimisha watu mazuri na mabaya ya katiba pendekezwa lakini si sahihi kuwapangia watu kura ya kupiga
 
Ni kiongozi wangu lakini sijapenda lugha yake ya ki-ccm ya kwenda kinyume na maaskofu wenzake. Asante Gwajima kwa kumpasha. Zaidi ya kumsamehe angemfanya nini? Haya, amemsamehe sawa lakini ujumbe ameshaupata. Aache kiherehere cha kuupigania ujinga unaofanywa na Serikali hii ovu! Tunataka katiba yenye manufaa kwa wote na mahakama ya kidini isiwe katika mikataba nyeti ya serikali isiyo na dini.
 

Msamaha wa pengo hauna uhusiiano na utendaji wa serikali na majumukumu ya sheria.
Unapo shauri sheria imsamehe muhuni kama huyu gwajima utaifanya sheria iruhusu wajinga wanaotafuta umaarufu kupitia migongo ya viongozi kama kadinari kuendelea kutusi wazee wetu wakijua kuna misamaha wataipata.
Mm sio mkiristo lakini sioni sababu ya gwajima kupata msamaha wa serikali.
Kadinari pengo anahitaji pepo utukufu wa milele anahaki yakusamehe kwakuwa mungu humpenda anae samehe.
Lakini serikali haihitaji pepo wala utukufu wa milele yenyewe inahitaji kusimamia sheria na kuzitekeleleza hiyo ndio sifa ya serikali bila kujali sheria inamkabili nani.
Ni muhim gwajima awe mfano wa wapuuzi wengine wanao tamani kufanya upuuzi kama alio ufanya gwajima.
Nilishangaa sana alipo jitetea akijifananisha na askofu pengo.
Nilijiuliza tokea lini sisimizi anajifananisha na tembo.
Ivi gwajima kapewa nanani uwaskofu mpaka ajifananishe na uaskofu wa pengo?
Lazima serikali isimamie sheria wahuni aina ya gwajima wasisubutu kututukania wazee wetu.
 

mi mwenyewe ni mkatoliki, lakin alichokifanya pengo si kizur, huwezi ukaja kuukana walaka ambao tayar umesha usaini (umuridhia), angefanya hivyo <kuukana> kabla ya kuusaini.Ni upuz
 

Una point mkuu. Lakini hiyo sharia inafanya kazi hapo kwa Pengo tu? Mbona haikuwa na meno kwa wengine kama pale alipopigwa kofi Warioba na kutukanwa, na pale Lowasa anapotukanwa na kina Nape na yule Malecela motto na yule aliyezawadiwa ukuu wa wilaya ya Kinondoni? Au sharia inafanya kazi pale tu anayeguswa anapokuwa kipenzi cha waziri mkuu?
 

Ingekuwa vyema zaidi kama angeenda mbali zaidi ili kuifuta kesi polisi alikopeleka malalmiko yake.Huo ndiyo utakuwa msamaha wa kweli.Kama alivyofanya Hayati Pope Paul II
 
Ingekuwa vyema zaidi kama angeenda mbali zaidi ili kuifuta kesi polisi alikopeleka malalmiko yake.Huo ndiyo utakuwa msamaha wa kweli.Kama alivyofanya Hayati Pope Paul II

mkuu nikutoe hofu tu mwadhama hajapeleka malalamiko ya polisi ni mihemuko tu ya polisi wetu unless Kama polisi wanajambo nyuma ya pazia
 
mkuu nikutoe hofu tu mwadhama hajapeleka malalamiko ya polisi ni mihemuko tu ya polisi wetu unless Kama polisi wanajambo nyuma ya pazia

Hata kama hajatoa since ameishamsamehe anajukumu la kwenda kuifuta ,ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi.Hasa kwa vile yeye kama kiongozi wa dini na anajua umuhimu wa kusamehe mara sabini wa sabini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…